Kesi za ardhi sasa kuharakishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi za ardhi sasa kuharakishwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Mar 25, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Kesi za ardhi sasa kuharakishwa Send to a friend Thursday, 24 March 2011 21:19

  Kesi za ardhiJames Magai
  MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi imeandaa mkakati maalumu wa kukabiliana na tatizo la mrundikano wa kesi za ardhi ili ziishe haraka.Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Lameck Mlacha, alisema kwa kesi za ardhi zinagusa uchumi wa nchi na kwa hiyo zinapaswa kumalizika mapema.

  "Chini ya mkakati huu jumla ya majaji tisa na mahakimu wakazi wakuu saba wenye mamlaka ya ziada watahusishwa," alisema Mlacha.Alisema mkakati huo utaendeshwa kwa kipindi cha wiki sita na kwamba katika kipindi hicho jumla ya mashauri 484 ya ardhi yatasikilizwa na kuamuliwa.

  Alisema maeneo yatakayohusika ni yale yenye migogoro mingi.Aliitaja mikoa itakayohusika katika mkakati huo kuwa ni Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Moshi, Arusha, Mwanza, Tabora, Dodoma na Mbeya.

  Naibu Msajili huyo alisema hadi kufikia Februari mwaka huu, kitendo kilikuwa na jumla ya kesi 5922 huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuwa jumla ya kesi 2200 ukifuatiwa na Mwanza wenye kesi 787.

  Aliongeza Mkoa wa Arusha unashika nafasi ya tatu kwa kuwa kesi 712 huku mkoa wa Ruvuma ukiwa mwisho kwa kuwa na kesi 79 tu.

  Mlacha alifafanua kuwa kesi zitakazohusika katika mkakati huo ni kesi za rufaa kwa mikoani, lakini kwa Dar es Salaam mkakati huo utahusika na baadhi ya kesi zisizo za rufaa ambazo zimechambuliwa kwa umakini.


  "Katika mkakati huu tumepanga kesi tatu kwa siku na tunalenga kuwa kesi itasikilizwa na kumalizwa siku hiyo hiyo.Hukumu zitasomwa siku ya Ijumaa ya kila juma au siku nyingine yoyote ndani ya kipindi cha mkakati," alisema Mlacha.

  Alitoa wito kwa wananchi wenye kesi za rufaa kwenye kanda zilizotajwa waende kuangalia orodha ya mashauri ili kujua kama kesi zao ziko katika mpango huo.Mlacha alisema majaji na mahakimu walioteuliwa watahama kutoka katika vituo vyao vya kazi na kwenda kwenye maeneo ya migogoro.

  Majaji walioteuliwa katika mpango huo na vituo vyao katika mabano ni Ibrahimu Mipawa, Haruna Songora (Dar es Salaam), Zainabu Mruke (Tanga), Kipenka Mussa (Moshi), Alice Chinguwile (Mwanza) Chocha (Arusha), Aghatoni Nchumbi (Tabora), Grace Mwakipesile (Dodoma na Pellagia Khaday (Mbeya).Mahakimu ni Dyansobera (Tanga), R. Rutatinisibwa (Moshi), E. Shaidi (Arusha), Lameck Mlacha (Mwanza), D. Mrango (Dodoma), Bernard Mwingwa (Tabora) na P.Lyimo (Mbeya).Mwisho.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kuwa kesi nyingi haziamuliwi kulingana na sheria bali matakwa binafsi ya wato haki.........na hivyo kusababisha rufani kurundikana za kupinga maamuzi ambayo yaliyokithiri kwa dhuluma...................
   
 3. Hiphop

  Hiphop Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli kuwa "Justice delayed is justice denied" lakini pia tuliangalie hili jambo la kuharakisha usikilizwaji wa kesi hizi na tukumbuke kuwa "Justice hurried is Justice burried"
   
 4. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,740
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hapa naona kuna uchemshaji wa hali ya juu sana.Hii taarifa imekuja ndani ya muda mfupi.Sidhani kama inawezekana ndani ya muda mfupi kila mtu,hasa wale ambao hawana mawakili wakapata taarifa hizi.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  bora wafanye jambo juu ya kesi mana urasimu mwingi sana
   
 6. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
   
 7. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
   
Loading...