Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
Katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mh Mbowe na wenzake watatu,leo Shahidi upande wa utetezi Ndg Lembrus Mchome mkaazi wa Wilaya ya Mwanga kaithibitishia Mahakama kwamba D/C Msemwa alikuwa akihudumu kituo cha police Oysterbay na si Central Police kama alivyodai wakati akitoa ushahidi wake kwamba alimpokea mshitakiwa Mohammed Ling’wenya.
Ndg Lembrus alikuwa akikabiliwa na kesi ya makosa ya mtandao.Pamoja na kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo pia aliweza kuwasilisha nyaraka mbali mbali zenye kuunga mkono madai yake.
Kupitia ushahidi huu ambao mawakili wa Serekali hawakuutarajia kabisa ni wazi sasa madai ya washitakiwa Adamo na Ling’wenya kwamba hawakuwahi kufikishwa Central police hata mara moja badala yake walipelekwa Vituo vya Police TAZARA na Mbweni yatakuwa yamepata nguvu kubwa kweli kweli.