Kesi ya Mbowe na wanasheria wa Tigo na Airtel ikumbushe wenye mamlaka kutunza siri za wateja ni muhimu kujenga sekta imara ya benki na mawasiliano

Jamani si tulikuwa tunataka kujua ukweli. Sasa ukweli unaanza kuwekwa wazi tumeanza kupiga kelele kuwa faragha za watu zimeingiliwa. Tutukuze nini ukweli au faragha za watu?
 
Hii sheria ina udhaifu mkubwa sana, haipaswi kuwa ni police officer au law enforcement officer bali inapaswa kuwa ni mahakama.
Yaani wakimpata mtu dhaifu na loyal kwao kama Fred wa Tigo wanajipatia taarifa za siri za mteja kwa urahisi sana!
Yaani Bora hata JF kuliko mitandao ya simu kwenye ulinzi wa taarifa za wateja!!
 
Mfano Kuna watu wanaka kukuua mleta mada wanawasiliana na simu kupanga wakuulie wapi unataka kampuni ya simu wasiripoti polisi kuhusu Hilo ili kunusuru maisha yako? Na wahusika wadakwe?

Ulinzi na Usalama wa watumiaji wa simu na wananchi ni wa kila mtu zikiwemo kampuni za simu

Jirani yako ukiona majambazi yamemvamia huhitaji kibali chake kuripoti polisi
 
Hivi hakuna watendaji wa hivyo vyombo ulivyotaja wanaotumia vibaya madaraka yao?
Utawatambua kwa kuwaona??
Kama wapo au hawapo ni nani atasimama katikati kama refa kulinda maslahi na haki za kila upande??
Je, ni nani atafanya maamuzi kuwa muamala fulani ni batili mwingine ni halali??
Trust no one!
 
Hii ni wakeup call, kuwa usitumie mitandao ya simu kama siyo lazima sana. Labda utumie zaidi data ili mawasiliano yawe kwa whatsap, skype au telegram, huduma ambazo savers hazipo nchini, lakini siyo sms wala calls, au kutuma hela
Sir,
Even these are susceptible to hacking !

Server kuwa mbali hakuzuii wadukuzi kufuatilia kila kitu
 
Nimeshangaa sana kuona mwanasheria wa kampuni ya simu anaweza kuwa hovyo namna hii huwezi kutoa maelezo kama layman flani, Kingai amemugiza cha kike aisee
 
Hacking ni uhalifu na makampuni yote yanayotumia mitandao yanajilinda kwa mifumo mbalimbali, ucha kurudia rudia huu utopolo wako.
Sir,
Even these are susceptible to hacking !

Server kuwa mbali hakuzuii wadukuzi kufuatilia kila kitu
 
Hadi benki hakuna mtu wa katikati kama refa ambayo inapaswa kuwa mahakama kulinda haki za wateja! Tumechelewa sana.
 
Kwa hiyo polisi waombe idhini kwa mhalifu ili wamchunguze?
 
Kwahiyo Tigo wanaweza kuvujisha siri kwa mkewangu zile text nachat na mchepuko!!


KichWa bOX
 
Kwa haya yanayozungumzwa na Wakili msomi wa TIGO ni dhahiri kabisa hawa ndio wanavujisha siri ya pesa zilizopo kwenye akaunti za watu kwa matapeli na wezi wa mtandaoni.
 
Naendelea kuwashangaa usioona udhaifu wa maelezo ya Wakili wa Tigo Alfred Kapala. Tatizo si kutoa taarifa Polisi, tatizo kubwa ni maelezo yake kuwa;
1.Siri za wateja wao si kipaumbele chao.
2.Taarifa inaweza kutolewa kwa yeyote akitaka hata mtu binafsi isipokuwa kama anahtaji taarifa ya mtu mwingine. Yaani Leo wewe ukijifanya ni Mimi na ukawa na vielelezo ni Mimi unapata taarifa zangu. Hili ni kweli kabisa wala hajadanganya. Ndo maana Tigo na Voda zimetumiwa sana na wezi (Ile hela tuma kwenye Namba hii) kuibia wateja. Mtu anapiga simu huduma kwa wateja Tigo kwa Namba nyingine anaomba Namba yake nyingine (ya mtu mwingine) isitishwe kwa muda simu ina tatizo na wao bila kujiridhisha wanaistisha na wezi wanatumia muda huo kuihamisha kwenda line nyingine na kuitumia kuibia marafiki na ndugu wa mteja wa awali. Huyu MWIZI anajifanya ni wewe una shida ya laki 5 umekamatwa au unaumwa kumbe Tigo wamemsaidia MWIZI kusajili line ya ndugu yako.
3.Kwa maelezo yake hata Polisi wasipofuata matakwa ya sheria kuomba taarifa za wateja, Tigo itawapa tu. Ndo maana kipindi Fulani kiongozi mmoja akamwambia Mkuu wa wilaya wa kike Nina taarifa zako zote maana mawasiliano yako hata ya usiku wa manane ninayo.
NB; Bado unaona wako sahihi?
 
Hii ishu kama nilisikia kipindi, nadhani ilikuwa America
 
Mfano wako mbona ni tofauti... Umeongezea facts mpya...!
Kutaka kuua. Majambazi...
Je, kwenye namba ya Mbowe na transactions zake umesikia kokote kuwa alitaka kufanya hayo??
 
Hapana sio sahihu hata kidogo
Nilikuwa sijaelewa kabisa kitu kilichokuwa kinazungumziwa
Baadae ndo nikapata kujua yametokea kwenye kesi ya Mh Mbowe
Nimeelewa kwa nini wamezungumzia mtandaoni sasa
 
Huu upumbavu wako ulirithi au umeutafuta mwenyewe?
 
imenishangaza sana hiyo ,kwamba ofisa wa polisi anaweza tu kuamua kuomba taarifa zako tigo na akazipata kirahisi tu!!!! looh!!!
 
Hadi benki hakuna mtu wa katikati kama refa ambayo inapaswa kuwa mahakama kulinda haki za wateja! Tumechelewa sana.
TRA wanajikwapulia tu fedha kiulaini...
Maduka ya fedha (Bureau de changes) yaliibiwa hivi hivi tena kwa ushiriki wa JWTZ...
Alafu mtu bado haoni mantiki ya unachokisema!
Ujinga tu!
Shame!
 
Kwa haya yanayozungumzwa na Wakili msomi wa TIGO ni dhahiri kabisa hawa ndio wanavujisha siri ya pesa zilizopo kwenye akaunti za watu kwa matapeli na wezi wa mtandaoni.
Hilo liko wazi sasa na ndo maana Kibatala akatoa mfano wa kesi ya hela alizoibiwa mteja na wao Tigo wameshitakiwa japokuwa Wakili Msomi fake wa Tigo anajifanya hajui kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…