Ganvie ni kijiji kilichopo kwenye ziwa huko nchini Benin ambacho kiko katika Ziwa Nokoué, karibu na Cotonou. Kikiwa na idadi ya watu karibu 20,000, kikielezwa kuwa huenda kikawa ndio kijiji kikubwa zaidi kilichopo kwenye ziwa barani Afrika na ni maarufu sana kwa watalii.
Kijiji kiliundwa mnamo karne ya kumi na sita kuelekea karne ya kumi na saba na watu wa Tofinu ambao walikwenda ziwani kuepuka wapiganaji wa Fon ambao walikuwa wakikamata watumwa kwa kuuza kwa wafanyabiashara wa Ulaya hivyo walikimbilia sehemu ambayo walikuwa hawawezi kufikiwa kwa urahisi kipindi hicho.
Unaambiwa kuwa licha ya kukimbilia huko watu hawa kutoka kabila la Tofinu walijitahidi kukifanya kina cha ziwa hilo kuwa kirefu na visiwa vya Ziwa Nokoue na wakategeneza bandari yao maalumu. wanakijiji wa Ganvie mara nyingi huitwa “watu wa maji” na eneo lenyewe mara nyingi huitwa “Venice ya Afrika.”
Hapo awali walitegemea kilimo, ingawa kwa sasa kazi kubwa inayowapatia kipato kikuu za kijiji hicho ni utalii, uvuvi na ufugaji wa samaki. Njia pekee ya kusafirisha kwenda na kurudi kijijini ni kupitia boti za mbao.
Unaambiwa watu wanapenda kwenda kutalii katika kijiji hicho sio tu kwamba ni kizuri bali kuwaona watu wanaoishi katika eneo hilo pia jinsi maji yalivyokuzunguka na njia zao/vyombo vya usafi ambavyo ni boto za mabo.
Kinaitwa kijiji cha maji au kijiji cha maajabu