Elections 2010 Khanga, Tshirt za CCM zakwama bandarini

Viwanda vya hapa nchini wagumu sana kutoa 10% wewe unafikiri akina Makamba, Amos Makalla watakulaje?
Bora wawapelekee wa China huko sio wazito kutoa 10%

10% ata ndani ya chama chao wenyewe!!! ama kweli awa wamekubuhu kwa ufisadi. Nafikiri ata ndani ya familia zao bado wanakata 10%. Mama akiachiwa fungu la chakula anakata fungu lake, dogo nae akipewa pesa ya ada anakata 10% kwanza. Kweli ufisadi ukikuingia ni sawa na virusi havikuachiii.
 
vipo lakini ni very expensive kutengeneza khanga na vitenge ukilinganisha na singapore, china, cambodia etc. the main reason ni kwamba sisi hatuna umeme ulio robust [pesa zote ndo hizo wanakula na ndugu zao], pia kodi za malighafi ziko juu na generally we like buying from outside hata kama ni malawi...
icon_clap.gif
icon_lol.gif


wewe unadhani ulaji wa kampeni menejaz unatoka wapi? si ndo vitu kama hivyo?
Nani anayesababisha kupanda kwa gharama za uendeshaji nakwa kuchapisha nje ndiyo wamevisaidia viwanda kupunguza gharama. Viongozi wetu tukiri ni mbumbumbu wanafikiri viwanda vitajiendesha bila kupata tenda kama hizo. Basi tufunge shule na viwanda kama tunadhani vya nje ni cheap. Wanashindwa kuelewa ni cheap kwa leo lakini ni expensive kwa kesho.
 
Mkuu zimeishatolewa acha uongo
Kwenye issues kama hizi zinazohitaji data ni bora ukawa hutoi comments utaharibu hata hicho kidogo walichonacho CCM, wewe saizi yako ni kwenye umbeya unakufaa sana.
 
Akili za kichina, mawazo ya kichina, makalio ya kichina khanga, fulana na mabango ya Kichina. Ndio maana hawajui kwanini Tanzania ni nchi masikini licha ya kujaliwa rasilimali kibao.
 
Akili za kichina, mawazo ya kichina, makalio ya kichina khanga, fulana na mabango ya Kichina. Ndio maana hawajui kwanini Tanzania ni nchi masikini licha ya kujaliwa rasilimali kibao.

Nashawishika kusema CCM ni chama cha Kichina!
 
Khanga,vitenge,shati,kofia,vipeperushi vya chama tawala kutengenezwa kwa wingi kutoka nje,kisa kweda ikulu?Kuna biashara gani huko ikulu?Je kama mmepewa zawadi hizo fadhila mtazilipaje? Kama mnakubalika kwa wananchi yanini kutumia mapesa ya wananchi ovyo?Kutoka Uhuru mpaka leo hamtosheki kuwatawala watu?Mnaposema wapinzani wana uroho wa madaraka miaka yote toka uhuru nani ameshika mpini,si ninyi tu?Takwimu zinaonyesha nchi maskini kabisa duniani katika nchi mahututi 10 Tanzania ni mmoja wapo,mbona utawala wenu auleti afueni bali ugumu wa maisha?Katika nchi za jumuia ya afrika mashariki inayoongoza kutembeza bakuli la kuomba omba ni Tanzania hamuoni aibu?Lini mtapunguza kuchonga midomo na kufanya maendeleo dhabiti na kurudishia heshima nchi yetu?
 
marando alishindwa kukomboa mzigo kama huo toka afrika kusini those days


...haha..kina mrema enzi zile walishindwa kutoa baadhi ya mizigo tunduma kwa sababu ya kupandishiwa kodi......lakini kuacha zile kanga na fulana zilizokuwa na picha ya mrema...zile bendera,scar f na kanga zenye nembo....ndizo zinaendelea kutumiwa na NCCR hadi sasa ...it was a huge stock....


as of ccm ni aibu kununua kanga china wakati wanasema wanataka kujenga viwanda vya ndani......tuna viwanda vya kanga ..hapa urafii,nida,karibu,metl,...etc.....ingeleta maana sana kama wangeunga mkono viwanda vya ndani...ATZ NA sunflag wanazalisha mafulana.......ma print ya karatasi za matengenezo viwanda ni vingi tu hapa...sijui kwanini wamepeleka kazi nje......yet wanasema wanataka kuongeza ajira...
 
TRA kukataa ni danganya toto, huyo kitilya lazima atatetea ulaji wake, tuwe macho inaweza kuwa EPA No.2
 
Bado kuna mizigo yenu imebaki bandarini inadaiwa kodi.

Mzigo utakuwa umetoka siku nyingi wewe unafikiri Mkurugenzi TRA anaubavu wa kukatalia mali ya CCM kwasababu haijalipiwa kodi kwani unafikiri hataki kubaki kuendelea na wadhifa wake wa kuwa MKurugenzi MKuu TRA, hiyo kamwe hawezi hata iweje mzigo uko nje na wananchi wameshagawiwa siku nyingi tuu.

CCM ndio chama kinachoongoza Serikali na ndio wanamamlaka ya kufanya lolote bila mtu mwimgine kusema lolote unafahamu kuwa Kamati Kuu ya CCM ndio inayoongoza nchi sasa kaa ufahamu HILO
 
Hizi gharama zote za uchaguzi kwa CCM ni za nini wakati wanajulikana nchi nzima na ndio waliokuwa madarakanai miaka yote? Chama kinachotumia gharama kubwa namna hiyo ama kinakuwa hakijulikani kwa hiyo kinataka kujitangaza kijulikane au hakipendwi na watu hivyo kinataka kuwafurahisha wapiga kura ili wakipende. CCM iko wapi kati ya hayo mawili?
 
Back
Top Bottom