.Ndio! Mechi ya jana kati ya Taifa Stars na Ivory Coast imedhihirisha hilo!Hakika 70% ya Watanzania ni 'Bendera Fuata Upepo! Habari ndio Hiyo!
ndio! Mechi ya jana kati ya taifa stars na ivory coast imedhihirisha hilo!hakika 70% ya watanzania ni 'bendera fuata upepo! Habari ndio hiyo!
Ungekuwa uwanjani ungeelewa mkuu, kwa asilimia kubwa Watanzania hawana msimamo!
sawa...Ungekuwa uwanjani ungeelewa mkuu, kwa asilimia kubwa Watanzania hawana msimamo!
Tunapokubali na kuruhusu wezi/mafisadi wawe ndio wafadhili wa timu zetu tutegemee uzalendo upi? Nakubaliana nawe kuhusu kurudisha michezo shuleni na mashindano baina ya shule na shule. Michezo inajenga afya kwa watoto na ushindani pamoja na kujiamini.Uzalendo sifuri na hii haina uhusiano na hali ya maisha wala nini? Inabidi turudishe uzalendo kuanzia shuleni kwa kuwa na michezo mingi shuleni. Waziri aliyefuta michezo shuleni ndiyo wa kwanza kulaumiwa kwa kuondoa uzalendo wa vijana wetu. Sasa JK ameanza kuijenga kwa kurudisha michezo mashuleni. Itachukua muda kidogo.
Wakuu tulipofungwa uwanja wote ulikuwa kimya. Tulipocheza vizuri tulishangalia. Drogba alizomewa. Mara he Drogba na wenzake wakaanza kushangiliwa. Mwishoni kabisa ndio kidogo tukawashangilia vijana wetu. Yaani tulikuwa hatueleweki kabisa!
Mpwa una uhakika na unachokisema?? we uwanjani kwa mechi hile kunaweza kukawa na Ivory Cst wangapi mule? Ushabiki upi uwekwe mbele mpwaa, tulivyofungwa kimyaaaaaa kukipigwa chenga kushabilia mara upande huu mara upande ule!!!! kama kushabikia walipaswa waanze mwanzo mwisho hata kama tumefungwa, sie watanzania tunakasumba tukiwa tumefungwa mashabi ndio wakwanza kuwavunja nguvu wachezaji hata kama wanajitahidi.Una hakika gani waliokuwa wakishangilia walikuwa watanzania? Na kama sivyo, mimi nadhani wanastahili pogezi kwa kuweka ushabiki pembeni na kufurahia mchezo wenyewe.
Amandla.......
Una hakika gani waliokuwa wakishangilia walikuwa watanzania? Na kama sivyo, mimi nadhani wanastahili pogezi kwa kuweka ushabiki pembeni na kufurahia mchezo wenyewe.
Amandla.......