Kesi ya madai dhidi ya Askofu Kakobe wa FGBF

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Kakobe , wadai wake watishiana kulipuana mahakamani Send to a friend
Sunday, 07 August 2011 21:51


James Magai
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe pamoja na wanaomshtaki kwa ubadhirifu wa mali za kanisa hilo, wametishiana kulipuana mahakamani wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa rasmi.Walalamikaji katika kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011, Dezedelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma wanaodai kuwa ni wachungaji wa kanisa hilo, wamemfungulia Kakobe kesi hiyo wakimtuhumu kwa matumizi mabaya ya fedha za kanisa hilo yanayokadiriwa kufikia Sh14 bilioni.

Wakati Kakobe akidai kuwa kesi hiyo ni mpango maalumu wa kumchafua na kwamba anasubiri aitwe mahakamani ili kulipua njama hizo kila mtu ajue, walalamikaji nao wamedai kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo kuna uchafu mwingi unaofanywa na Kakobe utafichuka.

Askofu Kakobe alikaririwa na Mwananchi akisema kuwa amefurahi sana kwa hatua ya wachungaji hao kumfungulia kesi akidai kuwa hiyo ni fursa nzuri ya kuweka wazi kila kitu ili kila mtu ajue ukweli .

Alisema ana vielelezo mbalimbali zikiwapo sauti zilizorekodiwa ambazo zinaonyesha kile alichokieleza kuwa ni umafia unaofanywa na watu hao dhidi yake na kwamba atakapoitwa mahakamani kwa ajili ya kujitetea kwa tuhuma hizo ataweka wazi CD hiyo na kile kilichomo.

Wakati Kakobe akidai kuwapo kwa njama hizo za kutaka kumchafua, walalamikaji wamepuuza madai hayo na kuonya kuwa kesi itatikisa kwa kuwa itaibua mambo makubwa na ambayo yatawagusa hata viongozi wengine wa kidini na hata taasisi nyingine za Serikali.

Juma lililopita Jaji wa Mahakama Kuu Dar es Salaam Agustine Shangwa aliwashauri walalamikaji ,wakatafakari upya juu ya madai yao kuona kama yana msingi na wanapaswa kuendelea nayo, huku akiwatahadharisha kuwa iwapo watashindwa wanaweza kumlipa Kakobe fidia kubwa.

Jaji Shangwa alisema kwa mfumo wa FGBF, Kakobe ndio Kanisa na kusema kwamba mapato ya kanisa hilo ni mali ya Kakobe kwa kuwa Kanisa hilo alilianzisha mwenyewe na kuhoji iweje wamhoji mtu anayetumia mali yake.

“Kwani ni nani alimpa Kakobe uaskofu? Kakobe alijifanya mwenyewe, ni tofauti na maaskofu wa Katoliki ambao mpaka waende wakasomee. Hizi fedha hapewi na Serikali ni za wale anaowatibu na wanaokuja kuombewa mapepo na kutoka katika mikutano anayoiandaa katika nchi mbalimbali. Kwa hiyo anakusanya fedha hizo kwa huduma, sasa mtamuulizaje na chake?;

Hata hivyo Jaji Shangwa alisema kuwa siyo kwamba ndio anatoa hukumu bali alikuwa akijaribu kutafuta suluhu kwa lengo la kupunguza mrundikano wa mashauri mahakamani huku akiwasisitiza kuyatafakari upya.

Lakini akizungumza na Mwananchi jana, mmoja wa walalamikaji hao, Dezedelius Patrick alisema msimamo wao ni kwamba wataendelea na kesi hiyo kwa kuwa ndio njia pekee ya kupata suluhu baada ya Kakobe kukataa kufanya nao suluhu kwa njia za kiroho.

“Sisi nia yetu si kumfikisha kiongozi huyo mahakamani, lakini tulimwomba kukutana naye na tukawatumia maaskofu maarufu nchini ili tuweze kufanya usuluhisho, lakini alikataa kabisa, hivyo tukaona hakuna njia nyingine isipokuwa kwenda kwenye sheria,” alisema.

Kuhusu madai ya Kakobe ya CD Patrick ambaye ni mlalamikaji wa kwanza katika kesi hiyo alisema kuwa hayana msingi kwa kuwa kinachosikika katika CD hiyo ni tofauti kabisa na madai yao yaliyoko mahakamani.

“Suala hili watu wanapaswa walitazame kwa mtizamo mpana kabisa kwani ni kubwa na litaibua mambo mengi na makubwa maana litazigusa hata na taasisi za serikali kama Rita ( wakala wa Serikali wa Usajiri wa Vizazi na Vifo na Ufilisi) na hata Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,” alisema.

Aliongeza kuwa hata Kakobe mwenyewe analijua kuwa kesi hiyo itaibua mambo makubwa na kwamba ndio maana sasa anatapatapa kwa kuhusisha na watu wengine kuwa kuna njama na kwamba ni la kisiasa.

Mlalamikaji huyo alisisitiza kuwa Kakobe anaihusisha kesi hiyo na mgogoro wa mradi wa upitishaji wa nyaya za umeme wenye msongo katika eneo la kanisa hilo kuonyesha kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja naye anahusika ili kupotosha ukweli.
 
wadai waache kujibizana na kakobe ila wamkatae jaji Shangwa kwa kuwa na maoni yenye kumpendelea Kakobe......................haiwezekani kanisa lililoandikishwa hapa nchini liwe miliki ya mtu binafsi kama jaji tajwa alivyooni hata kabla hajaipitia katiba ya kanisa hilo ambayo ndiyo msingi tanzu wa hii kesi ya madai..............
 
Jaji ametaja point. ila bado waumini ndio washika hayo mapato kama zaka na sadaka sio kakobe wakawadai hao waumini.. anyway patamu hapo.
 
this is another nonesense...kumfikisha kakobe courtini ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, kwasababu hela zile zote hajazila, amezitumia kwenye kazi ya bwana.....so shut-up your bit mouth, mwacheni jamaa aendelee kupiga injili...
 
Vipi Kanisa lake lipo chini ya baraza la wadhamini, kama ilivyo kwa Makanisa ya Roman Catholic, Anglican, na Kilutheri. Mali zote zipo chini ya Trustee of Diocese. Napata taabu kujua kama Askofu Kakobe kanisa lake lina wadhamini.
 
Kakobe ni "Mashine" kubwa,hao Waganga Njaa wanapoteza muda tu,hakika watashindwa!!
Giza halina Uzoefu wa Kuishinda Nuru!!!
 
Back
Top Bottom