Kiba & Diamond: Msingoje mchoke ndio mtafutane, the time is now

Kiba & Diamond: Msingoje mchoke ndio mtafutane, the time is now

Tua Ngoma

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2015
Posts
3,337
Reaction score
8,782
Leo nilikuwa nikitizama project za one8 na one campaign. Moja ya vipaji nilivyovishuhudia humo ndani ni wabongo, mtoto wa kihehe Alli kiba na mtoto wa kimanyema Diamond Platnumz. Nimesikia zile back vocal za Kiba katika Hands Accross the world, jamaa anajua. Nimesikiliza Single boy, My everything na Cindelela, jamaa ni talented tena sana kwa Africa labda wizkid kwa mbaali anagusa vocal za Ali kiba.

Nimesikiliza ngoma ya Africa rise up, Cocoa na Chocolate, Mbagala, Kamwambie, My number one na ntampata wapi. Diamond anajua ana kipaji, ana swagg, ni talented. Ukiangalia hizo video utagundua hata madirector wa hizo video za project, yaani one8 na one campaign, walikubali uwezo wa hawa jamaa wawili ndo maana wamekuwa wakiwaonesha sana hawa watu kwenye hizo nyimbo... Ali kiba na Diamond wanaweza kuteka muziki wa Africa na dunia kwa ujumla.

Jamaa hawa wanahitaji kushare skills zao ili kufanya mziki mzuri zaidi ya huu wanaofanya. Ni wakati wa hawa watu kushirikiana kufanya kazi pamoja na kuipaisha Tanzania kwa pamoja.

Msingoje mpaka mchoke, mpoteze mashabiki, mpoteze mvuto ndiyo mpatane na kufanya kolabo, haitaleta maana, Haitakiki, Haitawapa hela, itakuwa kama nyimbo ya underground wanaojifurahisha.

Wakati ni sasa, acha utoto fanya kazi, tafuta hela..

#TeamWCB
#AFTER THE MIDDLE FINGER INC.
 
Hiyo si lazima wao wapatane ila hata wewe unaweza kutumia FULSA KWA KUWAWEKA CHINI NA KUONGEA NAO BIASHARA
 
Hiyo si lazima wao wapatane ila hata wewe unaweza kutumia FULSA KWA KUWAWEKA CHINI NA KUONGEA NAO BIASHARA
Mi nasoma wewe....ada tu imenishinda ntaweza kuwaunganisha madangote hao,labda nimuombe jembe ni jembe
 
Hilo ni wazo zuri na fursa kwa atakae waunganisha na wao pia.Nakumbuka miaka kadhaa ilopita kuna mtu aliwaunganisha banza stone,muumini na choki watu watalikumbuka tukio hilo wote walikuwa vizuri sasa hawa vijana wetu wakiacha umimi wakaitizama fursa ni waqt wao na kama asemavyo mleta uzi waqt ukuta.
 
Mwenye uwezo wa kuwaunganisha anafaidika zaidi na bifu hili lisilo na kichwa wa miguu na hakika hayuko tayari kusikia wanapatana na naamini wanachokianda ni show kwenye jukwaa moja unakumbuka ile ya tigo kati ya wanaume halisi Vs family ile tour ilivyowapa mpunga basi subiri dalali wao anajipanga.
 
Kanumba alifariki akiwa na bifu na Ray. Hata kuongea walikua hawaongei.
 
Wakiungana mie nahamia kuwa mshabiki wa rich mavoko....waungane na sie na timu zetu tule wapi?....napinga hoja....bifu lao ndio biashara na mkate mezani kwetu.

Mumesahau bifu la pac na bigie?.....hakuna kuungana mpaka mwisho wa dunia kwa mmoja wao au wote.....kuungana kwao kutauwa biashara zetu....na wema na zari hakuna kuungana pia wema na kajala hakuna kuungana.....bifu ndio zetu na maisha yetu bila bifu hayaendi.

Hata mengi akiungana na rostam azizi mie pia nitapinga...bifu mwanzo mwisho

hata jeikei akiungana na mamvii mie nitapinga ...mwendo wa team el na team membe mpaka kieleweke....bifu ndio zetu.

Ingekuwa kuungana kisa sauti nzuri ndege kibao tuu huko porini wangeungana...bundi angeungana na kasuku bonge la beat...kasuku anachombeza bundi ana-rap kigangstarrrr....bifu ndio jadi yetu.

Kama vip simba na yanga ziungane tuwatowe waarabu....

Kifupi napinga hoja ya kuungana ...bifu ndio mtaji wetu wao zao sauti
 
Wapuuzi number one ni mashabiki wa Kiba na Diamond lakini kwa bahati mbaya hili halizuiliki ni lipo kila mahali lakini wapuuzi number 2 lakini ingawaje ni number 2 na ndio wapuuzi wakubwa zaidi ni wasanii wenyewe kwa kukubali kuburuzwa na upuuzi wa mashabiki wao! I hate to say this, inawezekana Ali Kiba is far better than Diamond lakini ni Kiba ndie anayemwetaji zaidi Diamond kuliko Diamond anavyomwitaji Kiba! Kwa sasa Diamond ana uwezo wa kufanya collabo na almost any musician in Africa lakini Kiba hana uwezo huo! Sasa ikiwa Kiba na Diamond wote ni wapuuzi nadhani Kiba ndie mpuuzi zaidi kuliko Diamond kwavile hakutakiwa kuburuzwa na emotions za mashabiki wake wakati anarudi!!

Waswahili husema, ujinga hafi mtu! Kiba aombe tu collabo na Diamond! Nafahamu, kwa kuwa wote ni wapuuzi, Diamond atajiona Kiba ameenda kutafuta kutoka kupitia kwake... mashabiki wa Kiba nao itabidi waingie mitini na wasitokee mitandaoni kwa kuwa hawatakuwa na ubavu wa kubisha tuhuma hizo, ambazo, hata kama Diamond ndie ataomba hiyo collabo, mashabiki ake watasema anataka kumsaidia "bwana mdogo...!" na mashabiki wa Kiba hawatakuwa na ubavu wa kupinga hili!!

Hivyo basi, hakuna shaka kabisa kwamba Kiba ana uwezo mkubwa ingawaje amekosa mbinu! Asione taabu kuomba collabo na Diamond, Diamond hawezi kukataa hata kidogo kwanza kwake itakuwa ni "fahari", kwamba Kiba jeuri yote kwishinei! Ninaamini hata Diamond akiomba collabo na Kiba, Kiba hawezi kukataa unless awe na inferiority complex! Funzo kwa Kiba hapa ni moja... aliyeomba collabo iwe Diamaond au Kiba mwenyewe; itaonekana yeye ndie mwenye shida anayetafuta kutoka... kwahiyo unless kama hayipo tayari kabisa kufanya kazi na Diamond lakini kama yupo tayari lakini kuanza yeye kuomba collabo anachelea kuonekana anatafuta msaada; basi hata kama atakayeomba ni Diamond bado ataonekana anatafuta msaada tu! Lakini akizingatia msemo wa Kiswahili kwamba Ujinga Hafi Mtu, basi anaweza kupuuza yote hayo!
 
kuna watu watawachukia wote wawili
What about you? Utawachukia wote? Yaani Watanzania tulivyo watu wa ajabu jamaa wakishapatana tu, jukwaa la celebrities hapa JF linadoda on the spot!!!!
 
Kwani Diamond si anaimba na wasanii wengine au hao wakoje?
 
Back
Top Bottom