KESI YA UCHOCHEZI: Tundu Lissu apandishwa kizimbani, apata dhamana, kesi yaahirishwa hadi Agosti 2

Yafaa viongozi wa Chadema watoe hesabu ya malipo ya mawakili kwa kila kesi. Inaelekea Viongozi wa Chadema wanafanya hila kula ruzuku kwa njia ya kujitafutia kesi za kisiasa. Wananchi wanashangaa kwa kiwango cha cdm kuichokoza mamlaka iliyoko madarakani. Mamlaka iliyoyochaguliwa na wananchi inakejeliwa kwa kushikwa ndevu ili wawekwe jela na kujidai wapigania uhuru. Nia yao hasa ni kupiga hela ya chama chao na kuiyumbisha serikali inayoyowajibika vilivyo kwa maslahi ya wananchi.
Naona unahangaika kutafuta cha kusema. Bk 2 utapata tu.
 
Lisu atashinda na huenda kesi ikafutiliwa mbali...
Sure,jamaa atashinda kesi serikali itaishia kulipa kesi na gharama zote,na usumbufu!hapo kwy usmbufu hao mawakili 17 ndio watakopotokea apo
 
IMG-20160630-WA0014-620x308.jpg

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki amesema, ‘namtaka dikteta uchwara mahakamani,’anaandika Faki Sosi.

Lissu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema hayo leo muda mfupi baada ya kutoka kusikiliza shauri lake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam la kudaiwa kutoa kauli ya uchochezi.

“Mimi na jopo langu la mawakili tunamtaka niliyemuita diktekta uchwara aje mahakamani kuthibitisha udikitekta uchwara wake,” amesema Lissu.

Lissu amefunguliwa shitaka la uchochezi katika mahakama hiyo, kesi yake inasikilizwa na Hakimu Yohona Yongolo ambapo kwa upande wa mashitaka, unawakilishwa na Benard Kongolo, wakili wa serikali mkuu.

Lissu alijisalimisha jana 5 asubuhi katika kituo hicho cha polisi ambapo alizuiliwa kupewa dhama na kulala hadi alipofikishwa mahakamani leo.

Wafuasi na viongozi mbalimbali wa Chadema walifika mahakamani hapo akiwemo Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho taifa; Salum Mwalim, Kaimu Katibu Mkuu Zanzibar na Benson Kigaila, Mkuu wa Operesheni wa chama hicho.

Wakili Kongolo amedai kuwa, Lissu alitenda kosa hilo tarehe 28 Juni mwaka huu katika eneo la Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kuzungumza;

“Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidiktekta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikitekta uchwara lazima apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

Hata hivyo, Lissu amekana shitaka hilo, amedhaminiwa na wadhamini wawili waliosaini hati ya Sh.2 milioni kila mmoja na masharti ya kutosafiri nje ya nchi na kwamba, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. Kesi hiyo itatajwa kwa kusikilizwa tarehe 2 Agosti mwaka huu.

Upande wa utetezi kuliwakilishwa na mawakli 11 miongoni mwao ni Michael Ngolo, Peter Kibatala, John Mallya, Hekima Mwasibu, Omari Msemo, Jeremia Mutasebya na Juma Nasoro.
 
Huyu dikteta si ndio alitoa ile kauli uchaguzi wa meya ufanyike chama chochote kikishinda kipewe ushindi!
 
Tundu Lissu ni shujaa na ni nembo halisi ya ukombozi .
Msishabikie mambo mengine yasiyo na maana. Angalia Tundu Lissu katoa hayo maneno ya kumsema vibaya rais, kwa kuwa ni mwanasheria na ana wanasheria wenzake watatumia udhaifu wa hiyo sheria kutafuta justification ya maneno mabaya aliyoyatamka. Kiuhalisia amekosea sasa unafikiri nini kinachohitajika kudhibiti watu kama hao. Ni huo udikteta anaousema
 
Msishabikie mambo mengine yasiyo na maana. Angalia Tundu Lissu katoa hayo maneno ya kumsema vibaya rais, kwa kuwa ni mwanasheria na ana wanasheria wenzake watatumia udhaifu wa hiyo sheria kutafuta justification ya maneno mabaya aliyoyatamka. Kiuhalisia amekosea sasa unafikiri nini kinachohitajika kudhibiti watu kama hao. Ni huo udikteta anaousema
Si kila unayemsoma humu anashabikia , sisi wengine ni wawezeshaji kamili , kwanza sikuona sababu ya polisi kumkamata Lissu kwa hoja ile , wangeacha hili jambo lingepotea lenyewe tu , lakini sasa limekuwa kubwa na wananchi wamelikubali kuliko kawaida ! Kumkamata mtu kama Lissu kwa lengo la kumtishia nyau au kumnyamazisha ni sawa na kupoteza muda tu .
 
Back
Top Bottom