Hiyo ya unabii imenikumbusha kisa cha Messi na Ronaldo kabla ya El-Classico ambayo Madrid walifungwa tano. Ronaldo alidai kuwa yeye ni nabii, ametumwa na Mungu wa soka kuja kuwafundisha WaCatalan jinsi mpira unavyotakiwa uchezwe. Kesho yake Messi alipoulizwa maoni yake kuhusu kauli ya Ronaldo, akatoa jibu fupi,"Mimi sikutamka maneno yale." Awali ile kauli haikueleweka, ila wachambuzi wakaja kugundua kuwa Messi ndiye mungu mpira ambaye anakana kumtuma Ronaldo! Iliniua mbavu ile scenario.