Kibonde wa Clouds anaharibu

Kibonde wa Clouds anaharibu

Hoja ya msingi hapa ni jinsi Kibonde alivyowaita wakazi wa Mtwara "WAPUUZI" kwenye chombo cha habari ambacho kinasikika Eneo kubwa la Tanzania.
Neno "WAPUUZI" alikuwa zuri kutumika Redioni,na hii haihitaji kujua saana sheria za vyombo vya habari kujua kwamba ni sawa au si sawa kutumia neno hili redioni katia njia ambayo dhahiri ni ya kudharau watu wa Mtwara
Suala hapa si kutafuta redio nyingine ya kusikiliza kwakuwa in many cases it is beyond our control ni redio gani usikilize(imagine you are in Public Transport na dereva kaweka hiyo radio ambayo hutaki kuisikiliza na abiria wengine wanataka kuisikiliza,etc) kwa hivyo inakuwa ngumu kusema utakwepa kusikiliza radio fulani 100%.Kimsingi alipaswa kutotumia neno hilo kwakuwa halikuwa zuri na pengine linachochea zaidi hasira kwa wana-Mtwara na watu wengine kiujumla.
Suala la maadili sio "choice", it is "mandatory" to stick to.
Mwandishi wa habari unapotakiwa kutoa maoni unatakiwa utoa maoni kulingana na hoja yenyewe na sio kuingiza maneno mengine ambayo ni ya uchochezi.
 
Katika kipindi cha Jahazi(Clouds FM) cha jana 3/1/2013, nilishangazwa sana na hatua ya Bw.Kibonde kuwaita wakazi wa Mtwara ni "WAPUUZI".
Kwa kufanya hivyo, amevuka mipaka hata km alikuwa na uhuru wa kutoa maoni yake.Kama mtangazaji hakupaswa kuchukua kuegemea upande
wa serikali na kupuuza maoni ya wananchi, kwa namna yoyote ile huyu mtu amekiuka miiko ya utangazaji.Ni jambo baya kutumia radio kukandamiza
kilio cha wengi kwa sababu tu yupo nyuma ya kipaza sauti.Ni bora waanzishe tafiti hata kwa njia ya kupiga simu au kutuma sms ili kusikia wananchi wanasemaje na si
kuwatusi.
unatakiwa utoe maelezo yote aliyoyatoa mpaka kufikia hilo neno upuuzi.au aliibuka tu nakusema watu wa mtwara wapuuzi kisha hapo ikawa ndo mwanzo na mwisho wa hoja yake?miongoni mwa mambo nsiyoyapenda ni pamoja na mtu kuchomoa neno moja au mawili kwenye habari ndefu halafu akaanza kulaumu au kuwashawishi watu wamlaumu mtu flani.mfano; kuna kipindi kikwete alisema "kuliko kutumia hela zote za serikali kulipa mishahara ya watumishi wa umma tu na kutofanya mradi wowote wa maendeleo na watu wengine wote ambao si watumishi wa umma wasipate chochoche kinachotokana na mapato ya serikali,ni bora kuto wapa malipo wanayotataka ili na mambo mengine yaeze kufanyika kwa maslahi ya wote.sasa kama kwa hili watasema hawatanipa kura 2010; ni bora wasinipe ila watu wote wanufaike na pato la taifa". kuna watu wakasema ; kikwete kasema "hataki kura za wafanyakazi" unaona maana inavyobadilishwa hapo?kwa hiyo tupe hoja yake kwa ujumla sio maneno mawili.
 
Angeegemea CHADEMA mngelia kama mnavyolia humu au ndiyo kwanza mngemwagia misifa kedekede?

Nani kakwambia CHADEMA wanahitaji watu wanaowaza wa kutumia tumbo? We changia hoja, hoja hauhusiani na vyama
 
huwa inakua shida sana mtangazaji akileta mapenzi kazini
 
Mm sizijui hzo regulations mnazojadili, ila huwa siskilizi cloudz fm tangu miaka miiingi sana kwa afya ya akili yangu.
 
Mh jaman kwani kwenye JAHAZI kibonde anaingia peke yake?kama alikuwa peke yake na akaisadia serikali bila kusikiliza hoja za wananchi unacholalamikia ni sawa ila kama kulikuwa na mtangazaji mwingine alikuwa na mlengo tofauti na Kibonde hapo yupo sahihi labda kidogo kusema wapuuzi ndio mi naona alitereza kidogo.
 
Kibonde mara zote huwa anavuka zile rules and traditions za utangazaji. Shida yake ni kuwa siku zote yeye huegemea upande wa serikali. Haijawai kutokea akatoa opinion yakuipinga serikali hata kama ni dhahiri kwa kila mmoja - hata kwa mtoto wa darasa la saba - kuwa serikali imekosea ktk jambo linalojadiriwa. Tatizo la watangazaji wetu - na hata wandishi walio wengi - ni kuwa wengi wao hawana ambitions zakukuwa ktk kazi zao. Wengi huitumia fani yao (Uandishi na utangazaji) kama ngazi tu ya kuwapeleka kule watakako. Mpate mtangazaji kijana wa Citizen TV ya Kenya na NTV akimhoji kiongozi wa serikali, harafu pata picha ya yule Mze wa kipindi cha Dakika 45 cha ITV naye akimhoji kiongozi wa serikali ndipo utakapoona tofauti ilivyo kubwa ktk career growth aspirations kati ya hawa wetu na wale wa wenzetu. Hapa kwetu utangazaji ni ngazi ya kumwezesha mtangazaji kujulikana ili wakubwa wampatie kazi na wakati kwa wenzetu utangazi ni kazi ya kumwezesha mtu kuishi vizuri na hivyo, anakuwa na hamu ya kujiendeleza kiutangazaji.

Hata hivyo, ktk hili binafsi nimekuwa upande wa Kibonde. Kwa mara ya kwanza nipo upande wa serikali kwani naamini wananchi wa Mtwara wamekurupuka na wanaendeshwa na interests za watu bila kujua. Rasilimali za Tanzania ni za Tanzania. Siyo za watu wa eneo zinakopatikana tu. Ndio maana wote tunalia mwishoni mwa mwezi na makato makubwa ya Pay As You Earn na pesa hizi hupelekwa kila sehemu ya nchi hii siyo Dar tu.

Katika kipindi cha Jahazi(Clouds FM) cha jana 3/1/2013, nilishangazwa sana na hatua ya Bw.Kibonde kuwaita wakazi wa Mtwara ni "WAPUUZI".
Kwa kufanya hivyo, amevuka mipaka hata km alikuwa na uhuru wa kutoa maoni yake.Kama mtangazaji hakupaswa kuchukua kuegemea upande
wa serikali na kupuuza maoni ya wananchi, kwa namna yoyote ile huyu mtu amekiuka miiko ya utangazaji.Ni jambo baya kutumia radio kukandamiza
kilio cha wengi kwa sababu tu yupo nyuma ya kipaza sauti.Ni bora waanzishe tafiti hata kwa njia ya kupiga simu au kutuma sms ili kusikia wananchi wanasemaje na si
kuwatusi.
 
Kaka,

Elewa Kibonde anatafuta kazi serikalini ndio maana siku zote usimtarajie kuwa atatoa opinion inayopingana na serikali. Kwake yeye, utangazaji ni daraja tu na siyo fani kamili inayoweza ikamfanya aishi vizuri. Ukifuatilia vizuri kipindi chake na opinions zake ktk issue zinazohusu wananchi na serikali, utagundua kuwa yeye hajawahi kuwa upande wa wananchi. Tatizo ninaloliona mimi hapa ni kuwa je, Clouds FM wanawapa wananchi the Right to Respond to the allegations that Kibonde levels against them? Hili ndio tatizo kwani kila mara Kibonde huwarushia wananchi tuhuma nzito kupitia kipindi chake na wakati mwingine utafikia kudhania kana kwamba Clouds ni sehemu ya Uhuru FM ila wananchi wanayo haki ya kujibu tuhuma hizi. Je, Clouds wanao huo utaratibu?

Baada ya kusema haya, nimeona ktk hili niwe upande wa Kibonde, kama ambavyo nimesha-post kwenye one of my earlier posts. Neno WAPUUZI, linatokana na neno PUUZA. KU-PUUZA ni kutotilia maanane au kutoheshimu kitu, mtu, jambo fulani. Hivyo basi, kusema wananchi wa Mtwara ni WAPUUZI, siyo tusi. Ni sawa na kusema Wananchi wa Mtwara wameamua wasiheshimu mambo fulani na mimi naamini kweli ktk maandamano yao, wananchi wa Mtwara wamepuuzia a lot of issues walizotakiwa wazi-analyse vizuri kabla ya kuandamana. These are the very same issues that are giving the government nafasi ya kujibu hoja za wanaMtwara kiurahisi zaidi.

Hoja ya msingi hapa ni jinsi Kibonde alivyowaita wakazi wa Mtwara "WAPUUZI" kwenye chombo cha habari ambacho kinasikika Eneo kubwa la Tanzania.
Neno "WAPUUZI" alikuwa zuri kutumika Redioni,na hii haihitaji kujua saana sheria za vyombo vya habari kujua kwamba ni sawa au si sawa kutumia neno hili redioni katia njia ambayo dhahiri ni ya kudharau watu wa Mtwara
Suala hapa si kutafuta redio nyingine ya kusikiliza kwakuwa in many cases it is beyond our control ni redio gani usikilize(imagine you are in Public Transport na dereva kaweka hiyo radio ambayo hutaki kuisikiliza na abiria wengine wanataka kuisikiliza,etc) kwa hivyo inakuwa ngumu kusema utakwepa kusikiliza radio fulani 100%.Kimsingi alipaswa kutotumia neno hilo kwakuwa halikuwa zuri na pengine linachochea zaidi hasira kwa wana-Mtwara na watu wengine kiujumla.
Suala la maadili sio "choice", it is "mandatory" to stick to.
Mwandishi wa habari unapotakiwa kutoa maoni unatakiwa utoa maoni kulingana na hoja yenyewe na sio kuingiza maneno mengine ambayo ni ya uchochezi.
 
hizi mada zingine zilishajulikana siku nyingi cha msingi mnaozileta mkumbuke kuwa kuna watu wanalipa gharama za server!
 
Katika kipindi cha Jahazi(Clouds FM) cha jana 3/1/2013, nilishangazwa sana na hatua ya Bw.Kibonde kuwaita wakazi wa Mtwara ni "WAPUUZI".
Kwa kufanya hivyo, amevuka mipaka hata km alikuwa na uhuru wa kutoa maoni yake.Kama mtangazaji hakupaswa kuchukua kuegemea upande
wa serikali na kupuuza maoni ya wananchi, kwa namna yoyote ile huyu mtu amekiuka miiko ya utangazaji.Ni jambo baya kutumia radio kukandamiza
kilio cha wengi kwa sababu tu yupo nyuma ya kipaza sauti.Ni bora waanzishe tafiti hata kwa njia ya kupiga simu au kutuma sms ili kusikia wananchi wanasemaje na si
kuwatusi.

hana aibu huyu jamaa. Yeye kinachoangukia katika ulimi wake atakaitoa kama kilivyo bila hata kukihusisha lau na fikra zake ili kujua atakayoyasema yatakuwa na athari gani kwa walengwa. Muumba amsamehe bure kwa ni nami nina interest na pande za huko kusini kwa kuwa mwenyeji wa huko. Nashindwa kuelewa kwa nini wanalazimisha wananchi wote waelewe kwamab wanakusini hawataki gesi isafirishwe kuja DSM. Najua wanatumia nguvu nyingi kupinga ukweli lakini kinachodaiwa na hao anaowaita 'wapuuzi' ni hoja juu ya sababu za kusafirisha gesi toka Mtwara badala ya kuwa processed hukohuko Mtwara. Mengine mengi yaliyo nyuma ya pazia juu ya mradi huu yamekuwa posted na wadau mbalimbali. Vyombo vya habari vina malengo pia ya kuelimisha umma juu ya mambo yanayotokea ndani na nje ya nchi yao lakini kwa hili nadhani kibonde na wenzake inawapasa kujipanga
 
atapewa ukatibu muhtasi kwenye shirika la nyumba la taifa
 
Yaya Toure,nakubaliana na wewe kuwa Kibonde anaumwa japo sijajua ugonjwa anaoumwa,na lazima atakua ameahidiwa donge nono na Serikali huwezi kusema ujinga kama ule na kwanini awatukane?
 
Kaka,

Elewa Kibonde anatafuta kazi serikalini ndio maana siku zote usimtarajie kuwa atatoa opinion inayopingana na serikali. Kwake yeye, utangazaji ni daraja tu na siyo fani kamili inayoweza ikamfanya aishi vizuri. Ukifuatilia vizuri kipindi chake na opinions zake ktk issue zinazohusu wananchi na serikali, utagundua kuwa yeye hajawahi kuwa upande wa wananchi. Tatizo ninaloliona mimi hapa ni kuwa je, Clouds FM wanawapa wananchi the Right to Respond to the allegations that Kibonde levels against them? Hili ndio tatizo kwani kila mara Kibonde huwarushia wananchi tuhuma nzito kupitia kipindi chake na wakati mwingine utafikia kudhania kana kwamba Clouds ni sehemu ya Uhuru FM ila wananchi wanayo haki ya kujibu tuhuma hizi. Je, Clouds wanao huo utaratibu?

Baada ya kusema haya, nimeona ktk hili niwe upande wa Kibonde, kama ambavyo nimesha-post kwenye one of my earlier posts. Neno WAPUUZI, linatokana na neno PUUZA. KU-PUUZA ni kutotilia maanane au kutoheshimu kitu, mtu, jambo fulani. Hivyo basi, kusema wananchi wa Mtwara ni WAPUUZI, siyo tusi. Ni sawa na kusema Wananchi wa Mtwara wameamua wasiheshimu mambo fulani na mimi naamini kweli ktk maandamano yao, wananchi wa Mtwara wamepuuzia a lot of issues walizotakiwa wazi-analyse vizuri kabla ya kuandamana. These are the very same issues that are giving the government nafasi ya kujibu hoja za wanaMtwara kiurahisi zaidi.

Mzee wa Bagamoyo ni mambo gani hawa wana kusini waliyapuuza kabla ya kuandamana?
 
Hakuna wajinga kama huyu Kibonde anajidai kila kitu anakijua. halafu hajui lolote.
 
Alitumia kauli gani kwani... Hebu mtoa mada funguka.. Alitamka maneno gani? Hiyo wapuuzi si ishu sana, sema ametumia lugha ya kuudhi..
 
Back
Top Bottom