Kesi ya Mbowe: Thamani ya ushahidi wa shahidi #4 ni ipi?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,763
35,731
Anita Valerian Mtaro shahidi #4 mkristo mwuuza pombe za kienyeji, alitimba mahakamani incognito ndani ya vazi la kiislam akiwa pia katupia barakoa lenye kumwachia macho ya kuweza kuona peke yake.

Shahidi huyu wa upande wa mashtaka amesikika akisema alishuhudia zoezi zima la kukamatwa kwa washitakiwa #2 na #3.

Kwamba alishuhudia yote yaliyojiri hadi kujitolea kutoa maelezo yake kwa niaba ya upande wa mashtaka central polisi Moshi.

Hata hivyo shahidi haelezi kwanini polisi walimpenda zaidi yeye, ikizingatiwa washtakiwa hawakukamatiwa kwake na wala yeye hakuwa karibu zaidi na eneo la tukio kuliko wengine wote waliokuwapo.

Shahidi huyu muuza mbege, alianza kwa kueleza aliona watu watatu wakinywa bia, wakiongea na simu, na kusajili line za simu. Shahidi huyo akadai tena kuona watu 2 waliokuwa wakipita pita kwenda na kurudi, huku wakiongea na simu.

Vipi haya yote kutokea muda huo huo?

Shahidi anadai zoezi zima la ukamataji lilianza saa 7 mchana likachukua takribani dakika 45 kisha safari ya kwenda central ikaanza. Akaandikisha maelezo kisha akaya saini saa 7 kamili mchana.

Zaidi sana shahidi anadai washitakiwa kwenye kukaguliwa walikuwa na bastola (A5340), kete za madawa ya kulevya na Simu zao tu.

Hawakuwa na pesa, hata 1/-.

Maajabu zaidi ya Mussa ya shahidi huyu ni kuwa ana sahihi tofauti tofauti akiwa kasimama na akiwa amekaa. Pia baina ya za kukaa nazo ni tofauti kama ambavyo za baina ya kusimama zilivyo tofauti.

Bila shaka ndiyo sababu upande wa mashtaka hawakutaka kabisa shahidi aanguke pale kizimbani 😁😁.

Shahidi ni mpangaji RAU madukani. Kumbe:

IMG_20211101_185600_293.jpg


Chama cha Mapinduzi - CCM.

CCM hoyeee!
 
Nilichoelewa Mimi watuhumiwa hao walikamatwa hapo wakiwa na bastola na hizo kete.
huyo ndo aliona.
 
Shahidi wa leo anaishi hatua kumi kutoka eneo la tukio, lakini wapo wanaouza duka la vipodozi waliokuwa karibu zaidi na eneo la tukio walipokamatwa watuhumiwa lakini polisi hawakuhangaika nao, walienda kumchukua huyu wa mbali ambaye ni mpangaji na kada mwenzao ili wamlishe upupu bila shida.
 
Lengo la ushahidi wake ni kuonesha kwamba ukamataji wa watuhumiwa ulifuata taratibu, na pia maelezo ya polisi ni ya kweli.
Wewe kwa akili zako hayo maelezo ya polisi yana ukweli gani kama waliwakamata watuhumiwa saa saba wakamfanyia mahojiano kwa 45mins it means walimaliza naye saa 13:45 kisha maelezo hayo hayo akayasaini saa saba kamili.....inakuingia akilini?

Hapo hizo hesabu zao waligawanya walizidisha au walitoa?may be walijumlisha who knows!
 
Shahidi wa leo anaishi hatua kumi kutoka eneo la tukio, lakini wapo wanaouza duka la vipodozi waliokuwa karibu zaidi na eneo la tukio walipokamatwa watuhumiwa lakini polisi hawakuhangaika nao, walienda kumchukua huyu wa mbali ambaye ni mpangaji na kada mwenzao ili wamlishe upupu bila shida.
Shahidi anatakiwa kuwa 'willing to volunteer' kuwa shahidi kwa upande wa ulalamikaji au mlalamikiwa

Huwezi kuchukua shahidi yeyote ambaye huna uhakika anaweza kubadilika katikati ya kesi na kutoa maelezo yanayousaidia upande mwingine (hostile witness) ndio maana polisi walitathimini kwanza ni yupi afaaye kutoa ushahidi bila kuyumbishwa kwa hongo au vitisho.
 
Shahidi ana matatizo ya kuona karibu anaweza kuona mbali tu. Rangi za gari kazijua ila T-shirt hajajua rangi yake.
Ndio maana kitabibu ni kweli baadhi ya watu wana uwezo wa kuona mbali au karibu kwa hiyo hakuna tatizo katika maelezo yake ya ushahidi.

Wakili ameshindwa kuhoji kama ana matatizo ya kuona na kwamba alishathibishwa hospitalini ili adai cheti cha kupimwa kwake. Mawakili wanaojifunza wanafikiri kila kinachofundishwa darasani ndicho kilichoko kwenye uhalisia ndio maana pakawepo na shule ya sheria (Law School) kumwandaa na uwanja wa hoja tunduizi
 
Back
Top Bottom