Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,245
Khadija Omar Abdallah Kopa (amezaliwa Zanzibar, 1963) ni mwimbaji wa muziki wa Taarab na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania. Mbali ya muziki, Kopa ni mama wa nyumbani, mfanyabiashara na pia mwanaharakati wa kisiasa nchini Tanzania.
Khadija Kopa
Jina la kuzaliwa: Khadija Omar Abdallah Kopa
Amezaliwa:1963
Kazi yake:Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, Mtayarishaji wa rekodi, mwanamuziki
Ala:Sauti
Miaka ya kazi:1990–hadi sasa
Ameshirikiana na Diamond Platnumz, Abdul Misambano, Ali Star, Mzee Yusuph, TOT
Anafahamika zaidi kwa ushirikiano wake mkubwa na bendi ya TOT. Ameanza kuimba Taarab tangu mwaka 1990 na bendi ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa Culture Musical Club.
Mtoto wake wa kike Zuhura Othman Soud, afahamikaye kwa jina la kisanii kama Zuchu ni mwimbaji pia. Alijiunga na Wasafi Classics na kutoa nyimbo maarufu kama vile: Nisamehe, Sukari, Yalaa, Cheche, Wana.
Hivi karibuni mwanamuziki huyu amejutia sana kitendo cha kufanya abortion na kutoa kauli kwa lengo la kuwaasa wanawake wenye tabia hiyo, Khadija Kopa anasema
Kutoa mimba ni ujinga sana, maana saizi ningekuwa na watoto wangu kama saba. Najuta kweli kweli, lakini unajua wakati ule ndio jina limesimama kweli kweli, sasa wakati huo nilee mimba wapi na wapi. Ila najuta pengine ukute mwanangu angekuwa Rais sasa. Namuomba Mungu anisamehe, najuta sana na vijana msifanye hilo. Mungu naomba anisamehe sitaki kulisikia tena jambo hilo"- Khadija Kopa