Kibanda: Kikwete mchovu, Pinda dhaifu

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Na Absalom Kibanda

VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wanaoongozwa na Rais Jakaya Kikwete wanapata jeuri ya kimamlaka na kuendelea kujiona mabwana wakubwa waliopewa dhamana ya kuendelea kuitawala nchi si kwa sababu ya ubora wao au weledi wao wa kazi na kiuongozi, bali misingi imara iliyowekwa na waasisi wa taifa hili.

Ni misingi hiyo imara ya uongozi iliyojengwa na viongozi waasisi wa taifa hili ndiyo inayowapa kiburi kina Kikwete, Mizengo Pinda na wenzao wengine kufaidi matunda ya madaraka wakati ushahidi ulio wazi umekuwa ukithibitisha pasipo shaka kwamba katika umoja wao wanaunda jeshi maarufu la viongozi wavivu wa kufikiri, wachovu wa kutenda, dhaifu katika kuona na wasanii katika maamuzi.

Matokeo ya uchovu na udhaifu walionao viongozi wa zama hizi za Kikwete wanaofikiri kwa ndimi zao na kuamua mambo mazito ya kitaifa kwa kuangalia mustakabali mwema wa matumbo yao na yale ya familia zao ndiyo ambao umetufikisha hapa tulipo leo.

Huhitaji kuwa na akili nyingi kubaini kwamba matukio ya siku za hivi karibuni kama yale ya sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, la mgomo wa wauza mafuta ya petroli, kushamiri kwa baa la njaa, mgawo wa umeme na hata kukwama kwa bajeti za wizara ndani ya Bunge ni matokeo ya mparanganyiko mkubwa ambao haujapata kutokea katika nchi hii katika kiini cha uongozi wa kitaifa.

Ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo kuiona serikali iliyosheheni viongozi ambao wamekuwapo madarakani kwa miaka mingi na wenye uzoefu mkubwa ikiyumbishwa bungeni kwa kiwango cha kupoteza mwelekeo na wabunge wachache vijana wanaotokana na vyama vichanga vya upinzani.

Ni jambo linalosikitisha kumuona Waziri Mkuu akilazimika kusimama katika nyakati zisizo zake na kwa dharura mara kwa mara ndani ya Bunge na kutoa hoja zisizo na mashiko za kujaribu kupooza hasira za wabunge na kuomba huruma zao ili kuifanya bajeti ya wizara fulani iweze kupita ilhali ikiwa na mafindofindo yaliyo bayana.

Lakini pengine ni kielelezo cha wazi cha udhaifu uliovuka mipaka unapomsikia waziri mkuu huyo huyo, akizungumza kwa kujiamini ndani ya Bunge wakati akijua kuwa anachokizungumzia hana mamlaka juu yake na tena anakisema kwa msisitizo hata kabla hajawasiliana na mkuu wake aliye na dhamana katika kile anachokisemea.

Nayaandika haya nikirejea kituko cha Pinda ndani ya Bunge aliposimama kuwakubalia wabunge wito wao wa kuikataa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na akawaahidi kuzifanyia kazi tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka zilizokuwa zikimkabili David Jairo ambaye alibainika kuandika barua kwenda katika taasisi kadhaa zilizo chini ya wizara hiyo akiomba michango ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kufanikisha kile alichokiita, uwasilishaji wa hotuba ya bajeti ya wizara.

Akizungumza kwa kujiamini huku akionyesha kukerwa na kitendo hicho cha Jairo, Waziri Mkuu Pinda ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema iwapo angekuwa na mamlaka (ambayo alipaswa ajue hata kabla hajashauriwa kuwa hana) angekuwa ameshachukua maamuzi dhidi ya katibu mkuu huyo.

Katika kuthibitisha kwamba Pinda alitoa matamshi hayo kwa kukurupuka na pengine kwa lengo la kupoza ki-propaganda hasira walizokuwa nazo wabunge dhidi ya Wizara ya Nishati na Madini, alikuwa ni mtu wa kwanza yeye mwenyewe kukiri siku moja tu baadaye kwamba alikuwa ameshapokea maelekezo tofauti kutoka kwa Rais Kikwete.

Wabunge na Watanzania walipaswa wawe wa kwanza kutambua kwamba maelekezo ya Rais yaliyokuwa tofauti kiutashi na mwelekeo wa awali wa Pinda kilikuwa ni kielelezo cha kwanza kwamba kauli ya waziri mkuu ama ilikuwa ni danganya toto au ilikuwa ina walakini.

Ni bahati mbaya sana kwamba hakuna aliyelipa uzito jambo hili wakati huo.

Kile ambacho Pinda alikiita maelekezo tofauti ya Rais Kikwete hakikuwa kingine bali uchunguzi ambao ulifanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa maelekezo ya Katibu Mkuu Kiongozi ambao ulikisafisha kitendo cha Jairo kuchangisha fedha kutoka katika taasisi zilizo chini ya wizara anayoiongoza.

Katika mazingira ya kawaida, ripoti ya CAG iliyotolewa sambamba na tamko la Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, ya kumsafisha Jairo ikiwa ni pamoja na kuamuru aripoti ofisini kwake siku iliyofuata ilipaswa kufuatiwa na matukio makubwa mawili.

Kwa serikali yenye viongozi wanaojiheshimu na wanaotambua maana ya uwajibikaji wa pamoja, Katibu Mkuu Kiongozi na CAG walipaswa kurejea mchakato mzima wa suala la Jairo na kubaini kwamba katikati alikuwapo Waziri Mkuu Pinda ambaye kwa bahati mbaya alishatoa kauli ya kipropaganda na isiyo na mashiko.

Wangekuwa ni viongozi wastaarabu, wanaotambua maana ya kuheshimiana wao kwa wao, hata kama si katika hali halisi, basi hata hadharani, Luhanjo na CAG Ludovick Utouh wangeshauriana na Waziri Mkuu Pinda kwanza na pengine wangemuachia yeye wajibu wa kulihitimisha sakata hilo la Jairo akilitolea kauli ndani ya Bunge kama alivyofanya siku alipoteleza kujitwisha uchungu wa kudhamiria kumtimua.

Kwa bahati mbaya hilo halikufanyika.

Ni wazi kwamba tungekuwa na serikali makini na ambayo inatambua maana halisi ya kusoma alama za nyakati (si zile za Kikwete za kuiogopa mitambo ya Dowans) Luhanjo na Utouh wangesubiri kwanza Mkutano wa 10 wa Bunge umalizike ndipo watangaze kile walichokuwa wamekusudia. Hili nalo halikufanyika.

Kwa kuwa haya yote mawili hayakufanyika basi, tulitarajia kulisikia jambo la tatu likitokea, nalo halikuwa jingine bali ni lile la kumsikia Waziri Mkuu Pinda akilitangazia Bunge uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake kwa hiari yake kwa kutoa sababu zifuatazo.

Kwanza; alipaswa kuachia ngazi kama hatua ya kutambua kwake na kukiri kwamba alikuwa amelipotosha Bunge kwa kusema jambo ambalo halikuwa kweli pale aliposema kwamba Jairo alikuwa amekosea kwa kufanya jambo ambalo linaacha maswali mengi, kinyume kabisa na matokeo ya uchunguzi wa CAG Utouh yaliyothibitisha kwamba ulikuwa uamuzi sahihi na wa kawaida.

Pili; alitakiwa atangaze kuachia ngazi kwa kuwa tamko la Luhanjo na Utouh lilikuwa ni ushahidi uliokuwa ukimchongea kwa wananchi na kwa Kikwete kwamba alimshauri Rais vibaya kwa tamko lake la ndani ya Bunge, akifanya kosa lilelile lililopata kumgharimu Waziri Mkuu wa zamani, John Samuel Malecela, zama za Serikali ya Awamu ya Pili.

Ili aweze kulielewa vyema kosa lake hili la pili, Pinda anapaswa kukitafuta na kukisoma tena (nina hakika alishapata kukisoma) kijitabu cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kisemacho; ‘Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania' ambacho ndicho kinachoaminika kumsukuma Rais Ali Hassan Mwinyi kubatilisha kama si kumfukuza kazi Mzee Malecela mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Tatu, kama tungekuwa tukiishi katika nchi zinazoheshimu mgawanyo wa madaraka ya mamlaka za dola (yaani Bunge, Serikali, Mahakama na Vyombo vya Habari) tamko la Katibu Mkuu Kiongozi na lile la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambao ni viongozi wazito serikalini, lililopingana waziwazi na mtazamo wa Waziri Mkuu anayetokana na serikali hiyohiyo lilikuwa ni sababu inayojitosheleza ya Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Pinda. Ajabu hili nalo halikufanyika.

Hatari ya kutokea kwa hili la tatu la kumpigia Waziri Mkuu Pinda kura ya kutokuwa na imani naye lilionekana dhahiri likikaribia kabisa kutokea ndani ya Bunge na kama si hoja aliyoibua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akitaka Bunge lijadili tamko la CAG na Katibu Mkuu Kiongozi, huenda leo tungekuwa tukizungumza lugha tofauti.

Ingawa ukiliangalia kwa haraka haraka unaweza ukaingia katika mtego rahisi wa kulishangilia Bunge kwa namna lilivyoonekana kukerwa na tamko la Utouh na Luhanjo, upande wa pili wa hatua hiyo ilikuwa ni kuokoka kwa Pinda katika tundu la sindano kwa namna ambavyo kama si ujasusi ulifanyika basi kilichotokea ni ukachero.

Ni wazi kwamba Rais Kikwete, Waziri Mkuu Pinda na viongozi wengine wa serikali wanapaswa kuwashukuru kwa dhati Zitto, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Spika Job Ndugai, Christopher ole Sendeka na wabunge wengine ambao walifanikiwa kwa kujua au kutojua kulifinyanga suala hili na hatimaye likamalizika kwa kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge.

Kwa namna mambo yanavyokwenda, kama ilivyokuwa katika misukosuko mingine iliyopata kutokea siku zilizopita, hatua ya Bunge kutaharuki kwa namna ilivyotokea, iliyokwenda sambamba na kile kinachoitwa uamuzi wa Rais Kikwete kumrejesha tena likizoni Jairo, akipisha kile kinachoitwa uchunguzi wa Bunge itamalizika ikimuacha Rais, waziri mkuu wake na serikali yake salama.

Mambo ya namna hii ya kumuacha Rais anayefanya kazi ofisi moja na kwa ukaribu mkubwa wa kimaamuzi na Katibu Mkuu Kiongozi akiwa salama na pengine kuonekana shujaa hata katika jambo ambalo mikono yake inaonekana dhahiri kuchafuka yanawezekana katika nchi kama zetu tu.

Sakata la Jairo ambalo yumkini limeshaanza kuchukua mwelekeo wa kutafuta mtu au watu wengine wa kuwatoa kafara kama ilivyo ada katika mishipa ya fahamu ya viongozi wa CCM na serikali yake litahitimishwa kwa ripoti ya kamati teule ambayo itaandaliwa mahususi kwa malengo ya kuficha uchovu wa Rais Kikwete katika kuongoza, kutenda na kuchukua maamuzi sahihi.

Kama hiyo haitoshi, hadidu rejea tano zilizotangazwa na Spika Makinda kwa Kamati Teule zimethibitisha hata kabla kazi haijaanza kwamba zitamnusuru Pinda na kuficha udhaifu wake mkubwa wa kutokuwa makini wakati anapofikia hatua ya kutoa matamshi mazito yanayogusa masuala ambayo yumkini yanahitaji utulivu na ukomavu wa kiuongozi.

Nayaandika haya kwa sababu kubwa moja tu kwamba baadhi yetu tumejifunza kutokana na misukosuko ya kimadaraka iliyopata kulikumba taifa letu kama ile ya EPA, Richmond, Dowans na mengine mengi ambayo hitimisho lake lilithibitisha kwamba viongozi na waongozwa tumekuwa mabingwa wa kufikiri kwa mioyo badala ya bongo zetu.

Sina hakika ni lini hasa wanasiasa wetu walio serikalini au bungeni watakuja kutambua na kuisimamia kwa vitendo dhana iliyozoeleka vichwani mwao inayowataka watambue kuwa uongozi walionao ni dhamana kwa taifa na si neema ya kujisitiri na kulindana kwa malengo ya kujitwisha sifa bandia za ushupavu na ujasiri wasiostahili au ya kuwatoa kafara wachache ili kulinda mustakabali wa nyadhifa walizonazo.

Tujisahihishe
 
Hivi inaweza ikawa ni rahisi sana kwa Ngamia kujitahidi sana na kupenya kwenye tundu la sindano, kulikoni kwa Nyani kujitahidi kidog tu kugeuka nyuma na kuangalia kundule
 
Mkuu hakuna aliyewaza kuwa hipo siku Rais ya Libya ataishi mafichoni.No,lakini wakati unakuja CCM kutemberea kuchwa.Miaka inasonga mbele na siku ya kila mtu kufa zinakalibia,
IDD NJEMA
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mhh huyu mwandishi ni mahiri sana kwenye kazi yake,nataka kuuliza je? Amepata kufanya kazi na jenerali ulimwengu? Hii kitu ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na pinda ingekuwa jambo zuri sana lakini ukweli ni kwamba jambo hili liligubikwa na hasira waliyokuwa nayo waheshimiwa wabunge dhidi ya Jairo hasa kutokana na kuwafananisha wabunge na zekomedi
 
Wakosoaji wa Matukio wapo sikuzote,

Hakuna mtu anayetoa suluhisho, kila mtu analaumu tu, Kujiuzulu katika nchi changa (kiuchumi) sio jambo la tija (tena kwa mara ya 2),
Tuelekeze nguvu zetu na kuzijumuisha katika masuluhisho ya maswala mazito sio milioni 50 mara idara kadhaa,

Wale walio manguli wa kufikiri lazima waonyeshe mifano katika majibu ya maswali rahisi, kama njia ya haraka ya kunusuru janga la umeme, tatizo la muda mrefu la maji, miundo mbinu mibovu, huduma legelege za afya, elimu ya mafua, masuala ya mafuta n.k

Tuwe sehemu ya suluhu, sio sehemu ya matatizo!
Ni Ujinga kulalama na kulaumu kila sekunde

Wazo rahisi kwa Serikali: Tafadhali lindeni nyaraka vizuri, watu wanapoteza muda kwa mambo yasio na tija

Zimwi likujualo ......
 
Wakosoaji wa Matukio wapo sikuzote,

Hakuna mtu anayetoa suluhisho, kila mtu analaumu tu, Kujiuzulu katika nchi changa (kiuchumi) sio jambo la tija (tena kwa mara ya 2),
Tuelekeze nguvu zetu na kuzijumuisha katika masuluhisho ya maswala mazito sio milioni 50 mara idara kadhaa,

Wale walio manguli wa kufikiri lazima waonyeshe mifano katika majibu ya maswali rahisi, kama njia ya haraka ya kunusuru janga la umeme, tatizo la muda mrefu la maji, miundo mbinu mibovu, huduma legelege za afya, elimu ya mafua, masuala ya mafuta n.k

Tuwe sehemu ya suluhu, sio sehemu ya matatizo!
Ni Ujinga kulalama na kulaumu kila sekunde

Wazo rahisi kwa Serikali: Tafadhali lindeni nyaraka vizuri, watu wanapoteza muda kwa mambo yasio na tija

Zimwi likujualo ......
suluhisho zinafahamika ila zimekosa watendaji ndio maana tunasema kuwa WATENDAJI ambao ni JK na PINDA hawatui usiku wala mchana koungoza nchi hii.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wakosoaji wa Matukio wapo sikuzote,

Hakuna mtu anayetoa suluhisho, kila mtu analaumu tu, Kujiuzulu katika nchi changa (kiuchumi) sio jambo la tija (tena kwa mara ya 2),
Tuelekeze nguvu zetu na kuzijumuisha katika masuluhisho ya maswala mazito sio milioni 50 mara idara kadhaa,

Wale walio manguli wa kufikiri lazima waonyeshe mifano katika majibu ya maswali rahisi, kama njia ya haraka ya kunusuru janga la umeme, tatizo la muda mrefu la maji, miundo mbinu mibovu, huduma legelege za afya, elimu ya mafua, masuala ya mafuta n.k

Tuwe sehemu ya suluhu, sio sehemu ya matatizo!
Ni Ujinga kulalama na kulaumu kila sekunde

Wazo rahisi kwa Serikali: Tafadhali lindeni nyaraka vizuri, watu wanapoteza muda kwa mambo yasio na tija

Zimwi likujualo ......
Hata wewe umeishia kulaumu hujatoa suluhisho. Sanasana umeendeleza uozo kwa kushauri wafiche nyaraka, mawazo yako finyu ni kuwa mnavyoendelea kutuibia na kutafuna kodi zetu huku mnaficha siri ndio suluhu ya matatizo ya nchi hii. Suluhu ya matatizo ya nchi hii ni kuikataa CCM na viongozi wake wote na sera zake zote ili tuanze upya baada ya miaka 50 ya uhuru.
 
Waandishi kama hawa wanatuelisha sana sis vijana amin hilo tunajifunza sana
 
Hawa wote wameprove failure namkumbuka ha ta EL (ingawa leo sina hamu naye) alikuwa strong kuonesha PM anavyotakiwa kuwa hasa anapokuwa na rais goigoi
 
Mwandishi ninampongeza sana kwa kujitahidi kufafanua utendaji katika serikali iliyopo madarakani.

Ndugu watanzania mliopo hapa Jf mnaona jinsi hii ccm inavyoyumba, na kuthamini vyeo zaidi kuliko wanaowaongoza. Jamani tunaipeleka wapi Tanzania, tunajenga jamii ya namna gani? Mababu na mababu zetu na baba zetu wamevumilia sana na sisi tuseme basi na wao wanaojaza matumbo sasa watuvumilie. Tunasomesha vijana wetu ili wafanye nini, kama mashirika yamekufa na makampuni yote. Ndio tunasubiri wawekezaji wajekuajiri watoto wetu au vipi. Hii serikali inajivunia nini kwa taifa letu. Tunajua ya kuwa Tanzania tuna vitu vingi tu ambavyo serikali ingetilia maanani tungekuwa mbali kuliko hata Kenya.

Tanzania tunataabika leo kwa ajili ya hii kurugenzi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kutumiwa na mchwa wanaokula mpaka mti wa matunda wakati wanajua kesho watahitaji huo mti kwa ajili ya familia, (ccm).
 
Hongera sana Kibanda kwa maoni mazuri na ya kujenga. Natamani waadishi wengi wangekuwa na mtazamo kama wako kweli tungefika mbali. Kikwete ni mchovu na hii siyo siri kwani hili limeshaanza kufahamika vizuri sana kadri siku zinavyokwenda. Pinda ni dhaifu na hili nakubaliana na wewe kwa asilimia zote.

Hongera sana kaka kazi yako nimeikubali ...
 
Radi na Ngurumo za mwezetu Absalom Kibada ni ukweli usiopingika hata kidogo; kila kitu ni dili na 'kusikilizia' hapa nchini.

Na Absalom Kibanda

VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake wanaoongozwa na Rais Jakaya Kikwete wanapata jeuri ya kimamlaka na kuendelea kujiona mabwana wakubwa waliopewa dhamana ya kuendelea kuitawala nchi si kwa sababu ya ubora wao au weledi wao wa kazi na kiuongozi, bali misingi ...

.....kina Kikwete, Mizengo Pinda na wenzao wengine kufaidi matunda ya madaraka wakati ushahidi ulio wazi umekuwa ukithibitisha pasipo shaka kwamba katika umoja wao wanaunda
jeshi maarufu la viongozi wavivu wa kufikiri, wachovu wa kutenda, dhaifu katika kuona na wasanii katika maamuzi.

Matokeo ya uchovu na udhaifu walionao viongozi wa zama hizi za Kikwete wanaofikiri kwa ndimi zao na kuamua mambo mazito ya kitaifa kwa kuangalia mustakabali mwema wa matumbo yao na yale ya familia zao ndiyo ambao umetufikisha hapa tulipo leo.

 
Kilichonisisimua kwenye hii makala na kunifikirisha sana sio Pinda na Kikwete kuchoka maana hilo lipo wazi bali uwezekano wa Zitto kutumika kwa kujua au kutokujua ili ainusuru serikali ya Kikwete na anguko lingine la pili la aibu. Kwamba inawezekana aliitwa chemba akaambiwa 'bwana eeh...wabunge wanaweza kuleta motion ya eidha kutokuwa na imani na Rais au PM na kwa mwenendo wa mambo ulivyo hali inaweza kuwa mbaya..sasa kwakuwa wewe upo chama cha upinzani kaanzishe zengwe, tutakupa watu wa kuunga mkono na mambo yatakuwa poa...' akaandaliwa Ole Sendeka atoe hoja ya kuundwa kamati teule ili baadhi ya mazuzu waiunge mkono na hatimae hoja ikapita watu wakapigwa chenga ya mwili kisayansi. Kudadadeki walah siasa za bongo tamu
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni uchambuzi mzuri ila una walakini. Kibanda umemtaja Zitto alivyomwokoa Pinda kwa hoja yake lakini umetuacha hewani kwa kutotwambia dhamila au maslahi binafsi ya Zitto katika kumwokoa Pinda. Walakini huu unaongezeka pale gazeti lako tzdaima linapoonekana mala nyingi kuandika habari zinazomkosoa Zitto bila kutaja hata kidogo mazuri yake. Zaidi ikumbukwe wateule wengi wa JK wakiwemo Luhanjo na Jairo ni chaguo lake na maswahiba wake wakubwa isipokuwa Pinda ambaye aliipata hiyo nafasi isiyo na mamlaka ya kutosha kikatiba baada ya EL swahiba mkubwa wa JK kupata ajali ya kisiasa kwa muujibu wa JK ambayo watz tunajua alihusika kuliibia taifa kwa kuitumia Richmond. Haya na mengine mengi yananijengea wasiwasi juu ya huu uandishi wako ndugu Kibanda dhidi ya Zitto.
 
hawa watu wasanii sana ila kitawagarimu sana kutokana nakutokuwa na akili zakufikiria muda gani na nani atoe tamko au amri ni mchanganyiko wa kuendeleza kudidimiza ccm au uongozi kuendelea kuonekana mbovu hauna mwelekeo wasanii wasanii .
 
Maoni shupavu kutoka kwa Mwalimu wangu Kibanda. Nakubaliana naye kimsingi katika mengi aliyoyaongelea, hasa pale alipohitimisha...

Mambo ya namna hii ya kumuacha Rais anayefanya kazi ofisi moja na kwa ukaribu mkubwa wa kimaamuzi na Katibu Mkuu Kiongozi akiwa salama na pengine kuonekana shujaa hata katika jambo ambalo mikono yake inaonekana dhahiri kuchafuka yanawezekana katika nchi kama zetu tu.

Zaidi ya kukubaliana na mdau hapo juu MwanaCBE ambaye kama mimi nastaajabishwa jinsi gani gazeti la Tanzania Daima chini ya uhariri wa Kibanda lisivyompa support ya kutosha Zitto Kabwe katika makala zake, vile vile niseme tu kwa ujumla tusichanganye ukomavu wa "parliamentary democracy" kuwa unatokana na udhaifu wa Serikali moja kwa moja.

Kibanda anasikitishwa kwamba Pinda inabidi anyanyuke mara kwa mara katika nyakati zisizo zake na kwa dharura ili kutoa muongozo wa Serikali na kuwasaidia Mawaziri kujibu hoja. Mbona hii inafanyika wakati wote sehemu zingine (mfano katika Bunge la Uingereza chini ya PM kutoka vyama tofauti), lakini haichukuliwi kwamba ni udhaifu unaoiweka nchi nzima mahali pabaya?

Pengine ni kwamba hatujazoea kuona Serikali ikiwajibishwa, kwahiyo tusichukulie kuwa tunachoshuhudia ni ishara ya udhaifu per se. Isijekuwa katika jitihada za kujenga hoja za kisiasa dhidi ya Serikali ya CCM tunaepuka makusudi kutafakari kwamba kinachotokea hapa ni jambo jema la kuwa na "activist" parliament ambayo inaiamsha Serikali kufanya kazi inavyopaswa, na sio kwamba tunashuhudia mpasuko katika Serikali ambayo ipo njiani kuanguka kama Kibanda anavyotaka tuamini.

Kwahiyo natoa angalizo tu hapo juu, lakini kimsingi nakubaliana na hoja kwamba suala la Jairo nimeshughulikiwa vibaya mno, tena kwa kujali tu "bureacratic procedures" na sio kujibu suala zima la maadili katika mtindo wa uwezeshaji wa kupitisha Bajeti za wizara Bungeni.
 
Nimepata elimu kutokana na thread. Thanx Kabanda God bless u. Na ndo maana uwa sikosi Tanzania Daima maana huu ndo utamu wenyewe ninaoupataga. KIKWETE & PINDA ni mazuzu. Nchi inaangamia wao wanakalisha masaburi ofinin. Wanafiki sana
 
"CCM NI CHAMA CHA MASULTANI"Kauli ya Sumaye!kaongezea ccm kufa wasipojirekebisha!Die ccm!go to hell
 
Back
Top Bottom