Khadija Kopa: Najutia sana kitendo cha kufanya abortion

Huyu mama pamoja na mambo mengine ni mkweli na anajua maana halisibya Toba tofauti na wengine wanaogugumia maumivu ya dhambi ndani

1. Kitendo alichokifanya kutubu hadharani dhambi kubwa kama hii ya mauaji ndicho hicho wakatoliki wanalalamikiwa na madhehebu na dini nyingine kuungama kwa binaadam mwenzake( Padre)

2. Huwezi kutubu moja kwa moja kwa Mungu usiyemuona ukasema dhambi imetoka. Kutubu lazima usikie aibu ya kile ulichokitenda, umweleze binadamu ambaye Mungu amemuumba kwa mfano wake na ukishatoa mzigo huo kifuani urudi Kwa Mungu na kuomba msamaha wa kutokurudia tena na Mungu atakusamehe

3. Kuna watu wana madhambi Makubwa , wanamfanya Mungu kama mjomba wao, wanamwomba kimawenge chumbani kesho wanarudia tena
Ni upumbavu kutangaza dhambi ulizofanya kwa kisingizio cha kutubu.

Hakuna mkamilifu hapa duniani jua hilo,hivyo kila uanayemuona ukidhani ni mtakatibu ndio inakuja dhana ya kwamba akikosea aseme hadharani.

Kama kila mtu ni mkosaji basi hakuna haja ya kuyatangaza mabaya yako,malizana kivyako na Mola wako
 
Kuna siku utaupata huo ukristu, endelea kuutamani kwa kufanya matendo ya huruma kwa maskini, heshimu kila binaadamu aliyeumbwa na Mungu epuka kinywa chako kutamka au mkono wako kuandika mambo machafu na mabaya dhidi ya mwenzako, hakika utamwona Yesu na utakuwa na nafasi yako mbinguni. Lakini mdomo wako ukitumika kuwasengenya wenzako na kuongea maneno mabaya hakika Mungu atakugeuzia kama sii wewe kizazi chako

Unamfunza mwenzio kuwa na lugha nzur hali ya kuwa comment ya juu umetoka kutoa lugha kali ? Hivi kweli vichekesho.
 
Hiki alichofanya kisheria inaitwa extra judicial confession, kimsingi anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria na akahukumiwa kwa ushahidi alioutoa dhidi yake mwenyewe tena bila kushurutishwa.

Mambo mengine yakifanyika jamii inaweza kuanza kumtetea bila kujua alichofanya kina impact kubwa sana kisheria especially sheria ya jinai dhidi ya utoaji mimba maana bado Sheria yetu inakataza kutoa mimba na kuna adhabu Kali sana.

Hawa wasanii ni vema wawe wanajiandaa kutoa hizi statement zao maana Zina impact kubwa kisheria na kijamii.
 
Huyo mama kwa mujibu wa imani yake bado hajajua maana ya toba.
Katika uislam mtu muovu mno ni yule anaefanya madhambi gizani(kwa kujificha) halafu akitoka hapo anaenda kuwasimulia watu.
Kwa mujibu wa uislam toba ni baina ya mja na mola wake.
Hii tabia ya kutubu kwa kuutangazia ulimwengu sio katika mila ya uislam.
Sahihi
 
Dah!...ila aliyetoa 'ameua' aliyebambika amelinda uhai japo 'ameongopa'.
Zote ni dhambi, na chanzo chake ni mimba zisizotarajiwa. Inaweza kuwa ajabu lakini ndivyo ilivyo, wanawake hawana utawala juu ya matumbo yao ya uzazi.
Hata wanawake matured above 40 wengi wanabeba mimba bila kutarajia licha ya uwepo wa njia za kuzuia mimba.

Sasa nini kifanyike kuepusha wanawake wasitumie abortions & paternity fraud kukabiliana na mimba isiyotarajiwa?
 
Huyu mama pamoja na mambo mengine ni mkweli na anajua maana halisibya Toba tofauti na wengine wanaogugumia maumivu ya dhambi ndani

1. Kitendo alichokifanya kutubu hadharani dhambi kubwa kama hii ya mauaji ndicho hicho wakatoliki wanalalamikiwa na madhehebu na dini nyingine kuungama kwa binaadam mwenzake( Padre)

2. Huwezi kutubu moja kwa moja kwa Mungu usiyemuona ukasema dhambi imetoka. Kutubu lazima usikie aibu ya kile ulichokitenda, umweleze binadamu ambaye Mungu amemuumba kwa mfano wake na ukishatoa mzigo huo kifuani urudi Kwa Mungu na kuomba msamaha wa kutokurudia tena na Mungu atakusamehe

3. Kuna watu wana madhambi Makubwa , wanamfanya Mungu kama mjomba wao, wanamwomba kimawenge chumbani kesho wanarudia tena
Umewapiga waprotestant kwenye mshono

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mama kwa mujibu wa imani yake bado hajajua maana ya toba.
Katika uislam mtu muovu mno ni yule anaefanya madhambi gizani(kwa kujificha) halafu akitoka hapo anaenda kuwasimulia watu.
Kwa mujibu wa uislam toba ni baina ya mja na mola wake.
Hii tabia ya kutubu kwa kuutangazia ulimwengu sio katika mila ya uislam.
Hizo mila ni za kipuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom