Kibaki Kacharuka, Kikwete Mbona Uko Kimya?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,679
70,979
Michezo ya Kimataifa kama Olimpic na mingineyo huwa inabeba Utaifa na ni njia mojawapo ya kulitangaza taifa pia kulijengea heshima. Katika michezo iliyopita ya London, jirani zetu Kenya walifanikiwa kupata medali 11. Dhahabu 2,Fedha 5, na Shaba 4. Na sisi hapa kwetu kama kawaida tuliambulia patupu.

Katika hali isiyo ya Kawaida Rais wa Kenya amecharuka na kuamua kuunda tume ya kuchunguza kwa nini Kenya imepata medali hizo 11 pekee na si zaidi ya hapo? Hii inaonyesha ni jinsi gani Rais Kibaki anavyopenda heshima ya nchi yake iendelee kuwa juu zaidi ya hapo ilipofikia.

Kwetu sisi pamoja na aibu ya kutopata kitu, ni Business as usual. Habari hiyo ndio imetoka wala hakuna hata tamko lolote. Mheshimiwa Rais wetu wewe umeridhika? mbona kama kuna medali hata moja tuu ingepatikana ungeiitisha Ikulu kuipokea kwa mbwembwe? Tafadhali nawe chukua hatua katika hili sio kujisifia kuleta makocha tuu ambao wanaishia kulipwa vizuri na heshima yetu nje inazidi kupotea kwa kutokufanya vizuri.

Mkuu charuka na wewe.
 
Hatukuzoea mambo hayo huoni hata jembe la kulima kwa mkono tunaagiza nje ila ngoma tunaweza kutengeneza
 
Jengeni uchumi kwanza, michezo gharama, gharama zinataka uchumi.

Nigeria wametumia USD 15 million kuandaa timu ya Olympic na hawajafanya lolote la maana. Possibly because that was not enough according to their strategy.

Watu masikini mnataka kujitutumua kwenye extravagant fleeting shows, wakati watoto wanasumbuliwa na njaa, utapiamlo na ujinga.
 
Timu ilikuwa na viongozi wengi kuliko wachezaji. Medali zingepatikanaje sasa? Nchi hii ni ufisadi tu kwa kwenda mbele.
 
Jengeni uchumi kwanza, michezo gharama, gharama zinataka uchumi.

Nigeria wametumia USD 15 million kuandaa timu ya Olympic na hawajafanya lolote la maana. Possibly because that was not enough according to their strategy.

Watu masikini mnataka kujitutumua kwenye extravagant fleeting shows, wakati watoto wanasumbuliwa na njaa, utapiamlo na ujinga.

Haihitaji uwe tajiri ili ukimbie mbio! Kuna michezo mingi ambayo siyo lazima uwe tajiri, kenya si matajiri kihivyo! Wao wamejikita kwenye riadha ambayo hata sisi tuna uwezo wa kujikita.
 
Unawezaje kuchachamaa kwa kukosa mavuno kwa usichopanda? serikali haikuwekeza chochote kwenye hiyo timu ya olimpiki leo itakuwa na haki gani ya kuhoji kuboronga kwake, JK ametumia tu busara kidogo aliyonayo kukaa kimya!
 
Jengeni uchumi kwanza, michezo gharama, gharama zinataka uchumi.

Nigeria wametumia USD 15 million kuandaa timu ya Olympic na hawajafanya lolote la maana. Possibly because that was not enough according to their strategy.

Watu masikini mnataka kujitutumua kwenye extravagant fleeting shows, wakati watoto wanasumbuliwa na njaa, utapiamlo na ujinga.
Kweli mental slavery ni mbaya...

Hata ukiwa maskini kiasi gani, always there is a starting point. Kujikita kwenye michezo kama riadha za mbio ndefu na amateur boxing kwa nchi maskini kama yetu sio gharama kama unavyodhani, tatizo hakuna initiatives kutoka serikali dhaifu ili private sector iendeleze. Only kwa kuwa unaamini kila kitu kizuri wanafanya wazungu wenye hela.
 
"Watanzania wakirudi na medali ya aina yoyote kutoka olimpiki, nachana vyetu vyangu pamoja na vya chuo kikuu" - Gidabuday
 
Rais wetu hajukani kama ni moto,vuguvugu au baridi,mwacheni amalizie muda wake labda tutapata chaguo lingine la Mungu wa ukweli maana chaguo la hili halijulkani ni la Mungu yupi
 
Washiriki wa5 ila jopo la watu 23 lilienda London, mwingine alienda na mkewe na ni kiongozi mkubwa tu wa chama hicho. Mungu sio Juma si mkewe akaugua ikabidi amrudishe kimyakimya TZ coz gharama asingemudu.

My Take..
WALIENDA KUTALII!
 
"mnataka medali kwani mmezigaramikia?"
"kwanza tumefanya vizuri sana tumekuwa wa 34 kati ya 104 waliokuwa wanashiriki mbio hizo".
 
Kwa TZ hilo ni jambo la kawaiiiiiiiiiiiiiida, hakuna haja ya tamko. TZ hakuna utamaduni wa ushindani, kwa hiyo hatuchukii kushindwa. TUNACHUKIA kutokuteuliwa. Kila kitu ni kuteua, kuteua, kuteua kwa kwenda mbele: huwezi kupata the best kutoka kwenye uteuzi, unapata watu wa kushindwa. ILI tushindane na kushinda, lazima tuachane na mfumo wa uteuzi, tupambane: kama ni majaji, watu wapambane kupata; kama ni mkurugenzi, watu wapambane; kama ni mpishi, pia watu wapambane nk
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom