Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,349
- 25,215
Tokea kesi ya Freeman Mbowe ya ugaidi iishe, na mara akaonekana Magogoni, sasa imekuwa ndio mpango mzima, wanasiasa hasa wa upinzani kufunguliwa kesi kama ile.
Tumeona wapinzani kadhaa wakifunguliwa kesi za ugaidi na uhaini na hii trend inashika kasi.
Kwenye kesi ya FAM ilichukua muda sana, na kuna watu walipata ukwasi kweli kweli kupitia ile, kesi...
Sasa tunaona kesi ya Tundu Lissu inaelekea ukingoni na imechukua muda kweli,kweli..akina Kagiraffe wamepiga kiasi gani, na wenzake...haya sasa John Pombe Magufuli naye kafunguliwa kesi kama ya Tundu Lissu, mbona ni kama mtaji unatafutwa hapa kwamba kuna mdau hajamaliza kulipa mafundi...
Huko gerezani wapo wenye same case!
Ikumbukwe enzi za John Pombe Magufuli kesi za uhujumu uchumi zilikuwa hazikauki, na watu walifanya Plea bargaining, watu wakatengeneza ukwasi! Je hivi sasa uhujumu uchumi au watu waliokuwa na tabia za kuhujumu uchumi kama enzi za John Pombe Magufuli hawapo hivi sasa?
Kwa nini kwa sasa hatusikii kesi za moto moto za uhujumu uchumi na Plea bargaining zikifanyika kama enzi za John Pombe Magufuli, badala yake ni ugaidi na uhaini...! So tukubali uhujumu uchumi kwa sasa ni bye bye, na wahaini pamoja na magaidi wameshika kwa kasi kwa sasa hapa nchi ya Kusaidika!