kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,633
- 7,021
Hiki ni kiapo cha ndoa ambacho hufanywa na mengi ya madhehebu ya kikristo!Hata hivyo biblia ambayo ni kitabu kinachoaminiwa na wakristo wengi kuwa ni kitakatifu,kinasema"Msiape!"Kwa kuwa binadamu hana uwezo wa kuubadili unywele mmoja kuwa mweupe.Yaani kwamba sisi binadamu uwezo wetu una mipaka.Sasa hili suala la kuapishana wakati wa kufunga ndoa lilianzishwa kwa vigezo gani?Kuna mapungufu hayavumiliki mf baada tu ya kiapo unakuta mwanaume ni impotent au akapata maradhi ya ghafla akawa katika hali ya kushindwa kabisa kujamiiana!Kiapo kitavunjika?Kumbuka pia imeandikwa mtimizie Bwana nyapo zake!Hili limekaaje?