Mbona kutekwa wamekataa kujadili na huku si kutekwa wakauawa, isijadiliwe piaHii ni habari ya kusikitisha sana na ni matumaini yangu hata huko Bungeni watatumia mjadala kuzungumzia hili. Huko Mkuranga hii si habari ya kwanza kuhusiana na mauaji ya polisi kama ninavyokumbuka. Nini kinaendelea? Hawa ni mashujaa na Taifa linahitaji kuwaenzi ipasavyo pamoja na familia zao. Lakini pia ni muhimu sana kwa viongozi wa jeshi kuangalia ni namna gani baadhi ya mambo kama haya yanaweza kufanywa kwani kama kumbukumbu yangu inanijia vizuri aina hii imewahi kutokea tena huko nyuma ambapo wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliwategea polisi wakiwa wanabadilishana lindo
saba tena??Askari wamepigwa ambush na magaidi huko kibiti Walikuwa ni FFU mpaka sasa askari Saba wamepoteza maisha
///As received///
kabisa, hawa jamaa ndio wamekua na roho ngumu ajabu, mpaka wamekua adui zetu, Mungu anawaonaPolis nao wana roho ngumu
Hiyo ni Bungu, mpaka sasa hakuna gari inayotebea. Kule hakufai ingawa kuna ulinzi mkali sanaHabari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi watatu wameuawa na majambazi huko Mkuranga, Mkoani Pwani.
Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.
Imeelezwa kwamba majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.
Global Publishers Twitter Page
:::::::::::::::::::::::::::::::::>>>>>
Mkuranga,Vikindu na Kibiti usalama wake haupo sawa.
Pole kwa wafiwa
hili nalo ni tatizoPolisi wa tz sio rafiki ya raia.
Atasema cyo habari ataachia vyombo vyake vifanye kaziTuaegemea mwigulu afungue kinywa sasa