Kiburi kinachelewesha maendeleo jiji la Mbeya

Nasikitika sana jiji la Mbeya kubeba taswila ya kutoheshimu, viongozi wakuu wa kitaifa na mamlaka zao. Matokeo yake jiji limekuwa linachelea kupata maendeleo ya haraka, kwa sababu ya kukosa ushirikiano dhabiti kutoka mamlaka za kiserikali.

Ipo wazi kuwa, wana Mbeya wafike mahari, watambue ipo haja ya kukubali kushirikiana na viongozi wakuu pamoja na mamlaka zao, katika kujenga jiji la Mbeya. Hii biashara wanayofanya ya kujionesha ni watovu wa nidhamu kwa serikali haitowafikisha popote, zaidi zaidi itakuwa ni hasara kwa kuendelea kukosa miradi ya maendeleo na kusahaulika.

Rai yangu: bado nafasi ipo ya kushirikiana na serikali, ifike mahari tutambue kwa busara yupi ni mtu sahihi ambaye anaweza kutuvusha katika daraja kuelekea katika maendeleo ya kweli, ifike mahari tutambue tunapaswa kujenga mahusiano mema na viongozi katika mamlaka zao za serikali kwa ajili ya maendeleo yetu, tukosoe kwa staha na adabu pale ambapo tunaona mambo hayaendi sawa, kuanzia sasa tujenge taswila mpya hakika jiji la Mbeya litatoboa, kwani lina sifa zote za kutoboa ila wanasiasa wanalichelewesha jiji kutoboa.
Acha ujinga na upoyoyo wewe, kama kodi wanalipa lakini ukataka wakusujudie ili uwape maendeleo na wao wakakataa basi jua anayetaka kusujudiwa ndiye popoma mkuu.
Hakuna sababu yoyote nzuri hapa duniani ya kuwanyima maendeleo walipa kodi, sanasana utakuwa unajitanabaisha kama mkoloni na mnyonyaji mweusi unywae damu za watu.
Uingozi ni swala waliloliomba wala hakulazimishwa mtu, kupendwa na kudharauriwa ni matokeo, anachopaswa kufanya kiongozi ni kutimiza wajibu wake tu basi.
Halafu nenda ukajifunze kutofautisha kati ya misimamo na kiburi.
 
Kwanza hujaeleza hujaeleza Mbeya kwamba kuna kiburi cha aina gani, pili ushirikiano unaousema ni ushirikiano wa aina gani? Mbona wakuu wa mikoa kibao wanashirikiana vyema na wananchi unataka kiaje yaani? Au unataka CCM itawale Mbeya mjini ndio useme sio kiburi?
Kidampa mmoja tu katumwa huyo ndo walewale wachumia tumbo aangalie mtwara lindi dodoma kote ni CCM kuna maendeleo gani?
 
Nimesoma bandiko lako,limenifanya kukumbuka mkoa wangu wa Singida,huku ni ccm kote,tena wanainyeyekea hadi kero.Ila hayo maendeleo sifuri.So unataka Mbeya hasa jiji nayo iwe kama Singida!!
 
Sidhani kama nimeshawishi upuuzi, pia sidhani kama nimempigia kampeni kiongozi fulani, andiko langu limejielekeza katika kubadilika wana Mbeya, biashara tunayofanya haitusaidii inatukata sana, tubadilishe huu utamaduni wa kujitia majeuri mbele ya walioshika makali.
Tupe mfano wa wanaotumia mbinu yako na kufanikiwa
 
Unaizungumzia Mbeya IPI?
Watu ndio viburi?
Wamekwamisha kipi?

Remember We dare to talk openly here
Nazungumzia mahusiano yaliopo kati ya wananchi wanaoishi jijini Mbeya, pamoja na viongozi wao, hapo tofauti iliyopo ni wananchi wengi wa upinzani au sio upinzani, kutowaheshimu viongozi na mamlaka zao, mkataba uliopo kati ya kiongozi na anayeongozwa ni kutegemeana kupitia kupeana ushirikiano, lakini jijini Mbeya kuna pengo kubwa la wana jiji hilo kujiona wako juu ya viongozi kwa sababu tofauti tofauti ambazo hazina faida yoyote kwa maendeleo ya jiji la Mbeya.
 
Kwanza hujaeleza hujaeleza Mbeya kwamba kuna kiburi cha aina gani, pili ushirikiano unaousema ni ushirikiano wa aina gani? Mbona wakuu wa mikoa kibao wanashirikiana vyema na wananchi unataka kiaje yaani? Au unataka CCM itawale Mbeya mjini ndio useme sio kiburi?
Kiburi mkuu ni kutokutii mamlaka pamoja na kutoheshimu mamlaka za viongozi hasa wa kitaifa, hii inaleta pengo la viongozi kukosa ushirikiano na wananchi katika kufanya kazi za maendeleo, ingawa kwa kiasi fulani wananchi wameanza kuamka, na wamegundua hii biashara wanayofanya inawakata sana, haina faida hata kidogo, zaidi zaidi ni maumivu tu.
 
Tupe mfano wa wanaotumia mbinu yako na kufanikiwa
Siku zote lazima ujue kula na kipofu mkuu, kama wananchi wa jiji la Mbeya watakuwa hawajui kula na kipofu, maendeleo ya kiuchumi watayasikia kwingine.
 
Ninavyojua maendeleo yanakuja na wananchi kwanza, kujipendekeza hakujawahi saidia watu. Nipe mfano wa watu waliofanikiwa kwa "kula na kipofu"
 
Huku RUVUMA niliko mm wabunge wote n CCM lakn nikisema ndio mikoa ya mwisho kimaendeleo ntakuwa cjakosea na wala huewez sikia wameipinga serikali
 
Nasikitika sana jiji la Mbeya kubeba taswila ya kutoheshimu, viongozi wakuu wa kitaifa na mamlaka zao. Matokeo yake jiji limekuwa linachelea kupata maendeleo ya haraka, kwa sababu ya kukosa ushirikiano dhabiti kutoka mamlaka za kiserikali.

Ipo wazi kuwa, wana Mbeya wafike mahari, watambue ipo haja ya kukubali kushirikiana na viongozi wakuu pamoja na mamlaka zao, katika kujenga jiji la Mbeya. Hii biashara wanayofanya ya kujionesha ni watovu wa nidhamu kwa serikali haitowafikisha popote, zaidi zaidi itakuwa ni hasara kwa kuendelea kukosa miradi ya maendeleo na kusahaulika.

Rai yangu: bado nafasi ipo ya kushirikiana na serikali, ifike mahari tutambue kwa busara yupi ni mtu sahihi ambaye anaweza kutuvusha katika daraja kuelekea katika maendeleo ya kweli, ifike mahari tutambue tunapaswa kujenga mahusiano mema na viongozi katika mamlaka zao za serikali kwa ajili ya maendeleo yetu, tukosoe kwa staha na adabu pale ambapo tunaona mambo hayaendi sawa, kuanzia sasa tujenge taswila mpya hakika jiji la Mbeya litatoboa, kwani lina sifa zote za kutoboa ila wanasiasa wanalichelewesha jiji kutoboa.
Pumbavu . Umeandika mavi matupu .Serikali ya wezi na wauwaji kama hii ndo ya kuunga mkono ?
 
Huku RUVUMA niliko mm wabunge wote n CCM lakn nikisema ndio mikoa ya mwisho kimaendeleo ntakuwa cjakosea na wala huewez sikia wameipinga serikali
Kuwa mbunge ni suala moja na kuwa mbunge mwenye ushawishi wa kupeleka miradi ya maendeleo jimboni kwako ni suala lingine mkuu
 
Nasikitika sana jiji la Mbeya kubeba taswila ya kutoheshimu, viongozi wakuu wa kitaifa na mamlaka zao. Matokeo yake jiji limekuwa linachelea kupata maendeleo ya haraka, kwa sababu ya kukosa ushirikiano dhabiti kutoka mamlaka za kiserikali.

Ipo wazi kuwa, wana Mbeya wafike mahari, watambue ipo haja ya kukubali kushirikiana na viongozi wakuu pamoja na mamlaka zao, katika kujenga jiji la Mbeya. Hii biashara wanayofanya ya kujionesha ni watovu wa nidhamu kwa serikali haitowafikisha popote, zaidi zaidi itakuwa ni hasara kwa kuendelea kukosa miradi ya maendeleo na kusahaulika.

Rai yangu: bado nafasi ipo ya kushirikiana na serikali, ifike mahari tutambue kwa busara yupi ni mtu sahihi ambaye anaweza kutuvusha katika daraja kuelekea katika maendeleo ya kweli, ifike mahari tutambue tunapaswa kujenga mahusiano mema na viongozi katika mamlaka zao za serikali kwa ajili ya maendeleo yetu, tukosoe kwa staha na adabu pale ambapo tunaona mambo hayaendi sawa, kuanzia sasa tujenge taswila mpya hakika jiji la Mbeya litatoboa, kwani lina sifa zote za kutoboa ila wanasiasa wanalichelewesha jiji kutoboa.
dada yetu Tulia bana, una mambo!
haya tumekusikia dada...lakini wenzio Mbeya wana rais wao ujue!
 
Kuwa mbunge ni suala moja na kuwa mbunge mwenye ushawishi wa kupeleka miradi ya maendeleo jimboni kwako ni suala lingine mkuu
Kwa hiyo Dada TULIA unawakashfu wabunge wenzako haya tuone wewe utakapochukua jimbo la mbeya town utakuwa na ushawishi wa kimaendeleo
 
Serikali ya mkoa na jiji wanatakiwa kutengeneza mazingira ya uwekezaji katika jiji la Mbeya. Uwekezaji wa majengo mazuri. Mji uwe planned ili ufae, uvutie na ueleweke kibiashra. Wajenge barabara ya maana kutoka mlima Nyoka hadi Mbalizi. Waweke utaratibu wa ujenzi kwa kupunguza gharama ya ardhi

Back
Top Bottom