KESI YA UCHOCHEZI: Tundu Lissu apandishwa kizimbani, apata dhamana, kesi yaahirishwa hadi Agosti 2

View attachment 361467 View attachment 361468 Mh Tundu Lissu a pandishwa kizimbani Muda huu mahakama ya kisutu kwa zile tuhuma za maneno ya kuudhi, nunachokisubiri hapa ni maneno mengine yenye tafsiri nyingine kwa watu wengine atakayoitoa leo baada ya kupata dhamana panapo majaliwa. Ndio kwanza kumekucha mapambano yataendelea.

UPDATES:

Lissu anatetewa na wanasheria 17 wakiongozwa na John Mallya Peter Kibatala na timu nyingine toka makao makao makuu ya Chama.

Viongozi wote wa makao makuu wameshawasili,

Tunasubiri Hakimu tu aingie kwenye ukumbi wa mahakama...

UPDATES,

Tayari Hakimu anayesikiliza shauri ameshawasili, sasa ni utambulisho wa mawakili wa pande zote,

Kesi inaanza kusomwa,

Mwendesha mashitaka: Tundu Lisu anashitakiwa kwa makosa ya uchochezi, mnamo tarehe 28/06/2016 akiwa eneo la mahakama kwania ya kudhalau umma dhidi ya mamlaka yao walioyoichagua kihalali, alisema huyu dikteta uchwara lazima tumpinge kila kona"

Hakimu: Mshitakiwa, unakubali au unakataa?

Lissu: nakataa yote

Mwendesha mashitaka: Mh Hakimu ushahidi wa shauri hili umekamilika, tunaomba tarehe ya kuanza usikilizwa,

Hakimu: Mawakili wa utete mnalololote la kusema?

Wakili: Mheshimiwa kwamjibu wa kifungu cha sheria na.... Mshitakiwa kosa aliloshitakiwa linadhaminika, hapa tunao wadhamini na zaidi mshitakiwa ni mbunge na mwanasheria wa chama, hivyo anadhaminika, na zaidi mshitakiwa aliliripoti mwenyewe mbele ya polisi baada ya kuitwa tu kwa simu. Ni hayo tu mh

Mwendesha mashitaka: Mshitakiwa aliyembele yako, mnamo tarehe 28 mwenzi huuhuu alifikishwa mahakamani kwa kosa...... Aaah nimesahau sina nakala ya mashitaka, na wenzake watatu na kudhaminiwa. Hivyo akatenda kosa hili, huyu ana nidhamu mbovu, ameona kutenda kosa ni kawaida,

Hakimu: Kwanini unamhukumu kwa kosa ambalo mahakama hii haikumtia hatiani...na siajabu akitoka hapa atatenda kosa tena....

Wakili: Mh hakimu nashindwa kujua huyu wakili wa serikali anajipa kazi ya hukumu kwa kesi iliyopo mahakamani, nimshauri arudi kwenye kesi iliyopo mezani kwakuwa kesi ya nyuma ni tuhuma tu na sio hukumu inayoweza kutumika kama kielekezo hapa.

Mwanasheria: Mh huyu mtuhumiwa ni mzoefu wa kutenda makosa...... Watu wanaangua kicheko kwa kwa kwa...

Hakimu..... Wakili

Wakili: Kwanza Mh hakimu naomba ifahamike kwamba upande wa serikali wamekubali kuwa suala la dhamani liko wazi, hili liweke katika kumbukumbu... Haya anayoyaleta sasa huyu mwanasheria hayana msingi, kwani kwa mjibu wa vifungu vya sheria na.....na... Vinampa haki yakupata dhamana, izingatiwe kuwa katika dhamana ya kesi ya mwanzo hakukuwa na mashariti ya mtuhumiwa kutotoa maoni ama kutenda kosa nje ya lile.. Izingatiwe kuwa sababu za kukidhi dhamana tumeshazitoa

Hakimu: Mahakama inaamua kuwa mtuhumiwa apewe dhamana, wadhamini wa mtyhumiwa waje mbele...kuhakiki nyaraka zao

Mwanasheria: Anainuka... Mh Hakimu...

Hakimu anasema Jamhuri haijajenga hoja za kutosha kuzuia dhamana.Kwahiyo hakuna Pingamizi la Dhamana

Anawaita Wadhamini

Wamejitokeza Mbunge Susan Lyimo, Madiwani Humphrey Sambo na Rose Moshi Kwa ajili ya kudhamini

Amepewa dhamana.Asanteni
Yafaa viongozi wa Chadema watoe hesabu ya malipo ya mawakili kwa kila kesi. Inaelekea Viongozi wa Chadema wanafanya hila kula ruzuku kwa njia ya kujitafutia kesi za kisiasa. Wananchi wanashangaa kwa kiwango cha cdm kuichokoza mamlaka iliyoko madarakani. Mamlaka iliyoyochaguliwa na wananchi inakejeliwa kwa kushikwa ndevu ili wawekwe jela na kujidai wapigania uhuru. Nia yao hasa ni kupiga hela ya chama chao na kuiyumbisha serikali inayoyowajibika vilivyo kwa maslahi ya wananchi.
 
Yafaa viongozi wa Chadema watoe hesabu ya malipo ya mawakili kwa kila kesi. Inaelekea Viongozi wa Chadema wanafanya hila kula ruzuku kwa njia ya kujitafutia kesi za kisiasa. Wananchi wanashangaa kwa kiwango cha cdm kuichokoza mamlaka iliyoko madarakani. Mamlaka iliyoyochaguliwa na wananchi inakejeliwa kwa kushikwa ndevu ili wawekwe jela na kujidai wapigania uhuru. Nia yao hasa ni kupiga hela ya chama chao na kuiyumbisha serikali inayoyowajibika vilivyo kwa maslahi ya wananchi.
Ndio mwisho wako wa uwezo wa kufikiri huu? Au ndio akili yenu kwa mawakili wa serikali kubambika watu kesi ili mtafune public fund?
 
Nakumbuka kwenye makala Fulani hivi ya Edo kumwembe kuna mahali alisema.

" Huwezi kuwa shujaa bila kuwa mhuni"

Huyu jamaa ana uhuni wa sheria hawatamuweza wataambuliwa kumweka selo tu ila sio kumfunga labda aue
 
Serikali haiwezi kushinda.

Kufungua kesi ilikuwa mistake. Angeachwa aseme tu.

Tundu Lissu akipatikana na hatia/ kufungwa jela, atapandishwa chati. Serikali ya Magufuli itajidhihirisha kwamba ni ya kidikteta.

Akionekana hana hatia, atakuwa kaweka precedent ya wengine kuweza kupata uhuru wa kusema ukweli.
Na ndo itakavyokuwa tatizo anao pambana nao hawana fikiri ya mbeleni
 
Back
Top Bottom