MTV waandaa collabo ya Ne-Yo na Diamond Platnumz, this is epic!

Mkalibari

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
659
396
Jionee mwenyewe.

Capture.PNG

============

Mashabiki wa Diamond Platnumz wavamia ukurasa wa Neyo wa Twitter
Baada ya MTV kutangaza Neyo atakuwa jukwaani kwenye utoaji wa tuzo za MTV mashabiki wa Chibu walivamia page ya Neyo na kila mmoja aliomba kolabo na Chibu.

Guess what? Neyo alipotua tu Durban akamtafuta Chibu kwa nguvu zote ma walipoonana kila kitu kitajulikana soon.

Kumbuka P Square tayari wameisha fanya na wakali kadhaa USA, Davido kapiga juzi kati na Meek na Wizkid kapiga na Drake.

Sasa ni zamu ya Diamond kuvuka boda ya Afrika.

View attachment 268939View attachment 268940
Check wabongo walivyo ivamia page ya Neyo.

Unajua chibu anajua sana kucheza na akili za wapenzi ni followers wake
Na wanamsaidia sana kwa kiasi kikubwa

=======
=======

NEYO AKUTANA NA DIAMOND AFRIKA KUSINI KWENYE TUZO ZA MTV AWARDS, 2015.
Haya sasa! Ne-yo na Diamond washakutana huko... Na kama tunavyomjua Diamond ni mzee wa Fursa... tutegemee kitu kikubwa kuanzia sasa..

Natamani kila Mwanamuziki hapa Tz awe inspired na mafanikio ya Diamond tupate hata wasanii 20 watakaowakilisha Tz ili tuje tuidominate Africa kimuziki maana inawezekana, kama vile 2face na Psquare walivyotengeneza njia ya Muziki wa Nigeria kuiteka Africa basi hata Sisi tutafika huko na hii ni kama tu tutasupport wanamuziki wanaofanya Vizuri nyumbani.
View attachment 268954

===========

NEYO ATUA KENYA KWENYE PROJECT YA COKE STUDIO
NE-YO IN KENYA
11201609_10153565768787012_7119675161688891380_n.jpg


Just landed in Africa! Shoutout to #KenyaAirways for the smooth flight #NONFICTION2015#CokeStudioAfrica
11915735_10153564239457012_3962219987706349981_n.jpg

===========

MENEJA WA DIAMOND ASAFIRI HADI KENYA KUOMBA COLLABO NA NEYO
Morning wakuu!

Kama ilivyo kawaida ya waswahili kuoneana wivu ndivyo ilivotokea baada ya msanii Alikiba kutangaza kufanya colabo na Neyo, Hali hiyo imeikaisirisha management ya Mondy na kuamua kumtuma Salim sk ambaye ni miongoni mwa meneja wa Mondy kwenda Nchin Kenya kuomba collabo Neyo ili imiwezekana lifanyike haraka na kurelease wimbo kabla hata ya collabo la Kiba na Neyo halijatoka.

Kwa bahati mbaya au nzuri Salim amekuta tayar collabo ya Kiba ndiyo imeanza jana usiku na baada ya coke studio itaachiwa rasmi.

View attachment 286581

NEYO ATAJA LIST YA WASANII ATAKAOFANYA NAO KAZI AFRIKA
Msanii nguli Neyo ametaja list ya wasanii amabao wame mvutia na yupo tayari kufanya nao collabo na wasanii hao ni P.square, Diamond na Vanessa Mdee. Neyo amesema hayo live wakati Anahojiwa katika kipindi cha coke studio pwilo Shardcole

COLLABO YA DIAMOND & NEYO: SHEDDY CLEVER AELEZEA JINSI ZALI LILIVYOMDONDOKEA
View attachment 286583

Wapo watayarishaji wengi na wazuri wa muziki nchini Tanzania, lakini Sheddy Clever wa Burn Records ndiye aliyebahatika kuchaguliwa na Diamond Platnumz kwenda Nairobi kusimamia zoezi zima la kurekodi collabo ya kimataifa ya Diamond na Ne-Yo kutoka Marekani.

Bongo5 imemtafuta mtayarishaji huyo wa ‘Number One' na ‘Ntampata Wapi' zote za Diamond, ambaye ametueleza jinsi alivyojikuta akitimiza ndoto ambayo hakuwahi hata kuiota, ya sio tu kukutana bali kumrekodi mshindi wa tuzo za Grammy Ne-Yo kwenye beat aliyoitengeneza.

"Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwasababu yeye ndiye muweza wa yote, pili naushukuru uongozi wa WCB kwasababu wao ndio wamefanikisha haya yote. Kwakweli nimejisikia furaha sana kwasababu sikutegemea kama nitakuja kufanya kazi hii." Alisema Sheddy.

Sheddy alianza kwa kuelezea jinsi ilivyokuwa mara ya kwanza anapigiwa simu na Diamond kupewa dili hiyo;

"Mi nimepigiwa tu simu na Diamond akaniambia kuna kazi inatakiwa ifanyike kwahiyo tunatakiwa kusafiri, nikamwambia poa nashukuru, na akaniambia kila kitu tiketi yako ipo jiandae kwa safari… basi tukasafiri tukaenda tukafanya hiyo kazi…nashukuru Mwenyezi Mungu. Ni kazi nzuri na naimani itafika mbali."

Katika wimbo huo wa Diamond aliomshirikisha Ne-Yo, yeye Sheddy Clever amehusika kwa kiasi gani?

"Nimetengeneza beat, na vocal za Diamond kila kitu yaani nimeutengeneza wimbo kwa ujumla, Ne-Yo yeye tulimfata kule kwaajili ya kuweka vocal zake, Beat tulitengeneza pale studio (Nairobi), studio ile Diamond alilipia kwahiyo nilikabidhiwa studio kila kitu, ila kulikuwa na producer wake na Ne-Yo ni mzungu pia ndiye ambaye tulikua tunashauriana naye kubadilishana mawazo na nikajifunza vitu vingi zaidi."

Tupe uzoefu wako wa wakati unamrekodi Ne-Yo akiwa booth, ni msanii wa namna gani?

"Ne-Yo kwanza ni mtu mmoja amabye yuko peace sana tofauti na nilivyokuwa namfikiria, japokuwa nilikuwa na uwoga pia nikasema hivi ntamwambia nini hivi akikosea ntaweza kumrekebisha kweli? Lakini Ne-Yo anapenda pia kurekebishwa anapokosea, na anapenda pia ushauri sana kila anachokifanya anauliza niko poa? Vitu kama hivyo."

Ilimchukua muda gani Ne-Yo kurekodi sauti?

"Kwa upande wake hatukusumbuana sana nafikiri tulipiga kama take mbili tu akamaliza kurekodi kwasababu ana uzoefu wa siku nyingi."

Ne-Yo anazifahamu kazi ambazo umetengeneza zikiwemo za Diamond?
"Yeah Diamond alimwonesha kazi zote ambazo nimefanya na anapenda sana wimbo wa Number One."

Sheddy ambaye pia anawania tuzo ya Producer wa Muziki Wa Mwaka kwenye tuzo za AFRIMMA 2015,amemshukuru Diamond kwa heshima ambayo amempa kwa kufanya naye kazi na kumkutanisha na wasanii wengi wakubwa.

"Diamond amenipa heshima sana , kufanya nae kazi na kunikutanisha na wasanii wengi tofauti kwahiyo hii ni heshima kwangu, najiona nimekuwa tofauti na nimekuwa mkubwa…" alimaliza Sheddy.


Chanzo: Bongo5

SHEDDY CLEVER ADOKEZA KUWA NEYO KAIMBA KWA KISWAHILI KWENYE WIMBO WAKE NA DIAMOND
Producer Sheddy Clever aliyehusika na upishi wa collabo kubwa ya kimataifa ya staa wa Tanzania, Diamond Platnumz na mwimbaji wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo amedokeza kidogo kuhusu wimbo huo.

Mtayarishaji huyo wa Burn Records amesema kuwa Ne-Yo aliimba baadhi ya maneno ya Kiswahili katika verse yake. "Ne-Yo kaimba Kiswahili katika single hiyo, Diamond alimuimbisha Kiswahili siwezi kusema ni maneno gani ya kiswahili bali watu wakae mkao wa kula" Sheddy aliiambia Millardayo.com.

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond kuwaimbisha Kiswahili wasanii wa kimataifa anaofanya nao collabo, alifanya hivyo pia kwenye remix ya Number One aliyomshirikisha Davido, ambaye naye aliimba maneno machache ya Kiswahili.


Chanzo
: BONGO5
 
Diamond platnumz aka chibu dangote anazidi kung'ara kila kukicha kutokana na ubora anaouonyesha kwenye kazi yake na kuwa wakipekee sana barani hasa linapokuja suala la utumbuizaji..

Ukiachana na show ya road to mama ambapo diamond anatarajiwa kutoa burudani Nigeria 3, jully diamondplatnumz amezidi kupata shavu kwa kuchaguliwa kuwa ataperform pamoja na Neyo kwenye stage siku ya utoaji wa tuzo za Mtvmama2015... Na hii ni dhahiri kwamba moja ya tuzo anayogombea "best live" ni yake anasubiri tu kupewa..

Vipi wadau mnahisi patachafukaje sikuhiyo wanyama wawili hawa wakikutana??

Tusisahau pia kumtendea haki kijana
Kupiga kura ingia link hii

Waweza piga kura mara nyingi kwa kila kategori

Tuzo 3

http://mama.mtv.com/voting/

View attachment 263081

Tanzania oyeeee
 
Tupige kura kuna nafas 20 za kura kwa category.

Bofya vya kutosha kumpigia kura diamond na vanessa
 
Diamond tuzo ya Best Live act niyake bila shaka pia tuongeze nguvu kwenye category hzo zingne. Vote vote vote Neyo×Diamond live on stage itakuashigidii Shidaaa
 
Kwa kweli kijana ana ni-inspire sana!

Tena sana!

Hii nyota yake in ina mwanga hatari. Ngoja yangu niyafanyie kazi ning'ae kivingine.

About voting, nimeshampa mbili 3 sana tu. Hope tutashinda.

We wont cheat! lol lol
 
Ila Ne-yo si chakula cha bwana? Asije kumshawishi ndomo kujiunga kwenye hiyo movement. ..imenifika hapaaa (sound brown voice)
 
Back
Top Bottom