Kibonde wa Clouds anaharibu

Kibonde wa Clouds anaharibu

Nyie mnaoleta post kuhusu kibonde mnamkuza bila sababu ni sawa na wasanii wanaojitengenezea kashfa kwenye magazeti ya udaku ili wapate umaarufu na magazeti yanunuliwe sioni sababu ya kumjadili mtu ambaye anaongea upuuzi
 
Mnaojifanya wanaCHDM mtaacha kelele siku si nyingi maana kaz yenu ni kubwabwaja tu dhidi ya serikali nani kawafunza kuwa upinzan maana yake kupinga kila kitu
 
Siyo wana Kusini. Ni watoto wa Mtwara mjini. Waliingia kichwa kichwa kwenye maandamano yenye nia yakupata umaarufu wakisiasa bila kufanya analysis ya matokeo ya agenda yao kwa jamii yenye maono tofauti. Hawakuweza kufanya analysis kujua malipo ya manesi, walimu, mapolisi pamoja na dawa wanazotumia mahospitalini, vitabu shuleni etc pale Mtwara mjini yanatoka wapi. Wangeweza kufanya hilo, wangepata kugundua kuwa pesa hizo kwa kiasi kikubwa hutokana na makato ya Pay as you earn ya watu wanaofanya kazi Tanzania popote pale na zaidi, wale wa Dar. Hilo lingeweza kuwafanya waelewe kuwa rasilimali za nchi hii ni za Watanzania wote na siyo wa eneo zitokako. Ngugu zangu hawa pia wangeweza kujua kuwa kwa vile mkopo wa ujenzi wa bomba hilo umetoka China at a very cheap price, then chances are that the force for them to say NO to the project, may have some western influences, kupitia vyama vilivyoamua kuwatumia. Kama wasomi, we have every reason to say NO to this type of Imperialism. Hayo ni miongoni tu mwa mambo ambayo wakazi wa Mtwara mjini na wale walioletwa kwa malori na vyama vya siasa waliyapuuzia. Besides, tumeambiwa mara kadhaa kuwa hawa ndugu zetu kwa sasa wana-surplus ya umeme by 5MW wakati sisi ndugu zao huku unakatikakatika kila siku, hivi, kuna shida gani kwa wao kutulea ndugu zao sisi ambao nasi ni Watanzania? Je, huu siyo uchoyo? Kama ni kazi, ni Mtanzania yupi anayekatazwa kwenda popote pale Tanzania kutafuta kazi au kusoma na akitaka kuhamishia ule utaalam alioupata kule alikozaliwa? Mimi ni mwenyeji wa Mbinga kule kusini ila naishi Dar na wewe pia inawezekana siyo mzaliwa wa Dar ila unaishi Dar. Jirani yangu hapa naye ni Mmachinga wa Mtwara mjini ila anaishi Dar. Dar ni ya Watanzania wote. Haya yote waliyapuuzia na wakatanguliza sera ya uchoyo blindly.

Mzee wa Bagamoyo ni mambo gani hawa wana kusini waliyapuuza kabla ya kuandamana?
 
Katika kipindi cha
Jahazi (Clouds FM) cha jana 3/1/2013, nilishangazwa sana na hatua ya
Bw.Kibonde kuwaita wakazi wa Mtwara ni "WAPUUZI".
Kwa kufanya hivyo, amevuka mipaka hata kama alikuwa na uhuru wa kutoa
maoni yake. Kama mtangazaji hakupaswa kuchukua kuegemea upande wa
serikali na kupuuza maoni ya wananchi, kwa namna yoyote ile huyu mtu
amekiuka miiko ya utangazaji.
Ni jambo baya kutumia radio kukandamizakilio cha wengi kwa sababu tu
yupo nyuma ya kipaza sauti. Ni bora waanzishe tafiti hata kwa njia ya
kupiga simu au kutuma sms ili kusikia wananchi wanasemaje na si
kuwatusi.

kwani sio wapuuzi?!
 
Nakubali kuwa tuna uhuru wa kutoa maoni lakini jambo la kuwaita watu wapuuzi si la kutetea, kibonde kateleza.
Pia, nilichokisikia mimi ni kuwa wana mtwara wanataka kiwanda kijengwe kwao sio kuitumia gas peke yao na kwa maoni yangu wamelenga kupata fursa zitakazoambatana na uwepo wa kiwanda. Mi naona wako sawa, kwanini iwe ni DSM tu? hata miji mingine inahitaji maendeleo na kiwanda ni moja ya hatua za kuyafikia.
 
kwani ni mara ya kwanza kumsikiliza kibonde hasa kwenye issue zenye reaction ya jamii fulani? mi kilawakati kukiwa na watu wanaoriot nimesikia kibonde akiwaita wapuuzi, wajinga, wapumbavu na tena anakandia huyo, mfano madaktari, tanesco, wanafunzi wa vyuo, yeye ni kupindua tu. mzoeeni tu hivyo, mkitaka kumsema, sina uhakika kama anakumbuka kama anaongeaga hivo. hivi ukienda kumuuliza mwendawazimu kwa nini jana umenitukana atakujibu? pengine anaweza akakuongezea tusi kwa kuona kuwa unamchokoza, leave him. kila mtu mwenye madai yeye huwa anachukulia mnaitaabisha serikali ya ccm ambayo ni kipenzi chake, atawatukaneni tu.
 
Wote mlio upande wa Kibonde MLAANIWE na nitaenda kuchukuwa uchawi wa NGENDE niwaroge wote yaan niny pamoja na Kibonde wenu, nitawageuza panya "chamaki nchanga" na nitafanya pati kubwa, nitawaalika wamakonde wote akiwemo Che Nkapa! "tutafaudu"
 
Huoni kwamba anaiharibia redio yake? Mtwara wakiisusia kisa wameitwa wapuuzi, si Clouds itakuwa imepoteza sehemu kubwa ya audience?
Kwa maoni yangu, hakupaswa kutoa maoni yake on air kama ilikuwa lazima ayatoe kwa style na lugha kama hiyo.[/QU unavyoandika ni kana kwamba unaitakia mema clouds, nenda huko nyie mtangazaji au radio haiwi njema hadi iisifie chadema, kila siku mnahamasishana hapa msiisikilize lakin bado kila siku hamuishi kuleta yanayosemwa na hyo radio,si ndio kusema imewabamba. Afu mod tusaidie kupunguza udhia kwa kututengenezea jukwaa la kibonde au clouds wasaga sumu wapate pakutema majungu yao!
 
Hahaha, Nyani Ngabu, nikikuita mpuuzi utakuwa ok? Umenikumbusha kuna ofisi ilibidi tukubaliane kuwa neno mpuuzi ni offensive na halitatumika kiofisi. Manake tulipata CEO lilikuwa at the tip of her tongue.
Huyo muite Mpuuzi Nyani Ngabu maadamu anakubaliana na hiyo "abusive language". Watu wengine bwana.........................
 
Kwa maoni yangu sioni ubaya wowote ule yeye kutoa maoni yake. Hata wanaomponda humu nao wanatoa maoni yao na hakuna anayedai JF ifungwe au watu wazuiwe kutoa maoni yao. Kila siku humu watu wanatumia lugha kali dhidi ya CCM na hakuna anayepinga. Lakini thubutu kuisema CHADEMA uone.

Kwa hiyo asiyependa maoni ya Kibonde basi na azime Clouds FM na afungulie Radio One, Magic FM, East Africa radio, Times FM, na kadhalika kama vile asiyependa JF ana uhuru wa kwenda kwenye blogu ya Le Mutuz, Sintah, Mange, au hata Da Jamilla aka Jestina Joji.

Uko sahihi kabisa NN. Tumechoka kila siku humu jamvini lazima kauli za kibonde zipewe attention....wakati mwingine mnampa mtu umaarufu ambao hana. Nimegundua pia kuwa wengi ni wasikilizaji wa hiyo Redio though kila mmoja anakataa kuwa alishaacha kuisikiliza.....sasa kama hamsikilizi ya kibonde mnayajulia wapi? Kama anawakera si radio zipo nyingi?

Mtu asiyekuwa tayari kusikia maoni ya mtu mwingine ni hatari sana na chanzo cha maafa katika jamii. Si lazima tukubaliane katika kila jambo.
 
Matusi gani? Yameorodheshwa? Extreme opinions and public broadcast of speech unbecoming of Tanzanian "traditionists" ndiyo mashudu gani hayo?

Nani anaamua hii ni extreme opinion unbecoming of Tanzanian "traditionists" na ile siyo extreme opinion unbecoming of Tanzanian "traditionists"? Wewe?

kwani kwetu sisi watanzania kuiita jamii fulani ni wapuuzi kwa kipimo cha ufahamu wako sio matusi?
 
Kibonde mara zote huwa anavuka zile rules and traditions za utangazaji. Shida yake ni kuwa siku zote yeye huegemea upande wa serikali. Haijawai kutokea akatoa opinion yakuipinga serikali hata kama ni dhahiri kwa kila mmoja - hata kwa mtoto wa darasa la saba - kuwa serikali imekosea ktk jambo linalojadiriwa. Tatizo la watangazaji wetu - na hata wandishi walio wengi - ni kuwa wengi wao hawana ambitions zakukuwa ktk kazi zao. Wengi huitumia fani yao (Uandishi na utangazaji) kama ngazi tu ya kuwapeleka kule watakako. Mpate mtangazaji kijana wa Citizen TV ya Kenya na NTV akimhoji kiongozi wa serikali, harafu pata picha ya yule Mze wa kipindi cha Dakika 45 cha ITV naye akimhoji kiongozi wa serikali ndipo utakapoona tofauti ilivyo kubwa ktk career growth aspirations kati ya hawa wetu na wale wa wenzetu. Hapa kwetu utangazaji ni ngazi ya kumwezesha mtangazaji kujulikana ili wakubwa wampatie kazi na wakati kwa wenzetu utangazi ni kazi ya kumwezesha mtu kuishi vizuri na hivyo, anakuwa na hamu ya kujiendeleza kiutangazaji.

Hata hivyo, ktk hili binafsi nimekuwa upande wa Kibonde. Kwa mara ya kwanza nipo upande wa serikali kwani naamini wananchi wa Mtwara wamekurupuka na wanaendeshwa na interests za watu bila kujua. Rasilimali za Tanzania ni za Tanzania. Siyo za watu wa eneo zinakopatikana tu. Ndio maana wote tunalia mwishoni mwa mwezi na makato makubwa ya Pay As You Earn na pesa hizi hupelekwa kila sehemu ya nchi hii siyo Dar tu.

Tatizo unajadili kitu ambacho hajakitafakari vizuri. Sioni kama una tofauti na hao waandishi wa tz kama kibonde ambao kila siku wanasubiri huruma ya watawala waweze kukithi haja zao. Wananchi wa mtwara wana hoja ya msingi inayohitaji kujadiliwa na watu wenye mawazo na fikra huru sio kama wewe unayekurupuka. Mnawalisha wananchi wa mtwara maneno wa uongo bila sababu za msingi. Shame on you. Tafuta ukweli na ujadili mada hujui hacha wengine wakupe maneno. Kinachosababisha waandishi kama hawa wa Clouds FM kuact unprofessionally ni kwa sababu ya kutojiamini na kutegemea huruma ya watawala kuliko uwezo wa taaluma yao. Historia imeonesha kwamba waandishi wa habari pamoja na vyombo vyao hushiriki na serikali iliyoko madarakani kugandamiza uhuru wa raia na kuwanyima haki zao kwa kuwaziba midomo. Jikumbushe kilichotokea rwanda wakati genocide. Jikumbushe kesi ya kenya katika mahakama ya the Hughe. Waandishi wa habari na vyombo vyao kama Clouds FM na Startv ni aina vyenye ushirika na watawala kuziba midomo ya raia masikini ili waweze kuendelea kuwatawala kirahisi. Tafakari.
 
Toka Gadner kipindi kimekosa mvuto huwa sisikilizi kabisa bora niskilize choice fm muzik wa kufa mtu
 
Angeegemea CHADEMA mngelia kama mnavyolia humu au ndiyo kwanza mngemwagia misifa kedekede?

We nyani sio lazima utetee kila upuuzi, kibonde ni nani mpak awaite watu wa Mtwara wapuuzi? Uhuru wa kutoa maoni yake anao na ndio hayo yanayotufanya tum judge kama hivyo.
 
unatakiwa utoe maelezo yote aliyoyatoa mpaka kufikia hilo neno upuuzi.au aliibuka tu nakusema watu wa mtwara wapuuzi kisha hapo ikawa ndo mwanzo na mwisho wa hoja yake?miongoni mwa mambo nsiyoyapenda ni pamoja na mtu kuchomoa neno moja au mawili kwenye habari ndefu halafu akaanza kulaumu au kuwashawishi watu wamlaumu mtu flani.mfano; kuna kipindi kikwete alisema "kuliko kutumia hela zote za serikali kulipa mishahara ya watumishi wa umma tu na kutofanya mradi wowote wa maendeleo na watu wengine wote ambao si watumishi wa umma wasipate chochoche kinachotokana na mapato ya serikali,ni bora kuto wapa malipo wanayotataka ili na mambo mengine yaeze kufanyika kwa maslahi ya wote.sasa kama kwa hili watasema hawatanipa kura 2010; ni bora wasinipe ila watu wote wanufaike na pato la taifa". kuna watu wakasema ; kikwete kasema "hataki kura za wafanyakazi" unaona maana inavyobadilishwa hapo?kwa hiyo tupe hoja yake kwa ujumla sio maneno mawili.

Give&Take! Hakuwapa wakamnyima
 
Back
Top Bottom