Kibanda amemuudhi nani?

Kibaya zaidi wametumia strategy zilezile zilizotumika kwa Ulimboka wamejua wakitumia hizo hawatafikiriwa wao watafikiriwa walewale waliofanya kwa Ulimboka. Poor Him. get well soon. Ila mimi nafikiri Huyo mwandishi anajua zaidi na ndiye wa kusema ukweli.

Kitu kingine kinachonipa maswali. baada ya kusikia taarifa ya habari kuwa Mlinzi alipoona amevamiwa akaanza kuhangaika kuwaita majirani tema baada ya wavamizi kuondoka. Kwa nini alisubiri wavamizi waondoke ndio awaite majirani?

- Pia hiyo nyumba yake iko peke yake haijapakana na nyumba nyingine ambazo zina walinzi ambao wangeweza kuto msaada?

- Hivi alikuwa anaishi peke yake yeye na mlinzi tu? hakuna watu wengine kwenye nyumba alilokuwa anaishi?
nimejiuliza maswali hayo nimekosa majibu na pia nikahisi huenda pia Mlinzi alikuwa anajua au pia alikula njama na wavamizi. maana pia inaonekana alichelewa kufungua mlango makusudi ili tendo lifanyike. ni mawazo yangu tu. Unajua hali iliivyo sasa nchini kwenye inatufanya vichwa vyetu kila linapotoke tatizo na majibu yasipatikana tunakuwa tunawaza vibaya.

Mungu tusamehe waja wako.

Mkuu umejiuliza km mi.
Hivi anaishipeke yake?hana familia?
 
nawe pia inawezekana akili yako inapaswa kuchunguzwa , katika isue makini kama hii inayogusa jamii yetu badala ya kuchangia hoja za maana unaleta usiasa hapa.
 
hii nji ni mbaya kuliko tunavyodhan,na watu wanazidi kupandikiza chuki mioyoni mwao...
Balaa linatunyemelea
dini
sias
vinatupeleka kubay
 
Hali hii kwa waandishi wa habari mpaka Lini?Si Mara ya kwanza kuona waandishi wahabari Wakikumbwa na misukosuko yakupigwa na hata kuuwawa, ukweli inatiauchungu sana.

Nalazimika kuandika haya wenye kuchukia nawachukie na wenye kuona kuna haja ya mamlaka husika sasa kuchukua hatua stahiki kuhakikisha hali hii inakomeshwa wataungana nami.

Kwanza ilikuwa kwa Saed Kubenea na Ndimara walivamiwa huku kubenea akimwagiwa Tindikali tena ofisini kwake, baadae ikajakwa mwandishi wa habari Daudi Mwangosiambaye yeye aliuwawa, ikaja kwa mwandishi mwingine huko kanda ya Ziwa na leohii kwa mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absarom Kibanda, hali hii mpaka lini?

Ni ukweli usipingika kuwa katikakuandika kuna kundi litaguswa kwa mazuri na lingine litagushwa kwa kudhanilinaonewa, lakini hii ndio kazi yetu kuwapashahabari, kukosoa pale palipo na mapungufu, kusifia pale panapopaswakuelimisha na kuhabarisha .

Sasa katika hili wanataka tuandikehabari gani? Tuzipike habari? Tunahitajiuhuru wa habari jamani , tuwahabarishe watanzania , sasa tuandike nini ikiwa kila tunachoandika ni kibaya? Upo wapiuhuru wa habari?

Juzi Kubenea, jana Mwangosi , leo Kibanda Kesho sijui atakuwanani? Tunaliomba jeshi la polisi kufanya uchunguziwa kina kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Hii inatia uchungu sana na aliyefanya haya ana lengo moja la kudhoofisha fani na utendajiwetu, lakini hawajui kwamba tupo kazini na tunafanya kazi kwa manufaa yawatanzania wote.

Kama unaona huitaji kuguswa kwa mabaya na kalamu zetu basikuwa muadilifu, tukuandike kwa mazuri , kwa faida ya watanzania wote waliokomijini na wale wasiofikiwa. '' UKATILI ULIOFANYWA KWA KIBANDA UNAPASWAKULAANIWA VIKALI''Mungu msaidie Absalom Kibanda aponeharaka arudi katika utendaji wake wa kazi wa kawaida. Daima mbele haturudinyuma._________________________________

......

Mkuu samahani lakini wakati unaandika hii kitu ulikuwa unakimbizwa mbona umeunganisha maneno kama mntoto anayejifunza kuandika?

Ebu jaribu kutuliza akili kwanza kabla ya kuanza kuweka mawazo hapa.
 
Ilisemekana kuwa Dr.Stephen Ulimboka aliudhi watawala wa juu.Akatekwa,akateswa,akatupwa na siku ya pili akaokotwa Msitu wa Mabwepande. Sinema yake bado haijaisha.

Leo,'ametekwa' na kuteswa Ndugu yangu kiuandishi Absalom Kibanda. Sasa ameshatua Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kukosekana huduma stahiki Muhimbili na hospitali nyinginezo za Dar es Salaam.Naye ana majeraha kichwani na jichoni.Ameumizwa vibaya na yuko katika hali mbaya.

Absalom Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima linalosemekana kumilikiwa na CHADEMA(sina uhakika wa umiliki).Baadaye,akajiunga na New Habari Corporation kama Mhariri Mtendaji.New Habari Corporation inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na Rostam Aziz.

Ni juzi tu,Kibanda aliandika makala ya kumsifu Abdurahman Kinana akichagiza kuteuliwa kwa Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama cha Mapinduzi. Nimjuavyo Kibanda,ni mwandishi nguli na mahiri. Ni msema anachokiamini.

Kitendo cha kushambuliwa leo kinaacha maswali mengi. Kibanda amemuudhi nani tena? Kwanini sasa tabia ya kuteka na kutesa inaonekana kama ni dawa ya kuwakomesha wasemakweli?

Uchunguzi wa kina unahitajika hapa;tena haraka. Amasivyo,kila mtu atajilinda kwa namna anayoiona inafaa. Serikali ifanye kazi yake ya kuhakikisha ulinzi wa raia wake.

Mkuu kama wewe bado hujaanza kujilinda mwenyewe shaurilo, you are next..!
 
Mi nawashangaeni mnaoongeeea afu mnahitimisha kwa kuliomba jeshi la polisi lifanye UCHUNGUZI wa kina, kwa ulimboka mlisema hivyo hivyo, Kubenea pia, Mwangosi, yule mwandishi wa Kigoma, yule wa dar aliyepigwa risasi nyumbani kwake pia. Hivi bado tu mna imani na hilo jeshi..!?? Leo tu Kova kasema kilichompata Kibanda "sio kitendo cha kihalifu". bado mnaamini watafanya "uchunguzi wa kina"?
 
Tatizo waandishi hawana umoja na ni waendekeza njaa. Mwangosi ameuawa na polisi lkn bdo wanaendelea kwenda kumsikiliza Kova.ACHA WAWANG'OE MENO NA WAWATOBOE MACHO MPK MTAKAPOACHA UNAFIKI WENU
 
Wamiliki wa gazeti la Tanzania Daima wachunguzwe.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Angekuwa ni mwandishi wa Tanzania Daima basi shutuma zote zingeelekezwa CCM na kuna watu wangekuja humu na kujifanya wana ushahidi kama vile walikuwepo kwenye tukio. Sasa katika hili Chadema yapaswa wachunguzwe vinzuri.
 
Ukisema wamiliki wa Tanzania daima wachunguzwe huku ukidai linamilikiwa na cdm ina maana unataka cdm ichunguzwe! Hivi kwenye tukio la ulimboka ccm ilichunguzwa?

Pili, cdm imeshazoea kupambana na wasaliti kwa njia za kistaarabu. Kwa mfano madiwani wa arusha mbona hawajawahi kubugudhiwa? shonza na mwampamba mbona wanatesa majukwaani hawajahi kudhuriwa? Wahariri wa magazeti ya uhuru, mzalendo, daily news mbona hawajawahi kuteswa na cdm? Iweje huyu kibanda ambaye hana madhara yoyote kwa cdm ateswe? Kwa umaarufu gani hasa aliokuwa nao? Maadui wa cdm ni wengi na wala kibanda si mmoja wao kamwe. Cdm itaendelea kulaani vitendo vya utesaji vinavyofanywa na serikali ya ccm bila kujali itikadi ya aliyeteswa. Uvumi kama huu uliwahi kusambazwa na ccm wakati wa kifo cha mh. Wangwe eti cdm ilihusika! Kama ndivyo mbona sijaona wala kusikia kiongozi yeyote wa cdm amekamatwa? Watanzania wenzangu tuweke itikadi zetu pembeni tulaani kwa pamoja ushetani huu wa kikwete na wanafiki wenzie. Laana ya mungu i juu yao.


Wamiliki wa gazeti la Tanzania Daima wachunguzwe.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
jaman ebu ifike mahala mkue,hz c hoja bali porojo tu,ifke mahala mtoe majibu muafaka hata kama n ya kusadkika.polen nyote make naona mnajichanganya sana oohh mara t-daim oohh mara wale wa ulimboka nasem kueni nyote hiii si facebook.
 
jaman ebu ifike mahala mkue,hz c hoja bali porojo tu,ifke mahala mtoe majibu muafaka hata kama n ya kusadkika.polen nyote make naona mnajichanganya sana oohh mara t-daim oohh mara wale wa ulimboka nasem kueni nyote hiii si facebook.

Yawezekana upo sahihi, lakini ulipaswa kuyakemea haya tangu ishu ya Ulimboka. Waache wachambuane maana CDM huwa ni wepesi sana kuwanyooshea vidole wenzao hata bila kufanya uchunguzi. Mimi huwa sipendezwi sana na hii tabia but ni vema pro-Cdm wakajua kuwa unafiki si kitu kinzuri. Watu huwa wanaongea utumbo humu na still wanajiona wapo above others.
 
Mimi sio mwanasiasa na sipendi siasa ila najiwazia tu..

Kama Kibanda angekuwa alitoka gazeti la Uhuru akahamia Tanzania Daima.. Basi watu wangeisema/kuishutumu sana CCM..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Dah kweli watu wana mbinu chafu . Kibanda aliwasikia eti afande mpige risasi. Nia yao ni kuupaka matope utawala na jeshi la polisi. Sasa. Hata issue ya ulimboka nimebadilisha mawazo yangu.
 
Mungu amjalie apone haraka... ila waandishi wa habari kalamu zao ni hatari sana kama hawako makini..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom