Kesi ya wizi wa kilo 5 za dhahabu.....shahidi amwaga radhi............ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya wizi wa kilo 5 za dhahabu.....shahidi amwaga radhi............

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Feb 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Shahidi aeleza mahakama watuhumiwa Kabla ya mauaji walidai dhahabu kilo 5 Friday, 04 February 2011 21:31

  James Magai
  SHAHIDI wa kwanza kesi ya maiti iliyokutwa ndani ya begi, Halfan Abdallah, ameileza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa, kabla ya mauaji wauaji waliomba dhahabu kilo tano au dola 100,000 za Marekani, ili wasitekeleze mauaji hayo.

  Katika kesi hiyo, mfanyabiashara mkazi wa Dar es Salaam, mwenye asili ya Kiasia, Vonoth Nadhesan, anatuhumiwa kumuua Abdul Abdallah kwa kumchoma na vitu vyenye ncha kali.

  Shahidi huyo ambaye ni mdogo wa marehemu, alitoa maelezo hayo wakati akitoa ushahidi wake juzi kesi hiyo ilipoanza kunguruma. Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Dk Fauz Twaib.

  Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Shadra Kimaro, akisaidiana na Cecily Mkonongo, shahidi huyo alidai kuwa, Februari 6, 2009 alimpigia simu kaka yake kujua mahali alikokuwa baada ya kupata wasiwasi kutokana na kuchelewa kurudi.

  Alida kuwa alipopiga simu ya kaka yake, ilikatwa na baadaye akapokea ujumbe mfupi wa maneno ukimweleza kuwa, atapigiwa simu baadaye kidogo.

  Aliendelea kudai kuwa, hakupigiwa simu na ilipofika saa 7:00 usiku alipiga simu tena, lakini ilikatika tena na kupokea ujumbe mfupi wa maneno ukieleza kuwa betri ya simu iko chini.

  Baada ya ujumbve huo, shahidi huyo alidai kuwa, muda mfupi baadaye alipokea tena ujumbe huo wa maneno ukimjulisha kuwa kaka yake ametekwa kwa sababu ya kudhulumu na kwamba, ili waweze kumwachia atoe dhahabu kilo tano au dola 100,000za Marekani.

  Shahidi huyo alidai kuwa, baada ya kupokea ujumbe huo alikwenda kutopa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi, kisha polisi walianza kumtafuta marehemu na watekaji hao hadi maiti yake ilipopatikana ikiwa ndani ya beki kwenye gari.

  Mshtakiwa huyo anatuhumiwa kufanya mauaji hayo Februari 7, 2009. Anadaiwa kuwa baada ya mauaji hayo aliweka mwili ndani ya begi kisha kwenda kuutelekeza ndani ya gari ndogo Jengo la Habour View Tower (JM Mall), jijini Dar es Salaam.

  Alikamatwa na polisi Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akijiandaa kwenda India.

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  When evil rules our lives death and destruction are the final outcomes..........................
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  The world is a dangerous place to live; not because of the people who are evil, but because of the people who don't do anything about it.
   
Loading...