Kidudu mtu-Bongoflava. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kidudu mtu-Bongoflava.

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Sizinga, Jul 26, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mi niseme nyie wasanii wa bongoflava kama hamna vitu vya kuimba ni bora mtafute ishu nyingine mfanye!!
  Sasa hivi taifa limegubikwa na kila aina ya matatizo lakini nyie wasanii ham-reflect kitu chochote kinachotuzunguka
  kwenye hizi kero zetu. Kwa sababu ya elimu duni, Ajira ngumu nyie wenyewe(wasanii wengi) m-meamua kuajiari kuimba, ajira ni tatizo, rushwa, magonjwa mengi, njaa kali, wizi, ufukara wa kutisha, janga la umeme, ukame, vifo mahospitalini...
  yaani mambo mengi mengi tu, lakini hamuimbi bali mnarushiana maneno tu.

  Sasa leo hii Offside Trick badala ya kumpa POLE mama MJAMZITO anayetaabika hospitalini kwa uzazi wa kisu eti leo hii
  mnampa POLE SAMAKI. Jamani, ndo maudhui gani haya??Ni maudhui ya matusi kwa kwenda mbele, Nyimbo za ovyo zinaimbwa kwenye huu muziki wa hovyo!!

  Sasa leo mwenzenu kajivua gamba kaondoka/kajivua gamba kundini mwenu kwa ajili ya nyimbo zenu za hovyo, eti mnamtungia nyimbo kawa kidudu mtu. sasahapa nani kidudu mtu, nyie au AT?? Mwenzenu anakula tuzo na nyie m-mebaki
  kulalama tu, au yeye ndio alikuwa kichwa hapo.

  Sasa angalia mlivyovuna aibu, nae kaamua kuwajibu na sijui OFFSIDE TRICK WAKALI WA ZANZIBAR mtajitetea vipi kwa
  sababu nyimbo ya AT kasema bila kuuma maneno kwamba nyie ni MAS.HOGA na anakula kwa mama ntilie coz mama zenu hawajui kupika. Sasa mnaipeleka wapi sanaa ya Bongo??
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Wanaoimba nyimbo za maana kama 20% hachukuliwi kwenye Fiesta.

  Tuzo 5,,lakini wamemwona anaimba mapambio.
   
 3. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siwalaumu sana kwa sababu wao wanaanglia wadanganyika tunataka nini na ndicho wanatuchotuimbia..bro,fanya hata research hapa JF utaona watu wengi tunapenda MMU..sasa utawalaumuje hao Ubongo wa fleva???...ni kawaida yetu kupenda mambo ya mzaha..masemo wa mkuu mmoja hapa bongo bora maisha uyafaye kama kitu cha mzaha manake uki-complicate
  umekwenda..
  Ila hapo mkuu..kwenye red, ebu nitumie basi kibao hiko cha AT unajua huku ughaibuni sometimes tunakosa mengi..
   
 4. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi ni kazi tu, musianze kuwasema OFSIDE TRICK kwasababu ya wimbo wa kidudu mtu. Kuna nyimbo huku bongo za kipumbavu zaidi wala hata hazivutii.
  By the way, OFSIDE TRICK me nawaona wapo chini kuliko AT. Coz AT anapiga mziki kama kazi then anapiga mziki kwa kujibu mapigo kutoka kwa wapinzani wake. Wimbo wakidudu mtu kabla kuujibu katanguliza nyimbo ya Mmemchokoza nyangumi then ndo akaujibu kwa wimbo wa VIFUU TUNDU (kuna kipande cha mashoga). Na bado kuna majibizano yaliyoendelea kati yao ila AT kikazi katoa wimbo ambao nasikia ni mzuri unaoitwa MSHAHARA HAUTOSHI.
   
Loading...