Nashauri katika sanaa ya muziki, ili mtu awe msanii wa muziki basi serikali iunde kozi fupi walau ya mwaka mmoja

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
WANAMUZIKI WENGI NI HAMNAZO NA LIMBUKENI

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Familia zenye heshima na utajiri, familia za kisomi na kitaaluma, familia zilizoshika dini, familia zenye mambo ya kimila nyingi zinaona muziki ni kazi mbaya, kazi ya kihuni, kazi isiyo na heshima.

Familia za viongozi wakubwa wa nchi wengi huuchukulia muziki kama kazi ya hovyo. Hata wasanii wenyewe baadhi yao wamekiri walipohojiwa kuwa, watawaruhusu watoto wao wafanye muziki wengi wao walikataa na kusema hawapendi.

Kwa upande wangu muziki ni sanaa nzuri lakini wahusika ndio wanaiharibu, wengi wanaojiingiza katika Sanaa ya muziki wengi ni watu wa hovyo, wahuni, watu wenye upeo mdogo, watu wenye elimu duni na hii ndio sababu kazi hii hudharaulika na kuonekana haina maana yoyote ile zaidi ya kuwa kichocheo cha kuharibu maadili ya kizazi chetu.

Muziki ni sanaa ya ajabu nzuri na yakujivunia kwani ni sanaa yenye kuburudisha jamii, kuelimishaa, kuonya na pia kujipatia kipato. Lakini wahusika waliojiingiza huko wengi wao ni watu wa hovyo, wahuni, wenye ulimbukeni wa ajabu. Ni nadra sana mwana muziki kuheshimika licha ya kuwa wao wenyewe wanajiona wanaheshimika lakini ukwei mchungu ni kuwa wanamuziki huheshimiwa zaidi na wahuni, watu wa hovyo, na watu wapendao mambo ya hovyo.

Katika nchi yetu ya Tanzania, sisi wote ni mashahidi, kuwa 80% ya wanamuziki ni watu wa hovyo, wenye elimu duni, limbukeni, bendera fuata upepo, wapenda mambo ya hovyo hovyo.

Ukitaka kuthibitisha jambo hili huhitaji akili kubwa au elimu ya chuo. Angalia nyimbo za hao wasanii wapuuzi, angalia maudhui yake, wengi huimba upuuzi, matusi ya nguoni, wengi huwaza ngono ngono tuu za hovyo, kutupiana vijembe vya kipuuzi.

Mbaya zaidi hata Baadhi ya wasanii wakubwa nao ni watu wa hovyo licha ya kujipatia umashuhuri na utajiri kupitia muziki wao wa hovyo.

Kama bado hukubaliani na mimi, angalia matukio yanayofanywa na wasanii hao hao wa muziki, wengi hufanya uhuni, upuuzi, umalaya na wengine wakiwa na kashfa ya ushoga. Unakuta msanii anaoa leo kesho anaacha au kuachwa, unalikuta lisanii linazaa zaa hovyo na kujisifia upuuzi kwa kuzalisha wanawake bila kufuata maadili. Wanamuziki wengi wako na tabia hizo, je hiyo ni tabia njema ndani ya jamii? Au ninawasingizia? Maana mnawajua nao wanajijua wenye tabia hizo za hovyo na ulimbukeni wa kitoto, na hii inasababishwa na malezi yao, uhaba wa elimu, na ulimbukeni.

Kama mtabisha na hilo, basi angalieni mavazi wanayoyavaa, Ili uwe msanii wa muziki unapaswa uzidiwe akili hata na mbuzi au kondoo. Wanamuziki wengi wanavaa mavazi ya uchi, kujidhalilisha, kujivua utu wao, wengi mawazo yao yanalenga kuonyesha mvuto wao wa kimapenzi, akili zao wengi wao zimekaa kingono ngono.

Kwa bahati nzuri nina connection na baadhi ya hao wasanii, ukiongea nao wengi akili zao ni kama zimefyatuka, ukiwashauri jinsi ya kuifanya kazi yao kwa heshima watakuona wewe ndio mshamba, sababu kubwa wanakuambia bila kufanya hivyo hawapati pesa. Hivyo ili wapate pesa basi ni lazima wafanye upuuzi.

Angalia hata Kick zao, zimekaa kitoto toto, zimekaa kwa namna ya kuiona jamii inawajinga wengi wa kuchekelea upumbavu wao.

Angalia interview za baadhi ya wasanii, yaani ni upuuzi mtupu wengi wao huongea mambo ya kushangaza ambayo hata Nyani kwa akili zake hawezi kuongea. kujisifia upuuzi upuuzi, mbaya zaidi hii haifanywi na wasanii wakike bali wanaume siku hizi ndio wamekuwa wapuuzi. Yaani msanii anajua kabisa yupo mbele ya Kamera lakini anashindwa kuchagua cha kuongea, anashindwa kuficha upuuzi wake walau watu wamuone wa maana.

Pia nisisahau hili, waandishi wa habari nao wengi wao katika hili wamekuwa ndio chanzo, yaani mwandishi wa habari anahoji mambo ya kipuuzi na msanii naye kwa vile hajielewi anajibu maswali ya kipuuzi hivyo wote wanageuka wapuuzi kwenye mahojiano ya kipuuzi.

Naipongeza serikali kwa kuunda sheria kuwa ili uwe muandishi na mtangazaji wa habari basi unapaswa kuwa na elimu ya uandishi wa habari tena kuanzia shahada. Sio jitu linajua kuongea tuu ndio linajiita liandishi la habari au litangazaji, matokeo yake ndio hayo mtu anahoji upuuzi tuu, wengine wanaongea matusi kabisa kwenye vyombo vya habari.

Nashauri katika sanaa ya muziki, ili mtu awe msanii wa muziki basi serikali iunde kozi fupi walau ya mwaka mmoja, watu wasome wafanye mitihani, wapewe vyeti, huko watafundishwa Ethics za Muziki na mambo mengi yahusuyo muziki. Kisha wapewe leseni na sheria kali zichukuliwe watakaoenda kinyume na Ethics za fani yao.

Lakini hawa wahuni waliokuwa kwenye hii fani watazidi kufanya maajabu alafu wakiyapa jina maendeleo ya muziki kumbe ni maendeleo ya upumbavu katika muziki.

Inashangaza tuna wanamuziki wanaoona muziki umeendelea kwa kuimba matusi, kuvaa nguo za ajabu na uchi, kuunda Kick za kipumbavu, ati huko ndio kuendelea kwa muziki. Hii ajabu sana.

Niwapongeze wasanii wote ambao mnazingatia maadili ya kazi yenu, ninyi ni kioo cha jamii, ninyi mnamchango mkubwa kwa jamii kuliko hawa wapuuzi wanaojifanya wao ndio wanauendeleza muziki kumbe wanaendeleza matusi na kuhamasisha ngono zembe ndani ya jamii.

Unakuta jingine linasema limetengeneza ajira, kumbe ni ajira ya kufundisha watu matusi, ajira ya kufundisha watu kuvaa uchi, ajira ya kuunda maneno ya hovyo ndani ya jamii. Ajira! Ajira za kihuni.

Wewe msanii anaunda kick ya kupewa zawadi ya Gari kumbe hajapewa lengo ni kuilaghai jamii kuwa naye ni mkubwa. Huo kama sio upuuzi ni nini?

Hakuna mzazi mwenye akili timamu, mwenye maadili ya kidini au ya kimila, au mzazi msomi ambaye ataruhusu mtoto wake afanye upuuzi unaofanywa na wanamuziki wengi hapa nchini. Labda kama Mzazi awe hana nguvu, masikini na asiye na elimu. Yaani mzazi timamu amruhusu mtoto wake aende akakae uchi mitandaoni, au kwenye magazeti ati hiyo ndio kazi, sijawahi kuona mzazi wa hivyo popote pale, kama nilivyosema labda mzazi asiye na nguvu au masikini.

Mwisho; Wana Muziki wajirekebishe, tafuteni elimu, acheni ulimbukeni, pendeni na iheshimuni kazi yenu. Waigeni ambao wanamaadili.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ukiona jambo lolote linafanyika duniani ipo roho nyuma yake inayosababisha jambo Hilo! Kumbuka mziki ni part ya mbinguni ambayo kiongozi wake alikuwa lusifa, ambaye ndiye shetani wa Sasa! Hivyo kinachofanyika kwa Sasa ni kazi ya shetani ndo maana washabiki wake ni wengi na sio Tanzania pekee ni dunia nzima,

wengi wa wanapenda nyimbo za utupu hizo na ndo Zina mashabiki wengi! Kikubwa hizi ni nyakati za mwisho shetani anatafuta watu wa kwenda naye motoni na kwa kiasi Kikubwa kafanikiwa kwa hilo! Hivyo huwezi kuzuia jambo hili kwasababu nyuma yake ipo roho za kishetani na ndo zinazowaendesha Hao wasanii!! Kikubwa ni kumkimbilia MUNGU na kutafuta wokovu wa Bwana Yesu ili uepukane na hasira ya MUNGU inayoujilia ulimwengu mda sio mrefu!!
 
Ukiona jambo lolote linafanyika duniani ipo roho nyuma yake inayosababisha jambo Hilo! Kumbuka mziki ni part ya mbinguni ambayo kiongozi wake alikuwa lusifa, ambaye ndiye shetani wa Sasa!...

Unataka kunambia kama serikali ikiamua kuzuia wanamuziki uchwara na muziki wa uchi itashindwa?
 
Mkuu Muziki ni taaluma hiyo ukishajua inatosha kuelewa mantiki ya uzi huu.
Kuna baadhi ya mambo nadharia na vitendo vinavurugwa makusudi ili kufikia lengo.
Uking'ang'ana na kanuni na sheria za makuhani unakufa njaa.
sio kwamba sijui.
 
kila taaluma ina ethics zake,
haya nambie kilichotokea Wasafi tv na gigy money sijui,
huoni athari za kuwa na wana muziki vichomi
Rejea andiko langu la kwanza, 'wakikiuka,watachukuliwa hatua.....'

Tumeona wameadhibiwa.
Hayo ndio maisha, au unataka watu wasifanye makosa?
na wengine wasijifunze?

Je, Umesoma hadhira iliyokuwepo eneo la tukio imelichukuliaje hilo tukio?

Amini usiamini wapo watu huwa wanavutiwa,kufurahi na kusuuzwa na matukio kama hayo.
Binadamu ndivyo tulivyo na Duniani kote iko hivyo.

Pengine changamoto ni swala la hivyo vitu kuwekwa kwenye Luninga tu,
vinginevyo si shida saana kama tunavyolazimishana.
Mkosaji zaidi ni alierusha tukio-TV sio Msanii (Kwa Maoni yangu mimi)

Kwanza, tukio limetokea usiku, eneo ambalo hakuna watoto shida iko wapi?

Mambo kama hayo ndio chachandu ya maisha na usishangae hata hiyo adhabu ikapunguzwa mara dufu punde tu.

Tusiwe serious sana jamani.
 
Kuna mataifa yanafanya mziki wa heshima, had Raja. Huku Tz wamejaa mateja, wanaigiza pono kwa tiketi ya mziki.
 
Wewe pia ni mpuuzi tu kama unashabikia muziki wa kipuuzi, mbona kaswida zipo nyingi tu na husikilizi!
 
Back
Top Bottom