Kidumu Chama cha Mapinduzi

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,897
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NI BABA LAO

Kama inavyofahamika na Watanzania wote, tarehe TANO ya mwezi wa PILI ya kila mwaka, Chama cha Mapinduzi (CCM) huadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Hii inatokana na kwamba Chama cha Mapinduzi kilizaliwa tarehe 05/02/1977 baada ya kuunganisha vyama viwili vya TANU na ASP, hivyo kwa sasa kimefikisha umri wa miaka 43.

Kama angekuwa binadamu, tungesema amefikisha umri wa mtu mzima ambao unamfanya aendelee kuheshemika katika jamii inayomzunguka.

Ndivyo ilivyo kwa CCM ambayo imejijengea heshima kubwa kwa Watanzania kutokana na kazi kubwa iliyofanya hasa ya kutunza AMANI na kuleta MAENDELEO makubwa ya kiuchumi yaliyopo hapa nchini.

Kama ulikuwa hujui, naomba uelewe kwamba CCM ndio chama pekee kilichoongoza nchi tangu uhuru, wakati huo kikiitwa TANU.

Ni chama kikongwe hapa nchini na kimefanya mambo makubwa sana yaliyoshuhudiwa na kunufaisha vizazi vingi hapa nchini. Hivyo, CCM kinaheshimika si tu hapa nchini, bali Afrika nzima na duniani kote.

Je, chama gani kingine hapa nchini kinaweza kulinganishwa na CCM? Hakuna hata kimoja kinachoweza kufananishwa na CCM. NI DHAHIRI, CCM NI CHAMA KUBWA, NI BABA LAO.

BAADHI YA MAMBO MAKUBWA AMBAYO CCM INAJIVUNIA KUYAFANYA:

1. CCM imeleta AMANI na MAENDELEO kwa nchi yetu na watanzania kwa ujumla. Maendeleo yaliyoletwa na utawala wa CCM ni pamoja na elimu, afya, uchumi, miundombinu, usafirishaji, nk.

Hakika maendeleo yaliyopo hapa nchini ni kutokana juhudi za uongozi bora na imara wa Chama Cha Mapinduzi.

2. CCM imekuwa BABA wa DEMOKRASIA hapa nchini. Hakuna chama kingine chenye demokrasia inayoeleweka kama Chama Cha Mapinduzi.

Tangu enzi za Uhuru wa Tanganyika chini ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere hadi wakati huu chini ya Dr. John Pombe Magufuli, CCM imekuwa ikibadilishana uongozi kwa amani bila ukabila wala mizengwe.

Hii inadhihirisha pia kwamba, misingi iliyowekwa na waasisi wa chama imekuwa ikizingatiwa na viongozi wa awamu zote. Kwamba, MTU yeyote ndani ya CCM anaweza akawa kiongozi ili mradi anazo sifa stahiki za kuwa kiongozi.

Na huo ndo umekuwa utamaduni wa muda mrefu ndani ya CCM, ambao kimsingi umesaidia kuleta usawa na heshima ndani ya chama.

3. Kuthibitisha kuwa CCM ni baba wa demokrasia hapa nchini, mwaka 1992 kiliruhusu mageuzi ya kisiasa kutoka chama kimoja na kuwa vyama vingi.

Lengo la mageuzi haya ya kisiasa lilikuwa kuchochea maendeleo ya kisiasa na kiuchumi kwa kuleta mawazo shindani kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa.

Kinyume na matarajio ya kuanzisha vyama vingi vya kisiasa hapa nchini, vyama hivyo vimekuwa vichaka vya ufisadi, ukabila, ubaguzi na vurugu tu.

Mbaya zaidi, badala ya kuchochea maendeleo chanya ndani ya nchi yetu, baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa ndio wapingaji na wazoroteshaji wakubwa wa maendeleo ya nchi yetu.

Kwa mtazamo wangu, hakuna haja ya kuwa na vyama vingi vinavyoleta vurugu kila siku, ni bora kubaki na mfumo wa chama kimoja ambao unaiweka nchi kwenye mikono salama na kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Vyama vyingi vya siasa hapa nchini vimeshindwa kutumia uhuru wa kidemokrasia vilivyopewa ili kuwaletea wananchi maendeleo, badala yake vimekuwa vikitumia uhuru huo kuhubiri na kupandikiza chuki dhidi ya serikali badala ya kuhubiri umoja, amani na mshikamano, kutukana viongozi wa serikali, kuchochea vurugu badala ya kuchochea maendeleo, kupinga juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikali, na vimekuwa vikifanya mambo mengi tu ya hovyo kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe binafsi badala ya kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

Pendekezo langu: kwa vile vyama vingi vimeshindwa kutimiza lengo la kuleta mabadiliko chanya kama ilivyotarajiwa wakati wa kuanzishwa kwake, vyama vingi vifutwe tu ili tubakiwe na chama kimoja kama ilivyokuwa zamani.

4. CCM kwa miaka mingi kimekuwa chama cha ukombozi kwa nchi nyingi barani Afrika. Kimesaidia kuzikomboa nchi nyingi barani Afrika kutoka katika makucha ya wakoloni. Baadhi ni Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Afrika Kusini, nk.

Ukizungumzia CCM unazungumzia chama kilicho makini na imara sana, ambacho kimezungukwa na marafiki karibu kila kona ya dunia hii. Je, nani kama CCM? Ndio maana tunadiriki kusema kwa dhati kabisa kuwa "CCM NI BABA LAO".

Ni mambo mengi CCM imefanya ndani na nje ya nchi, hivyo kinastahili kuenziwa kwa namna ya kipekee kabisa.

TAREHE 05 FEBRUARI KILA MWAKA IWE SIKU YA KITAIFA

CCM inaelekea kuadhimisha mwaka wa 43 tangu kuzaliwa kwake. Ni hapo tarehe 05/02/2020.

Kutokana na heshima kubwa kilichojijengea ya kujenga nchi na kuiletea maendeleo ya dhati nchi yetu, ingefaa tarehe 05 mwezi wa 02 kila mwaka itambulike kuwa ni siku ya KITAIFA, ili kukienzi vyema Chama Cha Mapinduzi, ambacho kwa hakika kimefanya kazi kubwa kuhakikisha nchi yetu inapata uhuru, inapata amani, inapata maendeleo, nk.

Huu ni utamaduni uliokuwepo huko nyuma kabla ya kuanzisha vyama vingi ambavyo kwa yakini, vimeshindwa kukidhi matakwa ya watanzania.

Ni vyema na haki sasa tukarejesha heshima ya CCM kwa kuifanya tarehe TANO ya mwezi wa PILI kila mwaka kuwa siku ya KITAIFA ya kuzaliwa CHAMA CHA MAPINDUZI.

Hii itasaidia kujenga dhana sahihi ya uwajibikaji na uzalendo kwa vijana wa nchi hii na kutunza vyema historia ya chama chetu na nchi yetu kwa ujumla, hasa kwa vizazi vipya. CCM NI BABA LAO.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
 
Back
Top Bottom