Gama
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 13,266
- 4,716
JF, nimetafakari kwa makini huu mwenendo mpya wa viongozi wa vyama kuamua kuwafukuza baadhi ya wanachama, kwa maono yangu mwenendo huu ukiachwa uendelee hakika usalama wa taifa utaenda mrama. Najiuliza, hivi kweli hawa wanaofukuzwa ni wakosefu kwa kiasi hicho? Hivi hawa wanaowafukuza wenzao hawaoni kama wanawaumiza watanzania pia kwa kuliongezea taifa mzingo wa kuchagua viongozi wengine-mf. Kuchagua mbunge, je inapofikia mahali hata mtu aliyepewa dhamana ya kugombea urais naye akavuliwa uanachama, je, wanaotekeleza haya hawaoni kama iko siku watamvua uanachama mtu ambaye sasa anatazamwa na taifa zima na si wanachama wa chama chake pekee?, hivi msajili wa vyama anasema nini kuhusu hili?, je, jamii haioni sasa kuwa kunahaja ya baadhi ya wanachama, mf, mnbunge, waziri au mgombea urais kuwa na kinga ya vurugu za ndani ya vyama?!, nawasilisha.