Siasa safi itatokana na uzalendo wa kitaifa wa wanachama na siyo matakwa ya wenye Chama

Nov 15, 2019
35
113
Licha ya uhuru wa kisiasa uliopo nchini kwa sasa ni mapema sana kusema kwamba hali ya siasa imeshakuwa shwari.

Siasa inayoendelea hivi sasa ni ile ya kuvuta utayari na kuwaaminisha watu kuwa kuna kile walichokimis ambacho kimsingi kwa sasa wanapaswa kukitarajia. Hii hali ni hatari katika siasa kwa kuwa aliyewekeza zaidi anaaminika zaidi kuliko anayetafuta mtaji.

Upatano uliopo (compatibility) kati ya "chama A", chama "B" na vyama vinginevyo unapaswa uwe na mipaka imara tena isiyoyumbishwa kwa malengo makuu matatu:-
  1. Kulinda imani ya chama kwa wanachama wake.
  2. Kutoa nafasi kwa chama kujitengenezea mikakati huru na ya ziada ya kiuendeshaji, na
  3. Vyama kuweza kupimana nguvu katika mlengo wa kuushawishi umma na hata kuibua dosari (loopholes) zilizopo kwenye miradi ya kiserikali.
Viongozi wa vyama vyote vya siasa wanapaswa kuwa mbali na kujitenga kabisa na ushawishi wa viongozi wa vyama hata kama ni chama tawala ili kuweza kulinda nguvu yao katika baadhi ya mambo na hatimaye waweze kuepukana na maneno kama vile kulambishwa asali na mengineyo mengi.

Kwakuwa Taifa ni letu sote na sisi ndio watanzania basi hatuna budi kukumbushana na kuwa siasa ianzie kwenye roho zetu na ibebe dhamana iliyokusudiwa na siyo kugeuza cheo na nafasi tulizonazo kujinufaisha, tutawaponza watanzania.
 
Back
Top Bottom