Tufute Upotoshaji kuwa mwanaume na mwanamke ni Sawa.

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
6,505
13,648
Inaonekana kwasasa jamii yetu na ya Dunia kwa ujumla ina struggle katika kujua sifa za asili za mwanamke kwa kuzingatia misingi ya mahitaji ya kijinsia.

Tokea kuumbwa kwa ulimwengu viumbe viliumbwa katika msingi wa kutegemeana ili kuweza kufunction katika dunia hii na kuishi.

Mfano ukienda porini simba hula wanyama walao nyasi, wanyama walao nyasi hula nyasi, nyasi hutegemea rutuba itokanayo na vinyesi vya wanyama, mizoga yao, na mabaki ya mimea mingine inayooza ili kuendelea kustawi.

Utegemezi huu ndio huunda mfumo wa Maisha ya wanyama kama tuyajuavyo. Vivo hivyo hata katika mifumo mingine kama mwili wa binadamu, viungo hutegemeana katika kumpa mwanadamu uhai, mfano, figo huchuja na kusafisha damu, moyo husukuma damu mwilini kote, ini hukusunya sumu na kuzificha ili izitoe, seli zikihakikisha micro activity zote za mwili zinakwenda sawa, lakini ubongo ukihakikisha hizi process zote zikiratibiwa bila kusimama wala kuzubaa, huku ubongo ukitegemea hivi viungo tajwa kupatiwa mahitaji yake ndipo uweze fanya kazi.

Kwa formula ile ile ya utegemezi, wanadamu tulipewa jinsia mbili ya kiume na kike ambazo kiutendaji zimetofautoana sana na hazifanani hata kidogo. Kuanzia maumbile ya uzazi, mahitaji ya chakula, nguvu za mwili na misuli, maumbile ya mwili, uwezo wa kiakili, namna ya kuprocess taarifa, uvaaji, kuhimili changamoto nakadhalika.

Katika utofauti huu ndipo umuhimu wa kuishi pamoja unapokuja ili kupunguza taabu zinazotokana na utofauti wa uumbaji.

Miaka ya kadhaa nyuma mataifa ya kimagharibi yakiongozwa na Marekani, yalianzisha, kukuza na kusambaza kasumba kuwa jinsia ya kiume na kike zipo sawa na zinafanya majukumu sawa sawa na hata zikiwa hazipo pamoja basi hakuna mapungufu. Wakafika mbali hadi kuja na hoja kwamba hizi jinsia zinaweza kuishi katika hali ya jinsia ile ile moja kuwa pamoja na wakaishi kama watu wengine, wendawazimu wa karne.

Miaka ya hivi karibuni mataifa ya magharibi kupitia mawakala wao yaani Feminists, CIA, balozi, vyombo vya habari, majarida, NGO’s na kadhalika wameendelea kusambaza wendawazimu kwa ustadi mkubwa na kufanikiwa kutumia madhaifu ya ukosefu wa elimu sahihi ya sayansi ya kijamii yaani sociology katika jamii changa kuziaminisha kuwa mwanaume na mwanamke ni viumbe sawa.

Rai yangu ni kwamba ni wakati sasa jamii yetu itupie jicho kali eneo hili na kuibua mijadala ili kuweza kukiokoa kizazi hiki na kijacho kutokana na upotofu wa kifikra huu ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kupokea taarifa zisizosahihi kutoka mataifa ya magharibi na kuziingiza katika mitaala ya elimu na mipango ya kijamii bila kujiridhisha uhalali wale na maudhui yake yanalenga nini katika kizazi chetu.

Mwanaume na mwanamke SI viumbe sawa na hawafanani katika maeneo yote. Kulazimisha kuprove hili, itakuwa katika gharama ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa mfano sasa tunaona madhara ni wanawake kuzaa nje ta ndoa kwa wingi, watoto wasio na baba mzazi karibu, vijana wa kiume wanaojinasibu kuwa na haiba ya kike, watoto wa kike wanao jiona ni wanaume, wanawake wanaohudumia na kulea familia kama baba wa familia, wanaume wanaolelewa, wanawake wasiojua kulea watoto, na kadhalika.

Tujitafakari.
 
Hivi Mwanamke alie kwenye Siku zake za Hedhi (tumbo kukoroga na tumbo kuvuruga) anaweza kuendesha Roli la Mafuta na kulifikisha Salama kutoka Kapilimposhi mpaka Kurasini Da' salama au kuwafikisha abiria walio kwenye Ndege/Meli akiwa kwenye uchungu wa kuzaa?
 
Hivi Mwanamke alie kwenye Siku zake za Hedhi (tumbo kukoroga na tumbo kuvuruga) anaweza kuendesha Roli la Mafuta na kulifikisha Salama kutoka Kapilimposhi mpaka Kurasini Da' salama au kuwafikisha abiria walio kwenye Ndege/Meli akiwa kwenye uchungu wa kuzaa?
Hapo anaweza itia kwenye mtaro mzee balaa la ile kitu huwa wanavurugwa balaa.
 
Hivi Mwanamke alie kwenye Siku zake za Hedhi (tumbo kukoroga na tumbo kuvuruga) anaweza kuendesha Roli la Mafuta na kulifikisha Salama kutoka Kapilimposhi mpaka Kurasini Da' salama au kuwafikisha abiria walio kwenye Ndege/Meli akiwa kwenye uchungu wa kuzaa?
kawaulize wale akina mama wanaoendesha magari makubwa ya mafuta, je wamewezaje?

Kwanza sijui nani amekwambia kuwa mwanamke akiwa kwenye siku zake basi tumbo hukoroga na kuvuruga. Kila mtu anareact kivyake vyake na kuna wengine hata hawana habari kwa siku kufika.

Usichanganye vitu ukaweka wote kwenye chungu kimoja, kama nyinyi wanaume kila mmoja yuko kivyake basi na wanawake wako hivo hivo.
 
Walipaswa kubaki kwenye "Haki za mwanamke"...wakaja kupotoshwa wakaja kwenye usawa wa jinsia...

Matokeo yake Simba na swala wanatakiwa kuwa na "Haki Sawa "..
Hasara ni kubwa Kwa wote..
 
Nature itajisettle yenyewe buda.... huu mkanganyiko utaendelea in the end utafika mwisho na dunia itajichekecha yenyewe kutengeneza eco system.....

Shida kubwa ni kwamba huko zamani mwanamke alikua anakandamizwa in many ways sote tunajua (mfano huwezi kuwa na ardhi bila mume au niaba ya nduguyo wa kiume, fursa za kielimu, fursa za kazini, huwezi achika hata kama umegeuzwa ngoma, mnaweza pangwa wengi kadiri mume anavyojisikia.... etc), katika kutafuta tobo la kutoka kwenye huu mfumo ndo kumeleta mkanganyiko wa kimaslahi na watu bado wanazidi kutake advantage

Mabadiliko yanawezekana kila mtu kwa nafasi yake binafsi na kizazi chake kadri awezavyo, ila society kubadilika itachukua muda sana after very massive destruction

Tulipo sasa ni kwamba:

FOR A MAN, OTHER THAN PROVIDING WHAT ELSE DO YOU BRING TO THE TABLE?
mwanaume nguvu ya uchumi pekee haitoshi sababu wanawake wanafanya kazi pia and wengi tu wanatengeneza pesa nyingi kuliko waume zao

FOR A WOMAN OTHER THAN SEX WHAT ELSE DO YOU BRING TO THE TABLE?
Sikuhizi ngono ipo kila mahali and hata mtu akitaka mtoto kuna watu hawaoni shida kuwa single mama kama baba unatoa matunzo

Pia hao hao wamama wa zamani, wengi tu ukiwauliza how they made it that far watakujibu sio kwamba walitaka ila mazingira hayakuruhusu

Hiki ni kipindi ambacho ukisimamia misingi ya tofauti zetu za kijinsia na kila mtu akiplay part yake, utaenjoy sana maisha ya ndoa na hata interactions za humu duniani,
HUWEZI JICHANGANYA NA VIKUNDI VYA KIJINGA VYA TOXIC FEMINISM
 
Back
Top Bottom