Kifahamu Chakula cha Ajabu kutoka Ufilipino Kinachoitwa Pagpag

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,090
Ulimwengu wa upishi umekuwa ni darasa kubwa ambalo watu hutumia kujifunza utamaduni na hata wengine kujipatia nafasi ya kuingiza kipato, ila wapo wanaovutika kutokana na ubunifu na pamoja na utamaduni za jamii mbalimbali, na hivyo maarifa kadhaa ya upishi yanasambaa zaidi. Walakini, mara kwa mara, vyakula fulani vimekuwa ni vya kipekee, na kugonga vichwa vya habari duniani. Ukienda Ethiopia wapo wana Tera Sega, ambayo ni nyama mbichi kabsa na nchi nyingi za Afrika zimetumia Panya kama kitoweo safi kabsa, ukienda kwa Wajapani kuna Basashi ambayo pia ni nyama ya farasa mbichi.

grilled-rice-field-rat-with-salt-and-chili-1-rotated.jpg


Hivyo ni wazi kila jamii ina mila na desturi zake linapokuja suala la chakula. Sasa huko Ufilipino kuna msosi mmoja unaojulikana kama Pagpag ni msosi ambao umejizolea umaarufu sana. Ni chakula cha ajabu sana ambacho ni maarufu kwa watu wa hali za chini, ila chakula hiki kimekita mizizi yake katika historia ya Ufilipino toka zamani na mpaka sasa watu hupendelea sana kula msosi huu.

screen-shot-2013-06-02-at-14-32-09.png


Pagpag inatokana na neno la Kifilipino "pagpagaw," ambalo hutafsiriwa kwa maana ya "kutetereka ama kutikisika." Neno hilo linarejelea mchakato na hatua za uandaaji wake kwani kuna shughuli ya kuponda ponda chembe za chakula kutoka kwa mabaki ambayo hutolewa kutoka kwa sehemu za kuhifadhia takataka au chakula ambacho kimetupwa, kifupi ni kwamba chakula hiki hutoka jalalani. Baada ya kuondoa uchafu, mabaki huoshwa, kisha hukupikwa, na kutengenezwa upya.

337848-620x430-1-79q0nb39pbyvx8q66q3csjoosvfz3uc16uy6pnto400.jpeg

Asili ya chakula cha Pagpag imeanzia mbali sana na inahusika moja kwa moja na watu wanaoishi katika maeneo maskini ya Ufilipino, kama vile Lanao del Sur, Sulu, Saranggani, Northern Samar, Maguindanao, Bukidnon, Sultan Kudarat, pamoja na Agusan del Sur. Ni ngumu kukutana na raia anayeishi Cebu, Batangas, Bukidnon, Surigao Del Norte, Isabela, au Cavite akitumia chakula cha Pagpag, yaani huko ndo wanapoishi wenye uwezo.

ZvlRgXjqAJybFai-800x450-noPad.jpg

Licha ya asili yake isiyo ya kawaida na yenye kutia shaka sana, Pagpag inashikilia nafasi ya kuvutia kwa kiwango kikubwa cha Matumizi katika historia ya Ufilipino, ikitumika kama ishara ya ustadi katikati ya dhiki, yaani palipo na dhiki basi watu walitafuta njia ya kuibadilisha dhiki na kuwa neema kwao.

Hata hivyo, ni muhimu kukubali kuwa kuna hatari za kiafya zinazohusiana na utumiaji wa chakula hiki cha Pagpag. Ukweli kwamba chakula hiki ni matokeo ya mabaki ya chakula ambayo yametupwa kwa sababu zinazohusiana na usafi na usalama hivyo kuongeza wasiwasi kuhusu magonjwa yanayoweza kutokea. Licha ya jitihada za wapishi katika kusafisha kabisa na kupika viungo, bado kuna hatari kubwa ya magonjwa na uchafuzi wa chakula.

unnamed.jpg


Kwa kumalizia, Pagpag, chakula cha kipekee kutoka Ufilipino, inafichua hali halisi yenye changamoto zinazokabili jamii zilizotengwa haswa za masikini wenye hali duni. Kutokana na ulazima, vyakula hivi visivyo vya kawaida vinasimama kama ushahidi wa ustahimilivu wa watu wa Ufilipino na ustadi wao katika kukabiliana na dhiki. Ingawa inaweza kuwa jambo lisilo la kawaida la kitamaduni na kivutio cha watalii au watu wan chi nyingine ila Pagpag ni chakula kizuri kwa masikini, ni muhimu kutambua masuala ya kimsingi ya kijamii ambayo inaakisi.
Karibu tule Pagpag!
 
Ohhh niliona youtube channel moja hivi, huyo mama anapika chakula kutokana na uchafu wa mabaki ya kuku kutoka kwenye migahawa kama hii ya KFC na inayofanana na hiyo.

Kwahiyo na yeye ana dishes zake, ambazo ni fried, stew etc 😯
 
Ohhh niliona youtube channel moja hivi, huyo mama anapika chakula kutokana na uchafu wa mabaki ya kuku kutoka kwenye migahawa kama hii ya KFC na inayofanana na hiyo.

Kwahiyo na yeye ana dishes zake, ambazo ni fried, stew etc 😯
Ila ajabu ni kuwa huwezi kukutana na chakula hiki sehemu ya town center :D
 
Duh. Inashangaza!

....Hata hotdog ya wazungu ni mabaki baki ya mafuvu ya kuku, ng'ombe, nguruwe, misuli, utumbo n.k yaani ni yale mabaki ya buchani yanachakachuliwa, kusagwa, kupondwa pondwa halafu wanaongezea spices....viola!

Kitu na boksi.

Walakin hili la pagpaw sijawahi kusikia.

Bora sie wala ukoko wa wali wa nazi.😝🤩
 
kuna sehemu niliikuta hii comments za watu ndio zilikuwa zinachekesha balaa.

jamaa mmoja akaandika"nilidhani wahindi wanakula vyakula vyenye ukakasi kwa wengine kumbe nilikuwa najidanganya"
hapa akimaanisha india wana street food kama kwetu kwenye vituo vya daladala na misosi ya meza,kukuta mtu anauza juice ya maembe imejaa maiti za nzi ni kitu cha kawaida tu na wala sio shida kwao.

ila hapa jamaa alisanda.
Your friend shared this video with you. Watch it now!
View: https://www.tiktok.com/@housegotcontent/video/7319909064916487457?_r=1&u_code=dece7c9h8743lc&preview_pb=0&sharer_language=en&_d=ebfld5ad4h5k3a&share_item_id=7319909064916487457&source=h5_m&timestamp=1707808524&user_id=6871304716488311813&sec_user_id=MS4wLjABAAAAH00eKrzTUWc-gEjdBvbYbl6Yj_3gBx156eBzsaxputeAusKt2CXZx7wGXlX2Xtb2&social_share_type=0&utm_source=copy&utm_campaign=client_share&utm_medium=android&share_iid=7334675317721138949&share_link_id=c27a975f-4564-4c0f-8323-83df377ca6fe&share_app_id=1233&ugbiz_name=MAIN&ug_btm=b6880%2Cb2878&enable_checksum=1
 
Ohhh niliona youtube channel moja hivi, huyo mama anapika chakula kutokana na uchafu wa mabaki ya kuku kutoka kwenye migahawa kama hii ya KFC na inayofanana na hiyo.

Kwahiyo na yeye ana dishes zake, ambazo ni fried, stew etc 😯
Kuna mwenzio akija Bongo atashangaa watu wanapamba foleni kwenye mishkaki ya vichwa vya kuku na Miguu ya kuku, Mbagala moja hio
 
Duh magonjwa vipi?
Nilipita jalala moja lililopo soko Kuu. Niliona jamaa anafakamia maembe, ndizi na mabaki mengine ya matunda yaliyokuwa yanaanza kuoza. Nikamuuliza kama haogopi kipindupindu. Alinijibu huku akicheka kicheko cha dharau "hebu jaribu na wewe uone" Nilichoka.
 
Kuna documentar moja niliiona ITV watoto wanaokota mifupa ya mabaki ya nyama pale mnadani Msalato Dodoma wanapeleka nyumbani kwa ajili ya mboga ya kulia ugali,mifupa inaoshwa na kupikwa mboga ya kulia ugali. Na wanatumwa na wazazi
 
Kuna documentar moja niliiona ITV watoto wanaokota mifupa ya mabaki ya nyama pale mnadani Msalato Dodoma wanapeleka nyumbani kwa ajili ya mboga ya kulia ugali,mifupa inaoshwa na kupikwa mboga ya kulia ugali. Na wanatumwa na wazazi
Aisee mbona ni hatari sana
 
Back
Top Bottom