Kesi ya wananchi dhidi ya Serikali kuhusiana na suala ya bandari kuanza kusikilizwa Jumatatu 3th Julai 2023 Mahakama Kuu Mbeya

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Katika kesi hiyo wakili Msomi Boniface Mwabukusi A.K.A Mayweather, Wakili msomi Mwakilima na mawakili wengine wanawawakilisha Alphonce Lusako, wakili Chengula na Nyarusi ambao ndio walalamikaji kwa niaba ya watanzania kwenye kesi hiyo.

Kwamba kesi hiyo imefunguliwa kwa hati ya dharura na kwamba itasikilizwa na kuamuriwa na mahakama kwa muda usiozidi siku 30. Kesi hiyo itasikilizwa mbele ya majaji watatu ambao ni mhe. Jaji Ndunguru, Mhe. Jaji Ismail na Mhe. Jaji Kagomba.

Washtakiwa kwenye kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi, Waziri wa Ujenzi Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire na Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi.

Washtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini Makataba wa kimataifa na kuupeleka bungeni kwa ajili ya kupitishwa bila kushirikisha umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa wananchi kutoa maoni yao, kinyume na sheria ya rasilimali za taifa no.5 ya mwaka 2017 kifungu cha 11 (1) na (2).

Sheria inataka mikataba inayohusu Mali asili ya nchi kabla ya lolote kufanyika ni wajibu na lazima kwa Waziri husika kuhakikisha serikali inaweka wazi Mkataba na Makubaliano yote kwa umma kupitia Vyombo vya habari vinavyofikika na wengi. Mfano wa vyombo hivyo ni Magazeti, Radio za kitaifa, Radio za jamii,Televisheni na njia za kidigitali, Mikataba na Majina ya wamilika wawanahisa wa Kampuni husika kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (1),(a),(b) na (c) cha sheria ya Tanzania Extractive Industries (Transparency
and Accountability) Act no 23 of 2015. Kwa bahati mbaya waziri hakufanya hivyo. Aliuficha mkataba huo tangu October 2022 mpaka ulipofichuliwa majuzi kupelekwa bungeni.

2. Washtakiwa no.1 na no.4 wanashtakiwa kwa kuwaongoza wabunge vibaya kwa kupiga kura za ndiyo badala ya kura ya Mbunge mmoja mmoja kama sheria inavyotaka (Natural Wealth and Resource Contract Act) no.6 ya mwaka 2017 kifungu cha 5 na 6. Sheria inataka
Jambo lolote ambalo linagusa Maliasili na raslimali za nchi linahitaji uthibitisho wa Bunge Kuridhia kwa kupiga kura ya mmoja mmoja na lazima jambo hilo lipitishwe na 2/3 ya wabunge wote kwa kuwa ni suala la Muungano kwa mujibu wa Katiba. Lakini katibu wa bunge kwa makusudi ama sababu anazozijua yeye aliwaongoza wabunge tofauti na matakwa ya sheria.

Mshtakiwa no.1 na no.4 wanashtakiwa kwa kushindwa kuliongoza bunge vizuri kufanya kazi yake ya kushauri serikali na kusimamia maslahi ya umma kwenye mikataba ya kimataifa kinyume na ibara ya 63(2) na (3) ya Katiba ya nchi. Kwamba kuwa suala la mkataba wa IGA kati ya Tanzania na Dubai ilikuwa ni jambo kubwa na muhimu, basi ilipaswa bunge kupewa muda wa kutosha ili kuwajibika kuuchambua na kutoa mapendekezo ya kuboresha kabla ya kuupitisha. Lakini washtakiwa hawakutoa muda wa kutosha kwa bunge kufanya kazi yake na kupelekea wabunge wengi kukosa muda wa kuchangia na kutoa mapendekezo yao kwa kile kinachodaiwa kwamba muda hautoshi.

4. Mshtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai wenye vipengele vinavyovunja Katiba (ibara ya 28(3) pamoja na Sheria za Ardhi namba 4 na Namba 5za Mwaka 1999 za Tanzania hususani kuhusu haki za Wageni auMakampuni ya uwekezaji yanayomilikiwa na wageni Katika Umiliki wa
Ardhi.

5. Washtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba wa "hovyo" unaozigawa rasilimali zetu za kimkakati kwa mamlaka ya nje ya nchi, kinyume na Katiba ibara ya 1, 8 na 28.

6. Kwamba Mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai una vipengele vinavyoweka rehani enzi kuu ya taifa letu (National sovereignty) na kuuza uhuru wetu, kinyume na ibara ya 1, 8 na 28 ya Katiba.

7. Kwamba Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai haukufuata sheria ya manunuzi ya umma no.64 ya mwaka 2011 na hivyo Mkataba huo kuwa batili tangu mwanzo (null & void ab-initio) Kwamba hakuna maelezo yoyote ya serikali yanayohusu ni namna gani kampuni ya DP World ilipata tenda hiyo kama sheria za nchi zinavyotaka.

Kutokana na mapungufu hayo ya kisheria mawakili wa wananchi wakiongozwa na Wakili Mwabukusi wanaiomba Mahakama imuamuru mara moja Waziri mwenye dhamana kuurejesha Mkataba ule Bungeni ukiwa na MoU, IGA na Mchanganuo wa Mradi ili Bunge na wananchi wapate haki yao ya Kikatiba ya Kutoa maoni ipasavyo.

Lengo ni :

(a) kuwezesha na Kutoa Muda wa Kutosha wa Bunge Kuujadili na kuufanyia Marekebisho.

(b) Kutoa Muda wa Kutosha kwa wadau na Wananchi kuuelewa, kuujadili na kutoa Maoni yao kuhusu mambo yanayojumuishwa katika mkataba huo wa IGA.

(c) Kuboresha Makubaliano ya IGA na kuweka bayana

i.- Ukomo na mawanda ya Mradi na utekelezwaji wa shughuli zote
zilizokubaliwa katika mradi husika

ii.- Kuweka kifungu cha kuongoza uvunjaji wa Mkataba.

iii. - Kuondoa Vifungu vinavyoashiria umilele.

iv.- Kuondoa Vifungu vyote ambavyo moja kwa moja au kwa matokeo yake vinaondoa Haki ya nchi ya umiliki wa raslimali (Sovereignty), haki ya nchi kufanya ushindani na fursa ya nchi kuruhusu wawekezaji wengine katika eneo la uwekezaji wa bandari.

v. - Kuhakikisha Uzingatiwaji wa Sheria Zingine za Nchi na kuhakikisha kwamba Mkataba huu hauwi juu ya Katiba ya nchi, sheria za Ardhi na sheria zinazolinda raslimali asili za nchi.

Mwisho ni kwamba kesi hii ni ya wananchi. Hivyo basi wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyenu, imani zenu au jinsia zetu mnapaswa kufika mahakama kuu kanda ya Mheya siku ya jumatatu ijayo tarehe 3th July 2023 kusikiliza shauri hili.

๐Œ๐๐ฎ๐๐ž ๐๐ฒ๐š๐ ๐š๐ฅ๐ข ๐Ÿ• ๐ฑ ๐Ÿ•๐ŸŽ ๐’๐ฎ๐ฆ๐ฎ ๐ฒ๐š ๐๐ฒ๐ข๐ ๐ฎ


IMG-20230628-WA0000.jpg
20230627_090904.jpg
 
Ktk vitu JPM na Kabudi waliupiga mwingi ni hio Sheria ya National Wealth ya 2017...otherwise hili jambo ht bungeni lisingepita, lingegongwa kimya kimya km TICTS, inaishia kwenye baraza la mawaziri juu kwa juu...Sheria ila layers za kupitia kabla hujapitisha jambo and on top of that inakasimisha mamlaka kwa raisi, so anything that can go wrong raisi wala bunge hawawezi kujitoa ktk lawama...
wangeongeza kipengele cha kifungo km ikitokea faulo ingekua poa zaidi, watu wangeogopa kufanya maamuzi ya hovyo.
 
Katika kesi hiyo wakili Msomi Boniface Mwabukusi A.K.A Mayweather, Wakili msomi Mwakilima na mawakili wengine wanawawakilisha Alphonce Lusako, wakili Chengula na Nyarusi ambao ndio walalamikaji kwa niaba ya watanzania kwenye kesi hiyo.
Mwisho ni kwamba kesi hii ni ya wananchi. Hivyo basi wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyenu, imani zenu au jinsia zetu mnapaswa kufika mahakama kuu kanda ya Mheya siku ya jumatatu ijayo tarehe 3th July 2023 kusikiliza shauri hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba kesi hiyo imefunguliwa kwa hati ya dharura na kwamba itasikilizwa na kuamuriwa na mahakama kwa muda usiozidi siku 30.

Shukrani umeandika kwa kina kuhusu mwenendo mzima wa kesi utakavyoenda na muda wake.

Tunaomba kesi hii ipate coverage ya kutosha na ya kina kikubwa kama ilivyokuwa ile kesi mbaya ikiyotikisa nchi na dunia iliyomkabili mwenyekiti wetu Freeman Mbowe na wenzie 3 tukapata elimu kubwa kuhusu nchi yetu na mifumo yake ya jinai haki Tanzania .

Kesi hii inaendana sawa na jukumu la kumpa uwezo na kumwezesha kila raia afahamu ibara za katiba kuhusu jukumu la kulinda nchi yetu ili wote kwa pamoja siku za mbeleni wasitokee tena watu watakaothubutu kutuuza kiujumla jumla bila wengi kufahamu kuwa tumepigwa mnada.
1687939457556.png
 
Naona sakata la DP World limekuwa blessings in disguise kwani linakwenda kutuunganisha Watanganyika na pia kuleta awareness kubwa kwa mustakabali wa Taifa letu. Hapa ndiyo kila mtu anaona hasara ya Katiba inayompa Rais mamlaka makubwa sawa na Mungumtu na pia hasara ya kuwa na bunge la chama kimoja kwani wakikaa kama kamati ya chama wanauvua utaifa na kuvaa uchama ili kubariki madhambi ya viongozi wao kwa tishio la kuvuliwa uanachama kama wakipinga maovu ya watawala ambao ni mabosi wao kwenye chama.
 
Back
Top Bottom