Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,669
Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi SABA wameuawa na majambazi huko Mkuranga, Mkoani Pwani.
Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.
Imeelezwa kwamba majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.
=====
UPDATES:
- Silaha zote (SMG) inadaiwa zimechukuliwa!
- Shambulizi limefanywa na mtu mmoja (jambazi/gaidi?)
=====
Came as a tip:
Jamani habari za usiku. Sisi huku BUNGU eneo la JARIBU mpakani tumepotelewa na askari saba(07) wa kikosi cha FFU.
Ilikuwa hivi:
Askari walikuwa wana-liviana ambapo section moja ilikuwa inatoka na nyingine inaingia. Sasa wakati hii inayotoka baada km 03, Jambazi/Gaidi lilikuwa limejificha porini karibu HIGHWAY baada ya gari kulikaribia jambazi/gaidi hili lilimshambulia dereva kwa mbele na gari kupoteza mwelekeo na kuanguka wakati huo jamba/gaidi liliendelea kushambulia.
Jambazi/gaidi alikuwa mmoja
=======
H. Crime Kibiti NR 62 MN 90 14/04/2017
Saa 02:30hrs kwa:
Upele Pwani (R) POL. Pwani (R) POL. Kibiti. Kbt/IR/337/2016.
Ilani ya kwanza
Kosa: mauaji (x)
Mnamo tarehe 13/04/2017 saa 18:15hrs huko Mkengeni kijiji cha Uchembe kata ya Mjawa tarafa na wilaya ya Kibiti (M) Pwani. Kundi la majambazi ambalo idadi yao bado haijafahamika wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la Polisi PT.3713 Toyota L/Cruiser na kuua askari nane ambao ni
1. A/INSP Peter Kigugu
2. F.3451 CPL Francis
3. F.6990 pc Haruna
4. G.3247 pc Jackson
5. H.1872 PC Zacharia
6. H.5503 PC Siwale
7. H.7629 PC Maswi
8. H.7680 PC ayoub.
Pia walimjeruhi askari no F. 6456 PC Fredrick kwa kumpiga risasi ya mkono wa kushoto na amepelekwa hospitali ya misheni Mchukwi kwa matibabu.
Baada ya majambazi hao kufanya mauaji kwa askari walifanikiwa kuchukua silaha tisa kati ya hizo SMG sita zikiwa na risasi 30 kila moja na long range tatu.
Awali gari ya polisi ilikuwa ikitokea Jaribu mpakani kwenye road block kuelekea Bungu, baada ya kubadilishana na shift nyingine ndipo walipofika maeneo ya Mkengeni sehemu yenye mteremko na majani marefu na kuanza kushambuliwa na najambazi kwa kupigwa risasi kioo cha mbele usawa wa dereva na kusababisha dereva kupoteza uelekeo na gari kuingia kwenye mtalo wa barabara na ndipo majambazi hao kufanya mauaji kwa askari.
Baada ya tukio hilo mahojiano yalifanyika na watuhumiwa waliokuwa wakishikiliwa na polisi ambao majira ya 02:15 hrs walienda kuonyesha eneo la msitu wa Kilima cha Mianzini barabara ya Nyamisati ambalo wahalifu hao hujificha.
Walipofika maeneo hayo walishambuliwa na majambazi hayo na kuwajeruhi wenzao waliokuwa mbele kwenda kuonyesha na baadaye walifariki dunia na ndipo majibizano ya risasi yakaendelea baina yao na polisi.
Katika majibizano ya risasi majambazi walifanikiwa kukimbia na kutelekeza silaha nne kati yao mbili za polisi aina ya polisi zenye no. Smg tzpl 10549 risasi 30, smg tzpl 26881630 risasi 30 na silaha mbili za majambazi smg moja na sar moja.
Eneo la tukio limekaguliwa na DCP Kashai, DCP Sabasi, SACP Mayala, ACP Ngoyayi, SSP Canute Msacky OCD - Kibiti na ASP Juma Kanena OC - CID Kibiti.
Miili ya marehemu imepelekwa hospitali ya taifa Muhimbili.
FCR/Maendeleo zinafuata.
Mwisho///////// toka: Crime (W) Kibiti
=======
IKULU, Rais Magufuli alaani mauaji ya Askari polisi 8 huko Kibiti mkoani Pwani. Ampa pole IGP na Askari wote kwa kuwapoteza wenzao.
Habari zaidi soma=>Rais Dkt. John Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa IGP na familia za Askari wote waliouawa
Walioua askari 8 wilayani Kibiti nao wauawa
FRIDAY , 14TH APR , 2017
Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, Nsato Marijani
Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.
Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.
Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.
Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.
Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.
Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kweny oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati” amesema Marijani
Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi
Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni