Kesi ya Mange Kimambi kuendelea leo Januari 28, Kisutu

Kesi ya Mange Kimambi kuendelea leo Januari 28, Kisutu

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
604
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwanaharakati Mange Kimambi inatarajiwa kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Soma pia PostGE2025 - Serikali ya Tanzania yamfungulia Mange Kimambi kesi ya Uhujumu Uchumi. Adaiwa kutakatisha Tsh. Milioni 138

Mange, anayeishi Marekani, ameshitakiwa kwa utakatishaji fedha TZS milioni 138.5, ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 1 na Machi 31, 2022 Dar es Salaam; kufanya uandishi wa habari bila kibali, pamoja na kudai fedha kupitia vitisho.
 
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwanaharakati Mange Kimambi inatarajiwa kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Soma: Kesi ya Mange Kimambi ya utakatishaji wa fedha kuunguruma leo Desemba 4, Kisutu

Mange, anayeishi Marekani, ameshitakiwa kwa utakatishaji fedha TZS milioni 138.5, ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 1 na Machi 31, 2022 Dar es Salaam; kufanya uandishi wa habari bila kibali, pamoja na kudai fedha kupitia vitisho.

1769584006378.png
Kesi hiyo, chimbuko lake ni mashitaka ya mwaka 2022, imezua maswali kuhusu ni kwa nini imefufuliwa wakati huu.

Shauri hilo la jinai namba 000021172/2025, lililofunguliwa na Jamhuri Agosti 28, 2025, linadai kuwa kati ya Machi 1 na Machi 31, 2022, katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Mange alijipatia Sh138.5 milioni akifahamu kuwa ni fedha za uhalifu.

Inadaiwa pia alipata fedha hizo kupitia kazi ya uandishi wa habari bila kibali na kwa vitisho. Mashitaka hayo yanatokana na kifungu 12(1) (d) na 13(a) cha Sheria ya Utakatishaji Fedha, Sura ya 423 ya mwaka 2019, kwa mujibu wa Sheria ya Uhujumu Uchumi

Desemba 4, 2025, shauri hilo liliitwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Hassan Makube. Upande wa Jamhuri uliiomba mahakama kuahirisha kesi kwa maelezo kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Kwa upande wa utetezi, Mange hakuwa na wakili, hivyo Hakimu Makube aliutaka upande wa Jamhuri kuhakikisha taratibu zote zimekamilika ili kesi ianze kusikilizwa katika tarehe itakayopangwa.
 
Ahadi ya mwanasheria mkuu. Mawakili wa serikali wanakazi sana.

Kuna jamaa angu aliamua kuacha na hizo kazi serikali yupo zake kitaa.

Anasema kuna mambo mnaletewa ukihoji inaanza kuwa shida kwako. Kumbe wewe unataka upate facts.
 
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwanaharakati Mange Kimambi inatarajiwa kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Soma pia PostGE2025 - Serikali ya Tanzania yamfungulia Mange Kimambi kesi ya Uhujumu Uchumi. Adaiwa kutakatisha Tsh. Milioni 138

Mange, anayeishi Marekani, ameshitakiwa kwa utakatishaji fedha TZS milioni 138.5, ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 1 na Machi 31, 2022 Dar es Salaam; kufanya uandishi wa habari bila kibali, pamoja na kudai fedha kupitia vitisho.
Dah! My country Tanganyika!! Why all these shits??? Mshitakiwa yuko US lakini ulinzi umeimarishwa Dar!!! Kwahiyo hayo magari ya maji ya kuwasha na polisi wenye siraha za kivita pale Morocco leo ni kwasababu ya hii kesi????
 
Upumbavu kama huu ndio wanaweza kuchukua hatua nani anaefuatilia hiyo kesi au mwenye haja au shida ya kukamata mange kimambi hapa tanzania,huku si ni kukosa kazi aisee?😂😂😂😂

Kuna vitu vinachekesha na kutia hasira at the same time yaani ni full utoto. Hii ni kama mtoto kabinuka sarakasi kaangukia sufuria la mchuzi kalimwaga lote ukimuangalia unashindwa kumchapa at the sametime unajikuta unacheka unashindwa tu.
 
Aliyemteua johari amtimue kabla hajaharibu zaidi. Huyu johari kamuingiza mkenge wa kuuza bandari na huu upuuzi wa kumshtaki Mange. Hana hata aibu kujiita mwanasheria!
 
Back
Top Bottom