Happy Bday Kwa Diamond Platnumz, Chibu Dangote, Baba Lao, Simba, Toto La Kimanyema, A Boy From Tandale

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Wana Celebrity What's up!

Tarehe kama ya leo 2.10.2020 alizaliwa Diamond Platnumz(Naseeb Abdul)katika mitaa ya kiswazi Sana Tandale.Alizaliwa katika familia ya kimaskini iliyokuwa ikilelewa na mama aliyetelekezwa na mumewe(Bi Sandra;Mama Dangote)

Pengine ugumu wa maisha na kushindwa kulimfanya awe na juhudi zilizomfikisha hapa alipo.

Ili kurekodi wimbo wake wa kwanza ilimbidi aibe pete ya dhahabu ya mama yake kulipia gharama za kurekodia katika studio.

Masikio ya wana burudani wengi yalianza kuona ujio wa kipekee wa star huyu katika wimbo wa "Kamwambie"wimbo aliouandika baada ya kuachana na mpenzi wake wa zamani akiutumia kama ujumbe wa kumfikishia popote alipo.

Baada ya wimbo huu nyota ilifunguka kwa star Huyu na kuwa mwangaza na mwanzo wa kubadilisha maisha yake.

Kwani aliendelea kutoa hit songs zilizopendwa na kusikilizwa na mashabiki wa muziki na alitokea kuwavutia sana.

Mwaka 2014 alitoa ngoma iendayo kwa jina "My Number One"iliyofanya vizuri sana.
Na remix yake baadae akaifanya na mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria "Davido"huu ukawa mwanzo wa mafanikio ya muziki wake nje ya Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla.

Amefanya mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya Bongo Fleva akiwa ni kati ya wasanii wanaolipwa vizuri kwa show moja.Kwa sasa itakugharimu takribani million 60 kwa show moja ya Diamond.
Na ni kati ya wasanii wa kwanza kuwahi Kuwa na dancers wake binafsi Tanzania.

Moja ya rekodi alizowahi kuvunja ni katika usiku wa Tuzo za Kili Music Awards mwaka 2014 ambapo aliibuka na Tuzo saba ndani ya usiku mmoja.Ndiye msanii pekee kuwahi kufanya hivyo.

Ameshirikisha wasanii mbalimbali wa nje katika nyimbo zake hivyo kufanya muziki wa Bongo Fleva kutambulika kimataifa.

Lebo yake ya WCB ni miongoni mwa lebo kubwa za muziki barani Afrika ikiwa na wasanii kama Lava Lava,Mbosso,Zuchu,Rayvanny na Queen Darleen.

Kwa sasa ni C.E.O wa Wasafi Media(Wasafi TV &Wasafi FM)

Mmiliki wa Lebo ya WCB wasafi

Muanzilishi na mmiliki wa Zoom Extra

Utajiri wake kwa mwaka 2018-2019 ulikadiriwa kuwa dollar million 4(Billion 8 za Kitanzania)
Kufutia endorsements za makampuni vitu na thamani za biashara anazomiliki.

He's an Inspirational icon to youths who are willing to achieve their dreams and make use of their talents
 
Sema hatujavuta tangu juzi. Wewe si unajua alosto?
 
October 2 kila mwaka ndio siku pekee utayosikia mazuri yake tofauti na siku ya kifo chake, hakika apewe sifa kabla akiwa hai
Innos b,hawa nitarejea , lavalava, rayvanny, mbosso, Kenny,n.k hawa wote wanamshukuru kwa namna tofauti.

Ndiye msanii aliyetengeneza ajira nyingi zaidi katika historia ya muziki bongo kuanzia dancers, photographers, body guards, producers, directors, drivers, models,n.k maana halisi ya kiwanda.

Kawafanya h baba, mwijaku,diva,carry mastory, waongelewe mjini.hawa watu hawawezi kusikika mjini bila kumuongelea direct or indirect.

Nae ni binadamu kama mimi na wewe, kama ambavyo umefanya makosa katika sehemu mbalimbali za maisha yako, naye pia ametenda. Mwenyezi Mungu atusaidie sote kwani sisi sote sio wakamilifu.

All in all huyo ndiye Diamond platnumz simbaaa baba lao, Tanzania one,true motivation, from zero to hero,
Legend of the decade,
The game changer,
The great Entertainer,
Revolutionist of entertainment industry.
 
Kwa watoto wa kariakoo,kwetu ushamba mwiko. ..huchezi na dada zangu,mi nacheza na dada zako


Dah kiba anadharau sana😂😂🤣🤣
 
Back
Top Bottom