Absalom Kibanda yuko sahihi, Nimeanza kumuogopa Kinana

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Katikamakala yake ndefu ya tarehe 22 Novemba 2013 mhariri mashuhuri BwanaAbsalom Kibanda aliandika wasifu wa Katibu Mkuu wa sasa wa Chama ChaMapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana baada ya uteuzi wake, katikamakala hiyo aliyoipa anuani "Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana."alinukuliwa katika miongoni mwa aya zake ikisema kuwa;

"..nimtu asiyejali au mpuuzi asiyejua vyema siasa za Tanzania anayewezaakasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baadaya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi mmoja wawanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu,mwanadiplomasia na kanali mstaafu wa jeshi, ABDULRAHAMAN KINANA kuwakatibu mkuu wa CCM.."

Baadaya makala hiyo ambayo ilikosolewa, kubezwa na kukosolewa hasa naviongozi wa vyama, taasisi na mashirikisho yenye mlengwa wa upinzaninchini, hatimaye Kibanda aliondolewa kutoka kampuni yake iliyomuajiriya free media akiwa mhariri mkuu na baadae kuhamia kampuni nyingineya Habari Corporation, pamoja na kufikwa na masahibu kadha wa kadhayaliyopelekea kumpa ulemavu wa kudumu.

Lakinisi Kibanda pekee, bali mwanazuoni, mwanasiasa chipukizi aliyehamaCHADEMA na kujiunga na CCM Ndugu Juliana Shonza nae aliandika makalaambayo aliisambaza kwenye mitandao ya kijamii yenye anuani "HUYUNDIE KINANA NINAYEMFAHAMU, MWALIMU WA SIASA NA KIONGOZI MWENYEUPENDO" ambapo kwenye makala hiyo, Shonza alisifu na kupongezahatua mbalimbali za utendaji na ufanisi wa Katibu Mkuu huyo.

Makalayangu italenga kutoa ushuhuda wa ukweli wa waliyoyaandika wanataalumahao, nikilinganisha na hatua na mafanikio mbalimbali ambayo Chama ChaMapinduzi kimeyapata kwa muda mfupi tangu kuteuliwa kwa NduguAbdulrahaman Kinana kuwa katibu mkuu.

Kwanzakabisa ningeanza kukumbusha jambo ambalo pia lilikumbushwa na muasisiwa TANU na CCM Baba wa Taifa hili, marehemu Mwalimu Julius KambarageNyerere katika hotuba yake aliyoitoa katika ukumbi wa Chimwaga mwaka1995, alipowakumbusha wanaCCM juu ya asili ya kuundwa kwa CCM,aliwaambia kuwa Chama Cha Mapinduzi hakijawa chama cha matajiri,akawakumbusha kuwa msingi wa kuundwa TANU na baade CCM ni kuwasemea,kuwatetea na kuwasaidia wanyonge, masikini, wakulima na wafanyakaziwa nchi hii.

Kwa hali ilivyokuwa awali ni kama vile tayari wanaCCMhasa viongozi walianza kusahau msingi huu na jukumu hili lakimaumbile la CCM. Kinana ameirudisha CCM katika msingi na asili yakuundwa kwake, CCM ya leo chini ya Kinana ndio inayohakikisha kuwamatatizo ya wakulima wa nchi hii yanapatiwa ufumbuzi, kero zawafanyakazi zinatatuliwa na sauti ya wanyonge inapazwa na kusikikakupitia Chama Cha Mapinduzi, tumeona na kushuhudia katika ziara zakealizofanya kote nchini, Ndugu Kinana akiwa na wananchi wa kawaida,mabalozi wa nyumba kumi, wenyeviti wa mtaa na vitongoji wakila pamojana kujadili pamoja.

Lakini pia tumeshuhudia maduhuli, posho na malipoya walimu na wafanyakazi wa Serikali na Mashirika yakitolewa baada yasauti za wafanyakazi hao kubebwa na Katibu Mkuu huyo wa CCM,tumeshuhudia bei ya korosho, Mahindi, Ufuta na utaratibu wa manunuziukiboreshwa baada ya sauti ya wakulima kupazwa na Katibu Mkuu huyo waChama tawala.


Katikamambo ambayo yameendelea kumfanya Kinana aonekane kiongozi mwenyemaono na uwezo wa kipekee ndani ya Chama ni hatua yake ya kuamuakukirudisha Chama katika msingi wa utumishi kwa watu. Chama kimerudikuwatumikia wananchi, wanyonge na masikini wa nchi hii. Viongozi waChama Cha Mapinduzi leo wanaweza kusimama na kutembea kifua mbele kwamafanikio na kazi nzuri ambayo inaendelea kufanywa na viongozi waChama hicho ya kuisimamia Serikali.

Miongonimwa mambo yaliyodhihirisha uwezo mkubwa aliokuwa nao Komredi Kinanani pamoja na ukweli kuwa Komredi amekabidhiwa Chama kikiwa na mpasukomkubwa wa kimakundi ambayo yalitishia kukizamisha Chama katikanyakati tofauti lakini kwa maoni na ufanisi wa hali ya juu KatibuMkuu huyo aliweza kuimaliza hatari kubwa iliyotokana na mpasuko huondani ya Chama, na sasa wanaccm ni wamoja, wenye mshikamano tenaimara na madhubuti kuliko awali.

Haliya uchumi wa Chama imeendelea kuimarika na maslahi ya watumishi waChama Cha Mapinduzi yameendelea kuboreshwa siku baada ya siku, ambapopamoja na kupanda kwa mishahara lakini pia viwango vya posho kwaviongozi, watumishi na watendaji wa Chama yameendelea kuboreshwa hatakwa watendaji na viongozi wa ngazi za chini kabisa kama makatibu wamatawi na wajumbe wa nyumba kumi ambao hapo awali hawakuwa katikautaratibu wa malipo.

Lakiniuimara huu wa Chama Cha Mapinduzi katika siasa za upinzani zinatoatafsiri moja kuu kuwa ni kudorora na kufifia kwa Upinzani nchini.Kila CCM inapozidi kuwa maarufu na kuendelea kuimarika kwenye mioyoya watanzania, ndipo kwa kasi hiyo hiyo upinzani unazidi kusahaulikana kufa kifo cha kawaida. Tumeshuhudia kupoteza mwelekeo kwa vyamavya upinzani nchini kukiongozwa na Chama kikuu cha Upinzani Chademaambapo viongozi wake wamekuwa wakihaha kukinusuru chama hicho ambachotayari kinachungulia kaburi.

Nadhaniwale ambao walibeza awali wameanza kumuelewa Kibanda hivi sasa,lakini wakati Bongo zao zikijitahidi kufanya tathimini ya uzito naukweli wa maneno ya Kibanda tayari wamejikuta katika mazingira ambayohawana tena utulivu na murua wa kufanya tafakuri jadidi ya kesho yaona vyama vyao. Huyu ndiye Kinana ambaye wanasiasa mashuhuri nawachambuzi wanamuogopa, nami naungana nao kwani sasa NIMEANZAKUMUOGOPA KINANA.
 
Super Dentist....huyu alitakiwa awe jela

images (1).jpg download.jpg images.jpg
 
KAULI mbiu ya 'Tutawasaka, Tutawakamata Popote Walipo' si ngeni tena masikioni mwa watu. Imezoeleka na watu wa rika zote pengine kutokana na hulka ya muasisi wake, Lazaro Nyalandu, kupenda sana ‘kujitokeza' kwenye vyombo vya habari hasa televisheni. Kwa kutumia kauli mbiu hii, Nyalandu alifanikiwa kuwaaminisha watu kuwa yuko makini na amejizatiti kikamilifu kupambana na ujangili, hasa wa tembo.

Wapo waliotahadharisha kupitia magazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba Nyalandu si kiongozi makini kama ilivyo matarajio ya wengi, kwamba hakuwa na lolote jipya. Wakatabiri kuwa angeivuruga Wizara aliyokabidhiwa katika kipindi kifupi. Katika shaka yao hiyo, baadhi walimtafsiri Nyalandu kama muumini mkubwa wa pesa na madaraka. Wapo waliofikia hatua ya kufananisha uteuzi wake na kitendo cha kumpa fisi ajira ya kulinda bucha la nyama, wakitilia shaka uadilifu wake katika vita dhidi ya ujangili.

Iliripotiwa kwenye mitandao ya jamii kuwa mara tu baada ya Balozi Hamis Kagasheki kujiuzulu, watuhumiwa wakubwa wa ujangili jijini Arusha walikutana katika hoteli moja maarufu na kufanya sherehe kubwa. Watuhumiwa hawa hawa wadaiwa kufanya tena sherehe kama hiyo kusherehekea uteuzi wa Nyalandu. Kitendo hiki kikapewa tafsiri moja tu na baadhi ya watu, kwamba Kagasheki alikuwa mwiba mkali kwa majangili na Nyalandu inawezekana kwa kiasi fulani ni kipenzi cha majangili. Ikawekwa wazi kwamba viatu vya Kagasheki havimtoshi Nyalandu.

Baadhi ya waandishi wakakumbusha mambo kadhaa yanayokinzana na maslahi kwa uhifadhi na taifa ambayo Nyalandu aliwahi kuyafanya au kushinikiza yafanyike akiwa naibu waziri! Kwa mfano, walihoji umakini wa Nyalandu pale alipowahi kushinikiza TANAPA ilipie milioni 560 kwa ajili ya mashindano ya Miss East Africa wakati nchi ikikabiliwa na janga kubwa la ujangili.

Wakakumbusha misuli aliyotumia Nyalandu kuisaidia Kampuni ya Asante Tours kukwepa kulipa tozo mbalimbali za Serikali. Wakagusia lile sakata la Nyalandu kuungana na baadhi ya kampuni kushinikiza mabadiliko ya mfumo wa tozo za hoteli kwa wageni ili uwe flat rate. Mabadiliko haya yangekubalika yangeipotezea TANAPA shilingi bilioni 70 kwa mwaka. Na zaidi wakakumbusha vitimbi vyake wakati akiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Kimsingi, waandishi hawa walitaka kutuasa kuwa kaulimbiu ya 'Tutawasaka, Tutawakamata Popote Walipo' ni ghiliba, uwongo, utapeli na usanii. Ni takriban miezi sita sasa tangu Nyalandu aukwae Uwaziri wa Maliasili na Utalii. Kaulimbiu hii bado inavuma kama maporomoko ya maji ya Udzungwa. Swali ni je, Nyalandu amewasaka na kuwakamata majangili wangapi hadi sasa? Je, mikakati yake ni ya uhakika (practical) au ni usanii mwingine? Je, ni kweli kwamba ana nia ya dhati kupambana na ujangili?

Itakumbukwa kwamba haukupita mwezi tangu ateuliwe kuwa Waziri, Nyalandu alianza vitimbi. Akaita zaidi ya waandishi wa habari 30 na kutangaza kuwaondoa wakurugenzi wawili wa Idara ya Wanyamapori kwa madai ya kutokuridhiswa na utendaji wao katika vita dhidi ya ujangili. Nyalandu akaagiza kuwa lazima kila mtumishi wizarani, kuanzia yeye mwenyewe, awe na viashiria vya utendaji (performance indicators) vitakavyopima utendaji wake. Kila mtu akaamini kuwa kweli huyu kapania kuchapa kazi. Aidha, akadai kuwa sababu nyingine ya kuwaondoa ni kutekeleza Azimio la Bunge lililotaka wasaidizi wa waziri waondolewe kutokana na kukiukwa kwa haki za binadamu wakati wa Operesheni Tokomeza!

Alichosahau Nyalandu ni kwamba yeye ndiye aliyekuwa msaidizi mkuu wa Waziri, hivyo alitakiwa aanze kuondoka! Hata hivyo, kwa sababu anazozijua, Nyalandu alichepuka ukweli halisi, kwani kilichoazimiwa na Bunge kilikuwa kuundwa Tume ya Mahakama ambayo ingechunguza sakata zima la Operesheni Tokomeza.

Kwa mujibu wa Hansard ya Bunge, Waziri Mkuu akiunga mkono kauli ya Mwanasheria Mkuu, alitamka maneno haya kutokana na kuwasilishwa ripoti ya Operesheni Tokomeza:

"…inawezekana kabisa pengine kazi hii (Ripoti ya Kamati) siyo timilifu, pengine inahitajika kufanyika zaidi. Taarifa walizozipata ambazo zimehusisha mambo fulani fulani inawezekana vilevile zinahitaji kuthibitishwa zaidi, na zithibitishwe kwa utaratibu ambao utatupa uhakika kwamba, wale wote ambao wamehusika wanashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu."

Nyalandu hakumuelewa Mwanasheria Mkuu wala Waziri Mkuu. Na cha kushangaza zaidi akafanya uteuzi wa wakurugenzi ambapo aliwaweka watu wenye rekodi inayotiliwa shaka katika utendaji. Mteule wa Nyalandu katika nafasi ya ukurugenzi mkuu ndiye aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uzuiaji Ujangili ambaye pia aliongoza Operesheni Tokomeza field.

Nafasi ya mteule huyu ilichukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Pori la Rungwa ambalo ndilo lililokubuhu kwa ujangili. Baadhi ya waandishi wamekuwa wakiwataja mabwana hawa kama manabii wa ujangili. Mshangao – Waziri anatiliwa shaka umakini wake dhidi ya ujangili, kisha anateua watu wanaotuhumiwa kwa ujangili. Halafu anatuambia – tutawasaka na kuwakamata popote walipo!

Mmoja wa waliong'olewa, Profesa Jafari Kadeghesho, alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kwa maana hiyo majukumu yake yalikuwa hayahusiani moja kwa moja na suala la uzuiaji ujangili na wala hakuhusika kwa vyovyote katika upangaji na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Ni kutokana na utata huu, mwandishi mmoja akashangaa mtunza stoo kufukuzwa kazi kutokana na mafundi kupindisha ukuta wa jengo huku ‘site manager' akipandishwa cheo.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba, kisheria na kikanuni, Nyalandu sio mamlaka ya uteuzi wala nidhamu kwa wakurugenzi hao. Alitekeleza uamuzi huo wenye utata bila kumshirikisha Katibu Mkuu kwani alijua kuwa Katibu Mkuu ni mtu makini na asingemuunga mkono hasa kwa kuwa, katika kipindi chao kifupi wizarani, wakurugenzi aliowaondoa walifanya kazi kwa uadilifu na weledi kiasi cha kuleta ufanisi mkubwa kiutendaji.

Kwa kadri siku zilivyokuwa zinakwenda, huku falsafa ya 'kuwasaka na kuwakamata popote walipo' ikiendelea kupasua anga, sababu za kung'olewa Profesa Songorwa na mwenzake Kadeghesho zikaanza kuwa dhahiri. Nyalandu alifanya uamuzi wenye utata ambao kwa vyovyote vile si Songorwa wala Kadeghesho wangeukubali. Pengine ili kuwafurahisha wafanyabiashara kwenye tasnia ya uwindaji, alipuuza sababu za kisayansi na kutangaza kurefusha msimu wa uwindaji kutoka miezi sita hadi tisa.

Hili likafuatiwa na kituko kingine. Akatumia mamilioni ya walipa kodi kugharamia ziara ya Martin Fletcher (na mwenzake) kutoka Daily Mail on Sunday la Uingereza. Katika makala yake, Fletcher aliichafua Tanzania na kumdhalilisha Rais wetu. Serikali ilikanusha vikali na kufikia hatua ya kulalamikia udhalilishaji huu kwenye ubalozi wa Uingereza.

Katika busara ya kawaida, tungetaraji Fletcher afunguliwe mashtaka kwa uzushi. Cha ajabu, Nyalandu akaamua kutumia mamilioni ya fedha kumzawadia ‘rafiki' yake huyostudy tour (ziara ya mafunzo) kuja Tanzania ambapo aliwalaza Serena na kuwapa ndege ya Serikali kwenda Selous kutalii. Aidha, akathubutu kuvunja sheria za nchi ili kuwafurahisha pale alipowaruhusu waingie kwenye ghala la meno ya ndovu na kupiga picha! Haya ameyafanya wakati anajua kuwa askari wetu hawana sare wala buti; magari yako kwenye mawe kwa kukosa vipuri na hamna mafuta ya kufanyia doria!

Nyalandu anahalalisha dhambi hii kwamba amefanya hivyo ili kumsaidia Fletcher kuandika 'a balanced story.' Hata hivyo, Nyalandu hajatuambia kuwa lengo hili lilifanikiwa kwa kiasi gani. Je, kitendo cha Fletcher ‘kutuvua' nguo hadharani baada ya ziara hii ndio ‘balanced story' aliyotegemea Nyalandu? Hata hivyo, mzungu huyu wa Nyalandu mwenyewe akasema bila kutafuna maneno kwamba aliuona mwaliko wa Nyalandu kama kituko cha mwaka!

Lakini hebu shangaa zaidi! Wakati Nyalandu anajikomba kwa wazungu, anawaponda waandishi wazalendo waliofichua mpango wake na James Lembeli wanaotajwa kutaka kuuza hifadhi akiwaita waandishi uchwara huku akishindwa kujibu hoja kwa madai kuwa zinampotezea muda kuwasaka na kuwakamata majangili! Mbona basi asiwasaidie waandishi hawa wazalendo kuandika a balanced story? Au tuamini kuwa waandishi wazalendo wana kazi moja tu ya kumsifu na kutangaza falsafa yake ya "Tutawasaka, Tutawakamata Popote Walipo?"

Ili kuendelea kuuzuga umma kuwa kazi ya kupambana na ujangili imepamba moto tukatangaziwa kuwa ujangili umepungua kwa asilimia 58 katika kipindi cha siku 37 tu tangu Nyalandu apate uwaziri kamili! Hata hivyo, hatukuambiwa vigezo (variables) gani vimetumika kuja na hii asilimia 58.

Tangu tutangaziwe mafanikio haya miezi minne imepita. Falsafa ya 'Tutawasaka, Tutawakamata Popote Walipo' imeendelea kuwa kibwagizo huku waandishi wa habari wakilipwa mamilioni ili kumtangaza na kumuonyesha Nyalandu alivyo ‘serious' kwenye vita dhidi ya ujangili. Yametumika mamilioni kuweka mabango yanayokemea ujangili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, tumekabidhiwa ndege za kupambana na ujangili (ingawa wambea wanadai kuwa ni feki), Waziri amekabidhiwa hundi ya dola za Marekani milioni 2.25 na marafiki zake TGTS ili kupambana na ujangili, Waziri ametumia mamilioni kuandaa mikutano mikubwa na kupanga mikakati ya kupambana na ujangili.

Hapa mtu makini lazima ajiulize; kama Nyalandu huyu aliweza kupunguza janga la ujangili kwa asilimia 58 katika siku 37 tu tangu ateuliwe kuwa waziri, inakuwaje katika kipindi cha miezi minne na katika kipindi ambacho amekuja na mikakati mipya, fedha na vifaa zikiwemo ndege ashindwe kumaliza asilimia 42 ya ujangili iliyobaki? Hapa sio anachezea akili za watu? Tunataka Nyalandu atoke hadharani akanushe habari kuwa si kweli kwamba sasa hivi ndio ujangili umepamba moto, pengine kuliko kipindi kingine chochote kilichopita!

Nyalandu hana nia ya dhati ya kupambana na ujangili hata kidogo. Tumeshuhudia alivyoungana na rafiki yake Lembeli kujaribu kushiriki mchezo mchafu wa kutaka kukabidhi uendeshaji wa hifadhi na mbuga zetu kwa asasi binafsi ya Afrika Kusini. Baada ya uchafu huu kufichuliwa alikataa kata kata kwamba serikali haina mpango wa kukabidhi hifadhi za taifa, mapori ya akiba na maeneo mengine yaliyo chini yake kwa asasi binafsi.

Hata hivyo Nyalandu huyu hasemi kilichompeleka Afrika Kusini kukutana na African Parks Network (APN). Alichofanya ni kuyashutumu magazeti yaliyofichua mpango huo akidai kuwa ni waandishi uchwara (gutter journalists) wanaotumiwa na majangili ili Serikali ipoteze muda kujibu badala ya kuwasaka na kuwakamata majangili!

Hadi leo Nyalandu hajatuambia kuwa kwa kugoma kujibu hoja hii ya ‘kuuza' hifadhi kumemsaidia kuwakamata majangili wangapi. Harakati zinazoendelea wizarani ni maandalizi ya kupeleka baadhi ya watu na wabunge E
)
thiopia, Chadi, Afrika Kati, Rwanda na Malawi eti kujifunza utendaji wa APN. Tujiulize, kama Serikali haina mpango wa kukabidhi mbuga yoyote kwa APN, Wizara inatumia mamilioni ya fedha (zaidi ya USD 120,000 kutuma watu kwenda huko kufanya nini? Je, huu ndio mkakati wa kuhakikisha kuwa falsafa yake ya "tutawasaka na kuwakamata" inatekelezeka?
 
Naikumbuka sana makala hii. Kwa kifupi kupitia makala hii bwana Kibanda ALIRUBUNIWA na akakubali KURUBUNIKA. Kibanda alijishushia hadhi na kujidhalilisha mno mbele ya jamii kupitia makala hii ambayo aliitoa kupitia Gazeti la Tanzania Daima akiwa kama Mhariri mtendaji. Ilikuwa ni makala iliyo onyesha kila dalili ya 'kunyea kambi' ikiwa ni wiki chache tu kabla ya kutangaza kujiunga na magazeti ya RAI.

Na ndio kuna watu wengi mno ambao hawakumuonea hata huruma wala imani baada ya kufanyiziwa na utawala wa kidhalimu ambao alikuwa ameanza kuupigia upatu. Makala ambayo ilikuwa karibia ya mwisho kabla ya kuhama magazeti ya Tanzania Daima kwenda kutumikia gazeti la RAI chini ya bosi mpya yule fisadi wa EPA Rostam Aziz. Itamchukua muda sana Kibanda kujirudishia heshima yake tena katika jamii tokea alipoishusha kwa siku moja tu kupitia mkala hii.
 
Zile tuhuma za Kibanda kuwa ni jangili ziliishia wapi? Au ndio yao yale kybebana. Upinzani Tanzania hauwezi kufa hata mhonge vipi km mlivofanya kwa kina Zitto
 
Naikumbuka sana makala hii. Kwa kifupi kupitia makala hii bwana Kibanda ALIRUBUNIWA na akakubali KURUBUNIKA. Kibanda alijishushia hadhi na kujidhalilisha mno mbele ya jamii kupitia makala hii ambayo aliitoa kupitia Gazeti la Tanzania Daima akiwa kama Mhariri mtendaji. Ilikuwa ni makala iliyo onyesha kila dalili ya 'kunyea kambi' ikiwa ni wiki chache tu kabla ya kutangaza kujiunga na magazeti ya RAI.

Na ndio kuna watu wengi mno ambao hawakumuonea hata huruma wala imani baada ya kufanyiziwa na utawala wa kidhalimu ambao alikuwa ameanza kuupigia upatu. Makala ambayo ilikuwa karibia ya mwisho kabla ya kuhama magazeti ya Tanzania Daima kwenda kutumikia gazeti la RAI chini ya bosi mpya yule fisadi wa EPA Rostam Aziz. Itamchukua muda sana Kibanda kujirudishia heshima yake tena katika jamii tokea alipoishusha kwa siku moja tu kupitia mkala hii.
Kwanini hampendi kuruhusu kila mmoja akawa na fikra huru, kwanini kila ambaye anafikiri tofauti na nyie awe ni amerubuniwa..? hivi ni kwamba tafsir ya uhuru wa mawazo imewapita pembeni au ni kule kuendelea na kuathiriwa na tabia za kikabe ndiko kunakowafanya muone kuwa nyie ni miungu watu ambao kauli zenu, maono yenu na fikra zenu hazipaswi kukosolewa wala kurekebishwa.

Kibanda aliandika makala hiyo akiwa mwandishi tena mhariri aliye huru na timamu, aliandika anachokiamini ambacho si tu kuwa ndicho kinachotokea leo bali ni jambo ambalo kila mwandishi makini na mtu yeyote anayewaza sawasawa anashuhudia kuwa kibanda alikuwa sahihi kuwa na woga kwa Kinana.

Suala sio kunyea kambi bali uhalisia wa uteuzi na mtu aliyeteuliwa ndicho kilichompa msukumo na ujasiri mwanahabari huyo kuyaandika aliyoyaandika, japo alijua kuwa atazodolewa, atakosolewa na kushutumiwa, na kweli hayo yametokea lakini pia yametokea zaidi ya hayo ambayo hakuyategemea kuwa Makala hiyo imemsababishia ulemavu wa kudumu wa kimaumbile.

Heshima ya Kibanda bado iko juu na kila mtu makini awe mwandishi, mwanasiasa ama mwananchi wa kawaida anajua nafasi na hadhi ya Kibanda mbele ya jamii ya watanzania.
 
Zile tuhuma za Kibanda kuwa ni jangili ziliishia wapi? Au ndio yao yale kybebana. Upinzani Tanzania hauwezi kufa hata mhonge vipi km mlivofanya kwa kina Zitto
Ni vigumu kuamini kuwa mawazo ya aina yako yanatolewa katika jukwaa linaloitwa "la great thinkers" ni aibu na kufedhehesha jukwaa. Hauna hoja, ni nadharia na uzushi wa maneno ya kutunga juu ya ukweli kuwa kifo cha upinzani ama chadema hakitokani na CCM.

Ni vyema sasa mkaacha kuisema CCM vibaya na kuinyooshea vidole kwa yale ambayo mmeyatenda kwa mikono yenu na mkiwa na akili na fikra huru bali muandae msako wa mchawi wenu ndani yenu.

Maneno ya kutunga na kuzusha kuwa Kibanda ni jangili hayakufanya kazi na hayatofanya kazi kwa sasabu kila mmoja anamjua kibanda ni nani.,na watu wanajua kuwa amesema kweli kibanda kuwa CHADEMA kiko alasiri na muda si mrefu wataenda kulala.
 
Ni vigumu kuamini kuwa mawazo ya aina yako yanatolewa katika jukwaa linaloitwa "la great thinkers" ni aibu na kufedhehesha jukwaa. Hauna hoja, ni nadharia na uzushi wa maneno ya kutunga juu ya ukweli kuwa kifo cha upinzani ama chadema hakitokani na CCM.

Ni vyema sasa mkaacha kuisema CCM vibaya na kuinyooshea vidole kwa yale ambayo mmeyatenda kwa mikono yenu na mkiwa na akili na fikra huru bali muandae msako wa mchawi wenu ndani yenu.

Maneno ya kutunga na kuzusha kuwa Kibanda ni jangili hayakufanya kazi na hayatofanya kazi kwa sasabu kila mmoja anamjua kibanda ni nani.,na watu wanajua kuwa amesema kweli kibanda kuwa CHADEMA kiko alasiri na muda si mrefu wataenda kulala.

Naona vjana wako wa propaganda hapo LUMUMBA WAMEKWENDA CLUB MAISHA WAMEKUACHIA LINDO ..AMA FUNGU LIMEKATA?
 
Kwanini hampendi kuruhusu kila mmoja akawa na fikra huru, kwanini kila ambaye anafikiri tofauti na nyie awe ni amerubuniwa..? hivi ni kwamba tafsir ya uhuru wa mawazo imewapita pembeni au ni kule kuendelea na kuathiriwa na tabia za kikabe ndiko kunakowafanya muone kuwa nyie ni miungu watu ambao kauli zenu, maono yenu na fikra zenu hazipaswi kukosolewa wala kurekebishwa.

Kibanda aliandika makala hiyo akiwa mwandishi tena mhariri aliye huru na timamu, aliandika anachokiamini ambacho si tu kuwa ndicho kinachotokea leo bali ni jambo ambalo kila mwandishi makini na mtu yeyote anayewaza sawasawa anashuhudia kuwa kibanda alikuwa sahihi kuwa na woga kwa Kinana.

Suala sio kunyea kambi bali uhalisia wa uteuzi na mtu aliyeteuliwa ndicho kilichompa msukumo na ujasiri mwanahabari huyo kuyaandika aliyoyaandika, japo alijua kuwa atazodolewa, atakosolewa na kushutumiwa, na kweli hayo yametokea lakini pia yametokea zaidi ya hayo ambayo hakuyategemea kuwa Makala hiyo imemsababishia ulemavu wa kudumu wa kimaumbile.

Heshima ya Kibanda bado iko juu na kila mtu makini awe mwandishi, mwanasiasa ama mwananchi wa kawaida anajua nafasi na hadhi ya Kibanda mbele ya jamii ya watanzania.

Moja ya miiko mikuu ya vita ni kumuheshimu Adui yako,regardless of uwezo wake, CDM na wapinzani, mlichelewa kumuheshimu Kinana, na uwezo wake kama adui yenu kwenye upambanaji wa kimbinu na kimkakati.wakati nyie mkiweka mapambano yenu mikononi mwa "red-hots" kina lema, CCM walikubali yaishe wakamkabishi maduguli mastacooker wao.

Yule bwana ni moja ya viongozi wachache wa CCM wenye uwezo wa kimkakati wa hali ya juu, Havard hakwenda kushangaa yale ma-hall.

CDM mmechelewa, tambueni hilo, jipangeni, mumuheshimu adui yenu, hapo mtakuwa na some chance ya kumshinda.
 
TandaleOne - Wewe endelea kumbeba na kusema unayajua juu ya Kibanda. Na sisi tuliyemfahamu Kibanda wacha tunene ya kwetu tunayoyajua vilevile kupitia uhuru huo huo wa mawazo.

Kwani ninaposema Kibanda ALIRUBUNIWA na yeye akakubali KURUBUNIKA ilikuwa ni hivyo na vinginevyo. Na alitumia mwamvuli au kichaka hicho hicho ucho kiita 'fikra huru' kupitia taaluma ya uana habari anayoitumikia. Kwani hata mimi leo hii naweza kukukanyaga kwa kudhamiria (makusudi ) na mwisho wa siku nikakupa 'samahani' yako na nikuaminishe kuwa ilikuwa bahati mbaya. Na mwisho wa siku ikawa dhamira yangu ikawa imetimia:). Na hicho ndicho alichokifanya Kibanda katika lugha nyepesi.

Lakini waweza endelea kumbeba na kumpaka mafuta utakavyo....lakini bado naamini makala ile ili mdhalilisha na ilimgharimu taaluma yake mpaka leo kama vile alivyojidhalilisha Prof. Shivji kwenye mjadala wa Katiba unao endelea nchini.
 
Sio kweli kuwa sasa ccm imeacha kuwakumbatia matajiri na kuwagalagaza wanyonge. Wanyonge wa Tanzania ni wakulima ambao ni zaidi ya 90% ya watu wote. Kuwajali hakutafutwi kwenye majukwaa bali ktk utendaji. Utendaji kumo katika mfumo wa upangaji wa uchumi ambao uwianishwa ktk mapato na matumizi ktk bajeti. Je ktk bajeti ya hadi juni 2015 mkulima amepewa unafuu gani kuanzia jinsi atakavyolima, kufuga. Kuvuna, kusafirisha, kuhifadhi, kuuza na mipango anuai kadhaa. Inajulikana dhahili kinachokwaza na kuwapandisha chati wapinzani ni ufisadi, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali na mali asili ambavyo ktk wakati huu ktk ccm vimetamalaki. Twambie Kinana amefanya nini na sisi tu muogope? Huku Kanda ya Ziwa, Kagera kahawa ilishafika sh 1500 kwa Kinana inatelemuka sasa ni sh 800 kwa kilo. Pamba hivyo. Wakati bei inatelemuka jirani zetu Uganda ni 2500 hadi mbunge wetu Tibaijuka anazuia serikali ituachie tuuze kahawa yetu magendo. Ukichanganya kuna upungufu wa chakula kutokana na mnyauko wa migomba na serikali haitujali.
 
Kibanda alisema kweli wengine wakambeza ngoja waone matunda yake daima ukweli haufichiki kinana ni zaidi ya tunavyomfahamu kwenye siasa za tanzania matokeo yake yameonekana kwa haraka sana.
 
Hata mimi namwogopa sana Kinana kwa hatima ya tembo wetu masikini. Hili jambazi la kisomali ni hatare!!
Kinana amefanya viongozi wa vyama vya upinzani washindwe kabisa kumudu vyama vyao nakuwa waropokaji na kufukuzana bila kujenga vyama vyao.
 
Huyu Nape kama anaendelea kujifariji kuwa Kinana amejenga CCM labda ni kwenye mitandao. Strong hold ya CCM ambayo ilikuwa vijijini sasa imetekwa na CHADEMA ,sisi tunaoishi huku vijijini ndo tunaona. Kwa ujumla CCM kama itabakia kujitapa kwenye mitandao na vyombo vya habari mwakani 2015 watashangaa na kama si viongozi wengi wa CCM kufa kwa kihoro. Ninachowashauli ni kuzingatia ushauri wa mwenyekiti wenu JK ( ingawa mnamdharau) mjiandae kisaikolojia kuwa wapinzani. Kamanabisha andaeni uchaguzi wa serikali za mitaa muone kazi itakayowapata. Mdharau meiba huota tende, shauri yenu.
 
Naendeleza: Hakuna ccm imeishagundua kuwa vijijini Kanda ya Ziwa hasa Kagera ambako ndiko kulikuwa ngome ya ccm sasa kumebomoka vibaya na ninyi mumebakia kumusifia Kinana. Vyama vya ushirika vilivyokuwa mioyo ya wakulima zamani sasa ni kampuni tanzu za ccm, wizi na ubadhirifu vinalindwa maadam sherehe na ziara za ccm zimachotewa fungu zuri sasa vyama vya ushirika havipo kwa ajili ya wakulima tena. Hili hawa wanyonge wanaliona wakati mikakati ya cdm inaonekana wakijhpanga. Natabiri baada ya uchaguzi wao ndipo utajua kuwa Kinana si chochote. Kinana sijui mnampimia nn? Yeye alijua kupendwa kwa cdm ni makosa ya utendaji wa ccm. Je utendaji umebadilika na kuwa mzuri? Yeye ni kuutabanisha ktk mikutano na watendaji kuwaita mizigo huku wao wakizidisha machungu kwa wananchi. Hapo ccm itapaa na cdm kuporomoka au kinyume chake? Hicho ndicho cha kumuogopea na kumsifia? Hata mnafikia kusema hayo ndio matunda ya Havard? Achana za kuleta za huyo msomali, cdm are more strategic subiri utaamini hivi karibuni.
 
Makala makini, nimeisoma na kuielewa.
Bahati mbaya kwa wengi hasa wapinzani wa CCM, hawa watu ambao wanaweza kuwa na maono ya kupima na kuzingatia mambo hasa katika hali hii ya Upeo, wengi ni wababaishaji wasio na mwelekeo na wasiojua kujifanyia hata tathimin binafsi achilia mbali tathmini ya vyama vyao.
 
Back
Top Bottom