Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Kama mlivyoliona gazeti la Mtanzania la leo Jumamosi mtagundua ghafla limebadilika sera -- yaani kuanzia sasa ni 'twanga chadema kotekote' bila ya huruma au kupumzika.
Change hii inatokana na kutua kwa Absolmi Kibanda kama Mhariri Mkuu pale New Habari na kapewa hadidu za rejea moja tu -- kwamba kama anataka kumrithi Salva pale Ikulu, basi ahakikishe mtu wake EL anatinga pale Mjengoni mwaka 2015.
Kwa maneno mengina sasa hivi tutaanza kuliona Mtanzania likitetea mafisadi na wale wote wanaodhulumu haki za wananchi wanyonge -- litakuwa linaangalia zaidi wale wenye nazo.
Kwa maana nyingine tena ni kwamba gazeti hilo, (pengine pamoja na lile la Rai) linaingia rasmi katika kundi la magazeti uchwara (gutter press) kama vile Sauti Huru, Hoja, Tazama na kadhalika, na asahau kulifanya liwe serious challenger kwa magazeti makini kama vile Mwananchi na Nipashe.
Angalau gazeti la Tanzania Daima (alikotoka Kibanda) lilikuwa limejijengea heshima yake ya kipekee na kuliwezesha kulipandisha mauzo hadi kuwa mojawapo tishio kwa hayo magazeti mengine makini niliyotaja.
Ni kamari kubwa anacheza Kibanda kwani anavyopanga Mungu katika mustakabali wa kisiasa wa nchi hii -- hata kwa mwezi mmoja ujao -- hakuna anayeweza kujua. Lakini nampa hongera kwa kuwa na ujasiri kuchukua uamuzi mzito kama huo.
Ila ajiangalie pale New Habari -- kuna vigogo na vigogo wa wahariri wakuu wamepita na karibu wote waliondoka kwa manung'uniko makubwa. Hakuna haja ya kutaja orodha. Pale pana pepo mbaya sana.
KILA LA KHERI MR KIBANDA!