Kibanda apelekwa kutibiwa Afrika Kusini

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda, kwa sasa yuko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.

Ndege imekodiwa na mwajiri wake. Hali yake si nzuri.

Tuungane kumwomba Mungu amjalie apone-arejee salama.

535441_348828325228148_1952363149_n.jpg
 
Mzee wa Kwembe Kati wewe huko salama? Maana mwenzako akinyolewa wewe tia maji.Nakupeni pole wanahabari na wapenda amani wote wa Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Mi mpaka sasa hivi hata sielewi ni nani waliofanya kitendo hicho. Tusubiri polisi wafanye uchunguzi.
 
Mzee wa Kwembe Kati wewe huko salama? Maana mwenzako akinyolewa wewe tia maji.Nakupeni pole wanahabari na wapenda amani wote wa Tanzania

Mungu si Mungu wa wadhalimu. Inatosha, inatosha! Mungu ingilia kati wauaji wote uwaangamize maana bila hatia wanamwaga damu za watu wako
 
Suleman kova yuko studio, kuweni wapole muda sio mrefu filamu mpya itatangazwa rasmi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
hata mimi nashangaa kwa sababu wakenya wamerudi kwao kupiga kura.

Sio wote waliorudi, nasikia kuna Wakenya zaidi ya 500 000 wanaishi nchini kwetu, hivyo wengine wamebaki wengi tu, ndio maana uhalifu hauishi!
 
Mzee wa Kwembe Kati wewe huko salama? Maana mwenzako akinyolewa wewe tia maji.Nakupeni pole wanahabari na wapenda amani wote wa Tanzainia

Kanga, unachosema ni kweli kabisa. Mimi naona hali si nzuri kwa wana habari. Muhimu ni kwamba kama tutatolewa uhai, jamii iwasaidie wategemezi tutakaowaacha! Kamwe hatuwezi kukaa kimya ilhali mambo ya nchi yakienda hovyo. Kwa Kibanda wamechelewa kwa sababu kazi aliyokwishafanya (Mungu amjaalie aendelee kuifanya) ipo kwenye maandishi. Tena basi, wakumbuke, maandishi hayafutiki! Woga ndiyo silaha dhaifu kuliko zote kwenye uwanja wa mapambano. Wanahabari na wapenda haki wote-tusonge mbele.
 
I hope watawahi hilo jicho maana nasikia the so called majambazi waliumiza sana jicho, mara wengine wanasema limetobolewa basi kila mtu lake. Jamani mwenye taarifa sahihi atupatie. Pole sana Kibanda na huko South upone. Nina hakika hutahitaji ulinzi mkubwa kama ule wa ulimboka alipokuwa huko!!!!!!
 
Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda, kwa sasa yuko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.

Ndege imekodiwa na mwajiri wake. Hali yake si nzuri.

Tuungane kumwomba Mungu amjalie apone-arejee salama.

mwajiri wake ni nani? tupeni taarifa ya tukio zima alitekwa? alivamiwa? au ni nini yaani hii kitu sielewi kabisa
 
Mungu katika Jina la Yesu Kristo atamponya kwakuwa yeye ni mtetezi wa taifa lake. Amen
 
Back
Top Bottom