Kesi ya Radio 5 na waliokuwa wafanyakazi wake kuunguruma tarehe 11 Juni, 2021

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
MAHAKAMA Kuu masijala Ndogo ya kazi Kanda ya Arusha kesho June 11 inatarajia kusikiliza kesi ya msingi ya maombi ya wafanyakazi wapatao saba kuomba mahakama hiyo kukamata mali za kituo Cha Tan Communication Media inayo miliki kituo cha utangazaji cha Radio Five kilichopo Njori jijini Arusha.

Kesi hiyo inakuja mahakamani hapo mara baada ya kuarishwa mwezi April kwa upande wa wadaiwa kutokuhudhuria mahakamani na kushindwa kutoa taarifa.

Hakimu mkazi, Itikila Theofilo Nguvava, alilazimika kuahirisha kesi hiyo ambayo ilikuja kwa ajili ya kusikiliza pingamizi lililowekwa na upande wa wadaiwa hadi Juni 11 siku ya kesho mwaka huu.

Wafanyakazi Saba wa radio hiyo wakiongozwa na Jofrey Stephen walifungua kesi namb 151 ya mwaka 2020, wakikidai kituo hicho cha utangazaji cha Radio five

zaidi ya sh, milioni 31.9 baada ya kuachishwa kazi kinyume na utaratibu.

Wafanyakazi hao walifungua kesi mahakamani hapo baada kutoridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama ya usuluhishi (CMA) baada ya kumpa ushindi mdaiwa.

Upande wa walalamikaji wanaongozwa na wakili Heri Makando waliiomba mahakama hiyo itoe idhini ya kukamatwa Mali za mdaiwa ambaye ni Tan Communication na kupigwa mnada ili kufidia malipo ya wafanyakazi hao.

Wafanyakazi hao waliomba mahakama hiyo itoe amri ya kukamatwa kwa Mali za mdaiwa,ambazo ni pamoja na Jengo la kituo hicho cha utangazaji cha Radio five, lililopo Njiro plot namb 153 n.a. 154 block J, Jenereta, vifaa vya studio pamoja na vifaa vya kufanyia matangazo.

Upande wa mdaiwa,ambao uliwakilishwa na wakili, Andrew Maganga aliwasilisha notisi mahakama kuu ya rufaa kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Johannes Masara, June 16, 2020 iliyowapa ushindi wadai jambo ambalo mpaka sasa imeshindwa kutimizwa rufaa.

Hivyo kupangiwa muda jambo ambalo walalamikaji wameona mahakama iwapae nafasi ya kusikiliza shauri lao la msingi la kuuza vifaa hivyo kufikia madai yao kwani muda unazidi kwenda na rufaa ya mdaiwa ikiwa imeshindwa kupewa tarehe rasmi ya kusikilizwa.
 
Back
Top Bottom