1. Pigana kwa muda mfupi kujua japo ufundi kidogo wa gari
2. Nenda kasome VETA kozi ya udereva,tafuta leseni kubwa class C na jizoeze kuendesha magari ya kawaida madogo kama Hilux na Toyota Land Cruiser
3. Baada ya hapo nenda chuo cha taifa cha madereva pale mabibo (NIT) soma (a) Advanced driver course grade two
(b) Advanced drive course grade one
(c) Senior driver course na itakuchukua muda wa miezi mitatu na nusu tu.
4. Ambatanisha na vyeti vyako vya elimu secondary au hata kama wewe ni muhasibu au una masomo yoyote yale,bora uwe na sifa hizo zitakazokuwezesha kupata kazi kwa ulahisi watakapoona sifa hizo.omba kazi ya udereva kwenye mashirika makubwa nakuhakikishia hutazunguka sehemu mbili tatu utapata kazi na ukiwa huko ukichoka udereva kusafili kwingi utakua na nafasi nzuri ya kuomba kazi nyingine kulingana na ulichosoma awali kama ni ulisoma mambo ya afya,utunza fedha,na nyinginezo
5. Driver wengi wa mashirik wanapata pesa kulingana na safari nyingi za kikazi na hata mishahara pia maana dereva wa mashirika wana mishahara hata zaidi ya walimu hapa nchini na hii itakufanya kubadilisha maisha yako ukiwa na uchungu wa maisha na ukiwa mzuri wa matumizi na kutunza akiba.
6. Epuka kabisa kuona aibu uombapo kazi ya dereva eti tu kisa wewe ulisoma Sociology Course au CPA ktk vyuo vikuu.angalia utapataje pesa na utatunzaje familia yako na mengine ni baadae.
7. Nimekua dareva wa mashirika kwa miaka 10 na mpaka leo nimeweza kujitegemea kuendesha mambo yangu japo kwa uchache lakini kusiko kwa kujuta
Go now.
JAH RASTAFARI MORNING AFRICA