Kifahamu kisa cha Giuseppe Veraldi

Military Genius

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
760
1,445
IMG-20200412-WA0054.jpg


February 1936 mwili wa mwanaume Giuseppe Veraldi maarufu kama Pepe ulipatikana chini ya daraja huko Catanzaro Italia, ilionekana kuwa aliruka kutoka kwenye daraja na kichwa chake kujibamiza kwenye chuma na kufa.

Uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa Pepe alikuwa amejiua mwenyewe lakini familia yake haikukubaliana na majibu hayo kwa sababu hakukuwa na viashiria wala sababu zozote za Pepe kujiuwa.

Miaka mitatu baadae January 1939 msichana Maria Talarico alianguka na kupoteza fahamu wakati akitembea darajani hapo karibu na eneo mwili wa Pepe ulipokutwa miaka mitatu nyuma, fahamu zilipomrejea alikuwa amepelekwa nyumbani tayari, akaanza kuzungumza sauti nzito ya kiume.

Sauti hiyo ilidai kuwa yeye ni Pepe aliyefariki miaka mitatu nyuma, na anataka kuongea na mama yake, akatoa na maelekezo anakopatikana. Wakati mama yake Pepe Catarina Veraidi anatafutwa, Maria akaomba apewe divai, sigara na karata za kuchezea, akawaalika watu walikuwepo hapo wacheze mchezo huo wa karata.

Mama hakwenda mwenyewe, alikuwa na hofu, akaongozana na wanaume watatu waliokuwa marafiki wa Pepe wakati huo, baada ya kufika akastaajabu kuona sauti ya mwanae Pepe inasakikila kwa binti Maria.

Sauti hiyo ilisema kuwa marafiki zake walimpiga, wakampeleka darajani na kumuuwa kwa kumpiga na chuma kichwani, akawataja na marafiki hao. Baada ya kumaliza binti aliondoka, akaenda hadi darajani tena, akalala na sauti hiyo ikamuondoka. Maria aliamka bila kumbukumbu yoyote ya kilichotokea.

Miaka 9 baadae mwaka 1948 mama alipokea barua kutoka kwa Luigi Marchete aliyekua mmoja wa marafiki wa mwanae aliyetoroka Italia na kwenda Argentina baada ya Pepe kufariki, barua hiyo ilionyesha anakiri kuwa alimuuwa Pepe kwa wivu wa mapenzi kwa mwanamke, haikujulikana kilimkuta nini.

Maelezo mengi ya barua hiyo yalifanana na naelezo aliyoyatoa mtoto Maria miaka 9 iliyopita kwa kutumia sauti ya Pepe. Japo walikuwa katika mji mmoja lakini Maria hakua anafahamiana na mama yake Pepe.

@military_Genius
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom