Kiama cha kufukuza wanachama na maslah ya taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiama cha kufukuza wanachama na maslah ya taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gama, Dec 19, 2011.

 1. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  JF, nimetafakari kwa makini huu mwenendo mpya wa viongozi wa vyama kuamua kuwafukuza baadhi ya wanachama, kwa maono yangu mwenendo huu ukiachwa uendelee hakika usalama wa taifa utaenda mrama. Najiuliza, hivi kweli hawa wanaofukuzwa ni wakosefu kwa kiasi hicho? Hivi hawa wanaowafukuza wenzao hawaoni kama wanawaumiza watanzania pia kwa kuliongezea taifa mzingo wa kuchagua viongozi wengine-mf. Kuchagua mbunge, je inapofikia mahali hata mtu aliyepewa dhamana ya kugombea urais naye akavuliwa uanachama, je, wanaotekeleza haya hawaoni kama iko siku watamvua uanachama mtu ambaye sasa anatazamwa na taifa zima na si wanachama wa chama chake pekee?, hivi msajili wa vyama anasema nini kuhusu hili?, je, jamii haioni sasa kuwa kunahaja ya baadhi ya wanachama, mf, mnbunge, waziri au mgombea urais kuwa na kinga ya vurugu za ndani ya vyama?!, nawasilisha.
   
 2. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  Mkuu Gama, heshima mbele.

  Maswali yako ni ya msingi sana.

  Mfano ni huyu kijana Kafulila, mimi kwa mtazamo wangu naona hii tabia itafutiwe ufumbuzi na ufumbuzi wenyewe ujali maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

  Nionavyo mimi mtu akishachaguliwa kuwa mbunge na wananchi ipitishwe sheria ya kuwa hakuna mtu anayeweza kumvua ubunge isipokuwa wananchi waliomchagua wenyewe... inabidi chama husika kisubiri mpaka next election wakati wa kupendekeza maina ya wagombea, otherwise :

  1. Ni kutowatendea haki wale waliomchagua na
  2. Ni kufuja kodi za watz

  Mbatia ndio tatizo NCCR kwa mawazo yangu.
  Waliobaki na wanaomsupport ni wale aidha wenye upeo mdogo(wale wanaoitwa wazee wa chama) au ni wale wenye maslahi binafsi...

  Chama kimekuwa mali ya Mbatia.
   
 3. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Chama ni lazima kiwe na mfumo wake ambao wanachama ni lazima waufuate.
  Suluhisho ni kuwa na mgombea binafsi katika nafasi zote za kugombea.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  una huruma kama jk
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wakizisoma na kuzielewa katiba za vyama vyao watasalimika kufukuzwa. Vinginevyo hakuna dawa nyingine zaidi ya kuwatoa berenge! Hapa ndipo unapogundua umuhimu wa mgombea binafsi
   
 6. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ufujaji wa pesa za umma unakuja tena! Magamba wanajpanga kupga campen kwa helkopta 3 kwa mpigo! Pesa za wanyonge kuliwa tena, mishahara kucheleweshwa mara dufu!
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  hatupaswi kushabikia mfumo,sheria,katiba etc ya chama inayoonekana kutojali haki ya wapiga kura, kumbuka kuwa mbunge hachaguliwi na wanachama tu bali wananchi wote kwa kumuadhibu mbunge unakuwa umewaadhibu wapiga kura wote hata wale wasio wanachama. Kuna haja ya kuwa na kinga juu ya watu hawa ili kuepusha maamuzi yanayolenga kumkomoa mtu na yasiyo na tija.
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuna mijitu humu ndani.......inapiga vita suala la mgombea binfasi......halafu yenyewe inajifanya kulaumu uamuzi wa NCCR.....damn!
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ukiona mtu anapinga tena kwa nguvu zote suala la Mgombea binafsi ujue ana maslahi na uwepo wa vyama kwenye ushindani!
  Mfano ccm kwakuwa wameshika dola wao wanaweza kukataa!
   
 10. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Nadhani dawa hasa ni mgombea binafsi. Tukiwapa kinga tunaweza kutengeza loophole ya watu kuvuruga VYAMA kwa sababu tu wana kinga ya ubunge. Miaka mitano inatosha kabisa kuvuruga kama sio kuua kabisa chama.
   
 11. N

  Nyadunga Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Huyu mdudu ....kuongea nje ya vikao imetoka wapi kwenye vyama vyetu vya siasa?!!!!.Mara oooh, kazungumza nje ya utaratibu......mara kuna vikao vya ndani....ina maaana wanachama hawana uhuru wa kutoa mawazo? Je mwenyekiti asipoitisha the so called vikao halali wanachama wasizungumze au wasitoe maoni? ama kweli vyama vinasumbuliwa nia mifumo iliyoasisiwa na CCM ya chama kushika dola..CHADEMA mjihadhari na masuala kama haya
   
Loading...