Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,743
- 2,601
DODOMA. Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma itatoa uamuzi wa mapingamizi yaliyowekwa na CCM dhidi ya Mchungaji Godfrey Malisa anayepinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho.
Mchungaji Malisa aliyefukuzwa uanachama Februari 10 mwaka huu, alipinga mchakato wa uteuzi wa Rais Samia uliofanyika Januari 19 na Mkutano Mkuu wa chama hicho, akisema umevunja Katiba ya CCM na Katiba ya Jamahuri ya Muungano.
Soma pia: Kesi ya Dk Malisa dhidi ya CCM yasogezwa hadi Agosti 19
Awali Agosti 6, Mchungaji Malisa aliwasilisha malalamiko yake katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, ambapo kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu, Jaji Joachim Tiganga, Jaji Evaristo Lungopa na Jaji Griffin Mwakapeje na CCM ilipewa siku saba kujibu malalamiko hayo.
Kesi hiyo ilitarajiwa wajibu Agosti 14. Hata hivyo, kesi hiyo ilisogezwa hadi leo Agosti 19.
Taarifa kutoka mahakamani hapo zinasema, mawakili wa CCM Fabian Donates na Alex Mgongolwa wamekuja na mapingamizi wakisema hatua za kufungua shauri hilo hazikufuatwa kabla, wakati na baada na kwamba ndani ya CCM kuna hatua za kufuata kabla ya kwenda mahakamani.
Akijibu mapingamizi hayo, wakili wa mlalamikaji, Denis Maringo amesema kanuni zilifuatwa, kwani Februari mwaka huu, Mchungaji Malisa alimwandikia barua Rais Samia akimlalamikia kuhusu uteuzi wake.
Hata hivyo, mawakili wa CCM wamepinga wakisema, mlalamikaji alipaswa aandike barua kwa katibu wa ngazi husika na kwa kuwa anamlalamikia mwenyekiti wa chama, alipaswa kumwandikia Katibu Mkuu.
Baada ya maelezo ya pande mbili, ndipo kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 22, 2025.
Akizungumzia kesi hiyo kwa simu leo, Mchungaji Malisa amesema kwa upande wao wameieleza mahakama kuwa wasingeweza kupeleka mashitaka kwa Katibu mkuu wa chama kwa kuwa yeye ndiye wanayemlalamikia na pia CCM wamevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
"Mawakili wa CCM wanasema hatukufuata utaratibu, tumewaambia kwamba mimi nilikutana na Katibu Mkuu, Dk Emmanuel Nchimbi tumeongea kwa saa mbili na ushahidi upo na picha zipo, taratibu gani nyingine?" amehoji.
Alichosema Mchungaji Malisa:
Mchungaji Malisa