Kidogo - Diamond ft. P-Square

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,205
15,162
Naam,ile ngoma iliyokuwa tukiisikia kwamba itatoka hatimae Leo imetoka rasmi tar 12 Julai 2016.

Ngoma inaitwa KIDOGO, msanii kutoka BongoLand Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz amewashirikisha ndugu mapacha waliokuwa wakiunda kundi maarufu kutoka Nchini Nigeria wakiitwa P.Square.

Beat la ngoma limetengenezwa na producer kutoka Tanzania aitwae SHIRKO huku ikifanyiwa mchanganyiko (mixing) kidogo ili kuleta ladha na producer kutoka Nigeria aitwae V-TECK. Producer wa WCB aitwae Laizer pia mikono yake imehusika kwa kiasi Fulani.
Video imeshootiwa na GodFather Productions kutoka Bondeni "South Africa"

Ngoma ni Kali na Msanii huyu kutoka Bongo anaonekana kuiweza hasa kazi yake. Twende tukaitazame kisha rudisha Maoni yako hapa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom