Kevin Hart alikuwa na ndoto yake kubwa tangu udogoni ya kuja kutangaza kwenye Tuzo kubwa za Oscar

Chilojnr

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
302
1,306
Kama unakumbuka ni mwaka 2019 tu hapo ambapo Kevin Hart alikuwa na ndoto yake kubwa tangu udogoni ya kuja kutangaza kwenye Tuzo kubwa za Oscar.
Wakati Tuzo zikiwa zimekaribia, bahati mbaya ama nzuri akaposti kitu kinachohusiana na mashoga, baada ya watu kuona amezingua kwa kuwaongelea vibaya, wakaamua kumchomoa, wakakatisha ndoto yake.

Tuje kwenye hii series sasa.

Kwanza nianze kwa kumpongeza mwandishi, Eric Newman kwa kuandika series kali na inayoangalizika, ambapo utakapoanza kuitazama tu, ninaamini utakwenda nayo mpaka mwisho.

Hii series imeandikwa kwa mtindo wa True Stry, maisha aliyopitia Kevin Hart kipindi alichokuwa akiishi huko Philadelphia kabla ya kutusua maishani mwake. Hapa nikwambie tu kwamba Kevin Hart na kaka yake, huwa haziivi kabisa kwenye makuzi yao, sasa kwenye hii series, wameamua kumuweka Wesley Snipes kama kaka yake Kevin aitwaye Carlton.

Series inaanza kwa mtindo wa flashback kwa scene ya kwanza halafu sasa inaanza moja kwa moja. Humu tunamuona Kevin aliyecheza kama kijana Kid akiwa supastaa kwa kufanya stand Up Comedy.

Amefanikiwa sana, ana pesa sasa alipoamua kwenda huko Philadelphia alipokulia, akaungana na kaka yake. Kiukweli humu Kid alionyesha kumpenda sana kaka yake ila tatizo kaka hapendeki, alipewa sana pesa lakini amejawa na madeni lukuki.

So siku moja Carlton anamwambia Kid waende klabu. Kid amebadilika, si yule aliyekuwa kipindi cha nyuma, hata pombe kwa kipindi hiki hanywi lakini alipojikuta ameshawishika kwa kwenda huko, akalazimishwa kunywa pombe, na baada ya kulewa, akaenda kulala na mwanamke.

Wakati anaamka asubuhi, mwanamke huyo amefariki dunia kitandani hivyo yeye na kaka yake wanaanza harakati za kuutoa mwili huo chumbani (Kumbuka hapo ni hotelini)

Ili kufanikiwa, kaka yake anamwambia kuna mwamba anaitwa Ari, huyo hashindwi kitu, kama kweli wanataka kuutoa huo mwili, basi mchizi boti aitwe na kufanya mambo, kweli anaitwa na kuutoa kirahisi kabisa, kwa maneno yake anasema aliivunjavunja mifupa ya maiti ya mwanamke huyo.

Kwenye malipo, Kid alimwambia angemlipa dola elfu hamsini, ila mwamba akataka kulipwa dola laki tano kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mzima, ambapo ukipiga mahesabu, jumla mchizi angemkamua kiasi cha dola milioni sita.

Ni pesa nyingi sana kwa kijana kama Kid. Ni kweli alikuwa akitengeneza pesa nyingi, ila kutoa pesa hizo, kwake lilionekana suala lisolowezekana, hivyo anaamua kumuua Ari humohumo hotelini.

Humu Kid ameonyesha maisha ya upande wa pili ya mtu maarufu. Unaweza kumuona anapata pesa nyingi lakini maisha yake yamejaa matatizo makubwa. Pia amewatumia ujumbe Wazungu kwenye masuala ya kibaguzi kama pale scene ya pili ndani ya ndege, jamaa ambaye alikuwa shabiki yake ambaye alitaka kumletea utani kwenye mambo ya ubaguzi, bahati nzuri naye baadaye akamuumbua sana.

Pia ameonyesha kuhusu sisi mashabiki wa wasatu maarufu, jinsi tunavyoweza kuwaletea matatizo ama hata kukubali kufanya jambo lolote lile wanalolitaka kisa tu tunawapenda, hatujali jamii itahathirika vipi, sisi tunafanya tu, hii imetokea kwa shabiki Gene ambaye alimpiga video Kid na kaka yake wakiutupa mwili wa mtu kwenye pipa la takataka lakini hakushtaki kwa kuwa alikuwa akimpenda sana Kid.

Kwa hii series nzima, Carlton alikuwa mtu mbaya, mtu ambaye anaweza kukufanyia mabaya mengi bila kujua, ukienda kuitazama utajua kwa nini nimesema hivi.

KASORO.

Ila kasoro kubwa nilioiona kwenye hii "True Story" ni vile inatulazimisha kuzikamata hali zote kihisia juu ya kijana Kid vile alivyoishia au alivyokuwa.

Mimi sidhani kama hii mini-series ina haki ya kukufundisha kwa lazima kujua hili au lile, maana ilitakiwa iache nafasi ya mtu kuamua ajisikiaje juu ya kijana maarufu aitwae Kid, lakini pia kama imeonekana ‘creators’ hawakuwa na maamuzi kuhusu character’s motivations, je unaweza kujiuliza huyu kijana Kid ni mtu mzuri aliekumbwa na situation mbaya? Inakupa mafikirisho kwamba pengine ni kijana mwenye ubinafsi na kujithamini yeye zaidi ndio mana alimjibu hovyo shabiki yake pale nje ya hospitali.

Hebu vuta picha kama "True Story" imeegemea kwenye hilo kiuhalisia! ambapo anawawakilisha watu mashuhuri ambao mifumo yao ya thamani imekandamizwa. Maana kuna wakati kama ilionekana kwenda "dark" na kuwa more interesting halafu tena inarudi kule kuliko sahihi kwaajili ya watazamaji.

Ikiwa inafanya hivyo kwa kuzuia maamuzi ya kweli ambayo binaadamu hufanya kama vile maamuzi binafsi (selfish decisions), ujeuri au fujo hasa kwa mtu mwenye uwezo wa kipesa kama alivyoonekana Kid.

Zaidi ya yote, hakuna tabia halisi ya kibinadamu ya kutosha tuliojengewa kuiona, hasa kwa kutupa ushawishi usiwezekana, mfano simu zilionekana zinatumika hazina password kama alivyoonekana Carlton na simu za watu.

Utakapoanza tu kuitazama episode ya kwanza, ni hapo hapo utakuwa "hooked", sababu kwanza imemuonesha Kevin ambae kaigiza more serious, emotional na ni nzuri for a change. Pia kulikuwa na twist nyingi kwenye hii mini-series, baadhi za kikatili ambazo unaweza usipende.

Series imewekwa kwenye "Moody dark theme" hapa ingependeza kama ingekuwa muvi, ila sio mbaya kwa kuwa series imekuwa short.

All in all ni moja ya "A must watch shows."

Credit: Nindi Jr and Nyemo.
IMG_20211204_124308_261.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom