Kesi ya Lissu | Shahidi wa Siri (P6): Lissu alisema tunakwenda kuvuruga uchaguzi na kukinukisha

Kesi ya Lissu | Shahidi wa Siri (P6): Lissu alisema tunakwenda kuvuruga uchaguzi na kukinukisha

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, ljumaa Februari 13, 2026 inatarajiwa kuendelea na Kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu katika kesi ya uhaini inayomkabili Kesi Yenye Na. 19605/2025 inayosikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru inayosikilizwa kwa mfululizo kuanzia Februari 09 hadi Machi 6, 2026.

Soma Pia:

1770984380997.jpeg


Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu tayari amefikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam msafara ulombeba ukiwa na magari 6 ya Jeshi la Polisi pamoja na Magereza.

Soma > Kesi ya Lissu | Shahidi wa siri (P5): Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha, uchaguzi mkuu hautafanyika

Wakati akishushwa kupita mlango wa nyuma wa gari aina ya Land cruiser Hardtop askari 16 walikuwa eneo hilo ambalo ni karibu kabisa na mlango mkuu wa kuingia mahakamani.


Lissu, tayari ameingia ndani ya chumba cha Mahakama Kuu kuendelea na usikilizwaji wa kesi inayomkabili.

Katika hatua ya leo, Lissu anatarajiwa kupata fursa ya kumuuliza maswali ya dodoso shahidi mwingine wa upande wa mashtaka anayefahamika kwa jina la P6, ikiwa ni mwendelezo wa ushahidi katika kesi hiyo.

Hapo jana siku ya Alhamisi kesi hiyo iliahirishwa baada ya Lissu kuiambia mahakama kuwa hajala jambo lililoibua hofu na hasira miongoni mwa wafuasi wake baadhi waliangua kilio baada ya kusikia kauli hiyo.

Aidha shahidi wa kwanza alisema kwamba 'aliona video ya Lissu akisema atakinukisha na uchaguzi mkuu hautafanyika'.Akimjibu Lissu alisema Nukisha inatokana na neno nuka na kwamba inaweza kuwa harufu nzuri au harufu mbaya'


Jana tuliishia sehemu ya 167, na leo tunaendelea na sehemu ya 168 ambapo kesi inaendelea Mahakamani muda huu;

Mahakama imeanza muda huu saa tatu na nusu.

Lissu anaingia akiwa amevaa kombati nyeusi.

Sauti ya High Courttt inapigwa kila mtu anasimama na kelele za kumsalimia Mwenyekiti zinasimama kidogo.

Majaji wanaandika kidogo pale mbele.

Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Ignas, Cathbert na Winiwa na wote tunawakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.

Sisi tuko tayari kuendelea na leo tumekuja na P6 yuko tayari, endapo Mshitakiwa atakuwa tayari.

Lissu anaulizwa na yeye anasema yuko tayari.
Jaji Ndunguru: Naomba shahidi aje sasa.

Mlango wa kizimba umefunguliwa muda huu.
Shahidi anaulizwa umri wake anasema miaka 24 na ni Mkristo so anaapishwa muda huu.

Jaji anauliza nani atamuongoza? Anajibiwa ni Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ndio atamuongoza.

Anamuuliza unanisikia.

Haya mkazi wa wapi?

Mimi natokea Ruvuma Songea na kazi yangu ni Afisa Usafirishaji Bodaboda, nafanyia huko huko Songea shughuli zangu.

Mwezi Oktoba 2024 ni mwaka ambao nilianza kushirikisha siasa za Chama cha Chadema.

Wakili: Ulishiriki kivipi?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kushiriki kwenye mikutano ya hadhara na kuwafuatilia viongozi mbalimbali wa Chadema na nikafanikiwa kuwafahamu, Lissu na baadhi ya Viongozi waliokuwepo Songea.
Wakili: wakiwepo akina nani?
Shahidi wa kificho P6: Nilimfahamu Katibu wa Vijana Songea.
Wakili: Alikuwa anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P6: Alikuwa anaitwa Chiza au Mwamba wa Kigoma maarufu kwa jina hilo.
Wakili: Januari 2025 unakumbuka nini?
Shahidi wa kificho P6: Nilianza kuwa nimeshiriki siasa za Chadema na kuvutiwa kuwa mwanachama wa Chama hicho.

Nikaanza jitihada za kutafuta viongozi waliopo Songea, nikamfuata kiongozi wa Vijana Chiza na kumueleza nia yangu ya kutaka kuwa mwanaChama.
Wakili: Nini kiliendelea baada ya hapo?
Shahidi wa kificho P6: Alinipokea na kunisifia kwa uamuzi mzuri. Akasema napaswa kuwa na kadi ya Chama, nilifuatilia hiyo kadi na nikaambiwa nisubiri mashine bado ni mbovu na ataendelea kunishirikisha kwenye shughuli za Chama.
Wakili: Zipi hizo shughuli za Chama?
Shahidi wa kificho P6: Sisi bodaboda huwa tunakuwa kwenye misafara ya Chama na bendera.
Wakili: Tarehe 04/04/2025 kilitokea nini?
Shahidi wa kificho P6: Hiyo tarehe nikiwa sehemu yangu ya kazi pia nikiwa na simu yangu ya mkononi aina ya infinix smart 8 nikiwa naangalia mtandao wa Youtube.
Wakili: YouTube ni nini?
Shahidi wa kificho P6: Ni mtandao wa kijamii ambao unamuwezesha mtu kutuma video, audio na maudhui mengine.

Anaendelea kuwa simu yake ilikuwa na internet na aliingia google kumuwezesha kuingia YouTube.
Shahidi wa kificho P6: Niliingia kwenye account ya Jambo TV nilifanikiwa kuona na kusikiliza hotuba aliyokuwa anatoa Mwenyekiti wa Chama cha Chadema ambapo alionekana akihutubia watu akisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi hivyo tunaenda kukinukisha.

Tunakwenda kuvuruga Uchaguzi pia nilisikia na kuona akisema tunakwenda kukinukisha na yeyote atakayekuwa pamoja nasi tutakwenda nae na ambae hatataka tutamuacha pia alisema kama kuna mtu yeyote anatarajia kugombea asahau jambo hilo.
Wakili: Pia akasemaje?
Shahidi wa kificho P6: Pia hata mimi kugombea uenyekiti msahau pia akasema bila mabadiliko hakuna Uchaguzi.
Wakili: Kingine kipi?
Shahidi wa kificho P6: Pia akasema watasema tunafanya uasi ni kweli utakuwa ni uasi kwasababu bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Sehemu ya 169

Mazingira aliyokuwa anayatolea ilikuwa ni kama sehemu ya Ukumbini, ndo nilimuona hapo.

Muda huu ameingia Mtaalamu, Wakili Msomi Peter Kibatala wakati kesi inaendelea.

Wakili wa Serikali: Muonekano wa Lissu ulikuwaje?
Shahidi wa kificho P6: Alivaa Kombati ya Kaki.
Namfahamu Tundu Lissu kama mwanasiasa mkongwe na mwanasiasa maarufu.
Wakili wa Serikali: Baada ya kuona hiyo hotuba wewe ulifanya nini?
Shahidi wa kificho P6: Nilivyoona hiyo video maneno yake yaliniingia moyoni na kunishawishi.
Hiyo agenda ya kukinukisha ni kufanya vurugu au kuharibu miundombinu.
Wakili wa Serikali: Huo uchaguzi ni upi?
Ukisikiliza majibu ya huyu Shahidi wa kificho ni wazi kaingia na desa anasoma majibu.
Anajibu hapa ni Uchaguzi Mkuu wa 2025 unaohusisha wabunge na Rais na Madiwani.
Wakili wa Serikali: Ikawaje baada ya kushawishika?
Shahidi wa kificho P6: Nikamfuata Mwenyekiti wa Vijana wa Songea alikuwa anaitwa Chiza maarufu kama Mwamba wa Kigoma.
Wakili wa Serikali: Ikaendelea nini?
Shahidi wa kificho P6: Nikamueleza nilivyoshawishika na maneno ya Mwenyekiti na kutaka kuwa miongoni mwa watu tutakaokinukisha.
Wakili wa Serikali: Kikaendelea nini?
Shahidi wa kificho P6: Alinisifia sana kwa uamuzi mzuri na wakishujaa na akanipongeza na kuniambia Vijana kama nyie ndio vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.
Wakili wa Serikali: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Aliniambia ataniunganisha kwenye magroup yanayojadili mipango ya kuzuia Uchaguzi, akaniunga Group la SIASA YETU.
Group lilikuwa linaitwa SIASA YETU UPDATES.
Wakili wa Serikali: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Niliendelea na shughuli zangu na yeye akaendelea.
Tarehe 06/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti wa Chadema atakuwa ziarani mkoani Ruvuma.
Wakili wa Serikali: Mwenyekiti ni nani?
Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Tundu Lissu, hiyo taarifa nilipata kutoka kwa ndugu Chiza.
Wakili wa Serikali: Ikakutaka ufanye nini?
Shahidi wa kificho P6: Ilitutaka tufanye maandalizi na tarehe 10/04 atakuwepo Songea.
Wakili wa Serikali: Mlipanga nini kuhusu mkutano?
Shahidi wa kificho P6: Tulipanga mkutano ufanyike uwanja wa matalawe. Tarehe 09/04/2025 nilipata taarifa kuwa Mwenyekiti amekamatwa Wilaya ya Mbinga akiwa kwenye ziara ya Mikuta.
Shahidi wa kificho P6: Nilimtafuta Chiza kumuuliza kuhusu taarifa za Mwenyekiti kukamatwa Wilaya ya Mbinga.
Wakili wa Serikali: ikawaje?
Shahidi wa kificho P6: Akanijibu ni kweli amekamatwa lakini ratiba ya Mkutano wa Tarehe 10/04/2025 itakuwepo palepale. Kwahiyo jiandae kuwepo eneo la Mkutano Tarehe 10.
Wakili wa Serikali: hiyo Tarehe 10 sasa nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Tulikusanyika uwanja wa Matalawe kusubiri viongozi walioambatana na Mwenyekiti kuhutubia mkutano.
Alikuwepo Godbless Lema na Dr. Wilbroad Slaa pia alikuwepo Mh. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Mh. Heche.
Wakili wa Serikali: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakati tunasubiria likatokea gari ya Polisi na kusema kwa siku hiyo hakuna mkutano utakaofanyika eneo hilo. Na haruhusiwi mtu kukaa eneo hilo.
Wakili wa Serikali: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Ikabidi tutawanyike na kuelekea ofisi za Chama ili tufahamu kwa siku hiyo nini kitaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Ziko wapi hizo ofisi?
Shahidi wa kificho P6: Ziko Songea sehemu inaitwa Mfaranyaki.
Wakili wa Serikali: kikaendelea nini?
Shahidi wa kificho P6: tuliwakuta viongozi ambao ni Adel Mayala ambae kwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini.
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakaja Polisi wakapiga mabomu ya machozi na kusema watu wote watawanyike.
Wakili wa Serikali: Saa saba mchana nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P6: Alikuja kiongozi Makamu Mwenyekiti na kusema kwamba amepokea barua kutoka Polisi kwamba kwa siku hiyo usifanyike Mkutano wa aina yoyote katika eneo hilo.
Wakili wa Serikali: Akasema nini kingine?

Sehemu ya 170

Shahidi wa kificho P6:
Akasema tutawanyike na atapanga tarehe nyingine ya mkutano huo.
Wakili wa Serikali: Huyo Makamu Mwenyekiti ni nani?
Shahidi wa kificho P6: Ni Heche.
Wakili wa Serikali: Tarehe 18/04/2025 nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Nilipokea taarifa kuwa tarehe 20/04/2025 siku ya pasaka kutakuwa na matembezi ya hiyari ambapo katika matembezi hayo yataambatana na kuvalia tshirt zilizoandikwa agenda ya No Reforms: No Election ili kuendeleza agenda ya Chama.
Wakili wa Serikali: Kingine kilichoendelea?
Shahidi wa kificho P6: Ukafanyika utaratibu wa kuzipata tshrit na tunachangia elfu 10 ndipo zitasafirishwa hadi kutufikia.
Tukaambiwa hadi kufikia tarehe 20 basi tutakutana kwa ajili ya matembezi hayo ya hiari.
Wakili wa Serikali: Tarehe 20/04/2025 kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Tulijikusanya kwa ajili ya matembezi ya hiari kila mmoja alipata tisheti yake na tukakubaliana jioni majira ya saa 10 ndio matembezi ya hiari yatafanyika.
Wakili wa Serikali: Ulipata wapi hizo taarifa:
Shahidi wa kificho P6: Group la Siasa Yetu.
Wakili wa Serikali: Matembezi mlikubaliana mkutane wapi?
Shahidi wa kificho P6: Songea Mjini kwa Disi Kitimoto na ilipofika majira ya saa 10 huku tukiwa na bodaboda huku tukisubiri wengine. Mimi nilikuwa kwenye muonekano wa kuvaa tshirt iliyoandikwa agenda ya No Reforms: No Election.
Wakili wa Serikali: Nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Wakaja Polisi wakajitambulisha kwa ghafla kuwa wanatokea kituo cha Polisi Songea na wakatuambia tunahitajika kituo cha Polisi Songea kwa ajili ya mahojiano.
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P6: Walitukamata na kutupeleka kituo cha Polisi Songea na wakatuhoji kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.
Wakili wa Serikali: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakasema tutatoka kwa dhamana lakini tulihitajika kwenda kuripoti ofisi ya RCO.
Wakili wa Serikali: Tarehe 25/04 nini kiliendleea?
Shahidi wa kificho P6: Tuliripoti Ofisi ya RCO tumuelezee kilichotokea hadi kufika sehemu hiyo.
Wakili wa Serikali: Mhe. Jaji ndio hayo kwa shahidi huyo.
Watu wanashangaa sasa huyu shahidi sijui alikuwa anazungumza nini na kinasaidia nini kwenye Uhaini ni Maajabu, ngoja Tunasubiri aanze kuulizwa maswali hapa.
Jaji Ndunguru: Vipi mshitakiwa tukupe nafasi ujikusanye vizuri?
Lissu: Mhe. Jaji huyu shahidi nilishajiandaa nae toka juzi.
Sasa shahidi sijui wewe ni Kaka au Dada lakini naomba ujibu maswali yangu sawa?
Shahidi wa kificho P6: sawa.
Lissu: Uliandika maelezo Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Sijaelewa swali.
Lissu: Kitaeleweka tu. Jibu swali langu Bwana.
Shahidi wa kificho P6: Niliandika
Lissu: Ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?
Shahidi wa kificho P6: Ndio.
Lissu: Ulisaini?
Shahidi wa kificho P6: Sikumbuki.
Lissu: Mhe. Jaji naomba aonyeshwe maelezo yake.
Shahidi wa kificho P6: Nimeyapata na ndio maelezo yangu niliyoandika Polisi Songea.
Lissu: Je yana sahihi yako?
Shahidi wa kificho P6: sahihi yangu ipo ndio.
Lissu: Ni maelezo ya Tar. 25/04/2025.
Shahidi wa kificho P6: Sioni hiyo Tarehe.
Lissu: Angalia juu mwanzoni, anamsomea hilo eneo.
Shahidi wa kificho P6: Sijayaona hayo maelezo.
Lissu: Waheshimiwa Majaji nataka ku impeach huyu shahidi, nitamsomea maelezo yake, anamsomea hapa.
Mimi ni mkazi wa Bombambili, kazi yangu Bodaboda na kituo changu ni miembeni.

Ilipofika mwaka 2025 nilimfuata Katibu wa Vijana Essau Chiza alinikaribisha kwenye Chama na kunifanyia mpango wa kadi ya Chama.

Nakumbuka tarehe 04/04/2025 niliona mtandao wa youtube hotuba ya Lissu iliyokua inahusu uchaguzi 2025 iliyokuwa ikihamaisha uasi. Ilinipa moyo wa kijasiri wa kutaka kuvuruga uchaguzi.

Nikamtafuta Essau Chiza ambae ni Katibu kunipa mipango mingine ikiwemo ziara ya Mwenyekiti Taifa.

Anaendelea kumsomea maelezo yake yote hapa.

Sehemu ya 171

Lissu anaendelea kumsomea Shahidi maelezo yake.

Amemaliza kusoma maelezo anamuonesha maeneo aliyodanganya au kuleta mkanganyiko.

1. Dini
2. Umri
3. Shughuli za Chama alizoambiwa atakuwa anataka kuzifanya
4. Tarehe 04/04/2025 ulikuwa na simu infinix smart 8.
5. Hiyo simu yako lilikuwa na bando la Internet
6. Uliingia kwenye mtandao wa youtube wa Jambo TV
7. Mimi mtuhumiwa nilisema yoyote atakayekuwa nasi tutaenda nae ambae hatataka tutamuacha.
8. Nilisema anayetaka kugombea udiwani au ubunge asahau na mimi niliyetaka kugombea urais nisahau
9. No Reforms: No Election.
10. Wanasema tutafanya uasi ni kweli tutafanya.
11. Niliitoa hotuba yangu ndani ya ukumbi na kulikuwa na bendera ya taifa na ya Chadema
12. Nilivaa kombati za kaki nayo nataka unioneshe.
13. Kwamba tutazuia uchaguzi kwa kufanya vurugu
14. Nataka niyaone maneno ya Mwamba wa Kigoma.
15. Kwamba Mwamba wa Kigoma alikusifia kwa uamuzi wa kishujaa na wewe ni mojawapo ya vijana mnaotakiwa kulikomboa Taifa.
16. Tarehe 06/04/2025 ulipata taarifa kuwa Mh. Tundu Lissu atatembelea Mkoa wa Ruvuma.
17. Ulipewa taarifa ya kumpokea Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Lissu anamsomea maeneo ambayo shahidi amedanganya au ameyasema leo lakini kwenye maelezo yake ya Polisi hajasema.

Anaweza msomea maeneo hata 50.

Kwa kifupi anachokifanya kuyataja hayo maeneo ni kama anamuandaa au kumlainisha shahidi kabla ya kuanza kumsokota, kuonyesha uongo wa shahidi.

Ameonyesha maeneo 20.

Lissu: Anamuuliza je ungependa maelezo yako yapokelewe kama sehemu ya ushahidi na mimi nikuhoji sawasawa?
Shahidi wa kificho P6: Amenyamaza hasemi chochote, hapo haya ndo maelezo yangu na kama kuna kitu hakipo mimi ni binadamu siwezi kukumbuka kila kitu na kama kuna kitu nimekizungumza mahakamani siwezi kukumbuka kila kitu.
Lissu: Shahidi Kaka yangu ungependa hayo maelezo yako yapokelewe kama kielelezo?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu niloyoyaandika Polisi au niliyozungumza hapa Mahakamani ndio nimetakiwa nizungumze mbele ya Mahakama.
Lissu: Wambie ungependa yawe sehemu ya ushahidi mahakamani.
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yangu yawe ushahidi Mahakamani.

Hatimaye amekubali.

Majaji wanaandika sasa.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka?
Renatus Mkude anasema No Objection.
Jaji Ndunguru: Basi maelezo haya yatakuwa ni D4.
Lissu: Anasema ahsante sana, sasa anaendelea.
Kabla hujaapishwa hapa Mahakamani uliulizwa dini yako ukasema wewe ni Mkristo?
Shahidi wa kificho P6: Kweli
Lissu: Waeleze majaji kwenye hayo maelezo yako eneo la dini yako umeweka nini?
Shahidi wa kificho P6: Sijaona hapo.

Anasimama Katuga anaweka pingamizi watu wanamzomea.

Jaji anasema tuendelee
Shahidi wa kificho P6: Hapa Dini imeandikwa sioni vizuri.
Lissu: Dini imeandikwa Muislamu?
Shahidi wa kificho P6: Hapa sioni vizuri.
Lissu: Umri wako je?
Shahidi wa kificho P6: Miaka 23 imeandikwa hapa.
Lissu: Ulisema shughuli za Chama ulizopewa ni kuongoza misafara ya Chama ukiwa na bendera na pikipiki?
Shahidi wa kificho P6: Ni kweli.
Lissu: Sasa hayo maneno yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yanaonesha nitashiriki kwenye mikutano ni vitu ambavyo sikuviandika.
Lissu: Kwahiyo hayo yameandikwa au hayajaandikwa?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo yameandikwa kushiriki mikutano.
Lissu: We Chadema wa Mapolisi usitupotezee muda, tuambie yapo kama yapo.
Shahidi wa kificho P6: Sijui
Lissu: Tarehe 04/04 umesema ulikuwa na simu yako infinix smart 8 tuambie kama hayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Lissu: Sijakuuliza unayafahamu au huyafahamu, nimekuuliza yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.

Sehemu ya 172

Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P6.

Lissu: Jaji naomba shahidi ajibu maswali yangu.
Jaji: Hebu muulize tena.
Lissu: Hayo maneno ya simu infinix smart 8 yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Jaji: Nafikiri lengo lako mshitakiwa ni ku empeach credibility ya shahidi kwahiyo akisema hafahamu wakati kielelezo kipo na sisi Mahakama tutakipitia. Basi acha aendelee kusema hafahamu.
Lissu: Maneno kwamba ulikuwa na bando la kuingia YouTube hebu tuoneshe kwenye maelezo yako hapo?
Shahidi wa kificho P6: Yapo.
Lissu: Tuonyeshe.
Shahidi wa kificho P6: Majira ya saa nne niliona mtandao wa YouTube hotuba ya Tundu Lissu.
Lissu: Swali langu ni ulikuwa na bando la internet.
Shahidi wa kificho P6: Hayo hayapo.
Lissu: Kumbe una akili unaelewa. Tukienda hivi itakuwa vizuri. Haya tuendeleee.
Ulisema uliingia katika mtandao ya Jambo TV?
Shahidi wa kificho P6: Nilisema niliingia kwenye account.
Lissu: Hivyo hivyo account eheee yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Lissu: Umeeleza kwamba wakati nahutubia huo Mkutano nilisema maneno kwamba yeyote atakayekuwa nasi tutaenda nae na asiyetaka tutamuacha, yapo kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Lissu: Ulisema nilisema kuwa kama kuna anayetaka kugombea udiwani asahau na anayetaka kugombea ubunge asahau, hayo nayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Polisi nilitoa ila hapa kwenye maandishi sioni.
Lissu: Ahsante, Polisi ni waongo wamekuibia maneno yako, tuendelee.
Haya umesema nilisema maneno No Reforms, No Election, haya ni maneno yangu kweli nimeyasema sana.
Shahidi wa kificho P6: hayo sikusema. nilisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Lissu: Basi twende na hayo hayo, yapo kwenye maelezo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: Hayo maneno siyaoni kwenye maelezo.
Lissu: Turudi kwenye simu kwenye maelezo yako yote Polisi nataka uniambie ulisema kama ulikuwa na simu popote pale? Nataka unioneshe humo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Nilisema nimejiunga na magroup ya WhatsApp kwahiyo maana yake ni simu.
Lissu: Waeleze majaji kama maneno ya bendera za taifa na Chadema yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Lissu: Kwamba nilivaa kombati za Kaki nayo pia yapo humo kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo siyaoni.
Lissu: Umemuelezea mtu anaitwa Essau Chiza pia anaitwa Mwamba wa Kigoma sasa tuoneshe Mwamba wa Kigoma kama yapo?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Lissu: Ulisema Essau ni Katibu sehemu nyingine ni Mwenyekiti kipi ni kipi?
Shahidi wa kificho P6: Mimi sijasema hivyo.
Lissu: Sasa wewe leta hayo maelezo nikuoneshe, anamsomea aliposema Mwenyekiti na aliposema ni Katibu.
Shahidi wa kificho P6: Mimi sikusema hivyo watakuwa polisi ndio walikosea.
Lissu: Pole kwa kuingizwa chaka na mapolisi.
Shahidi wa kificho P6: Ahsante sana.
Lissu: Ulisema ulivyohamasika kufanya vurugu tuoneshe hizo habari nazo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: anasoma mambo tofauti kabisa.
Lissu: Wewe ulihamasika kwamba utazuia uchaguzi kwa kukinukisha ndio nayataka yapo?
Shahidi wa kificho P6: Mimi binafsi maneno ya Mwenyekiti wa Chama yalinihamasisha na kupata moyo wa kijasiri na kunipa hamasa ya kuvuruga uchaguzi mkuu 2025 kwa kukinukisha.
Lissu: Ohoo Hongera sana kumbe wewe na mimi letu lilikuwa moja ila Mwenzangu uko kizimba cha shahidi nashangaaa. Haya tuendelee lakini.

Sehemu ya 173

Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P6.

Lissu: Pameandikwa tarehe 06/04 kutakuwa na ziara ya Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Songea, umeona vizuri hapo.
Shahidi wa kificho P6: Naweza kurudia pia wilaya ya songea anaisoma.
Lissu: Twende Tarehe 10/04 umesema hivi ukiwa umekusanyika uwanja wa shule ya Msingi Matalawe na kuwataja viongozi ghafla gari ya polisi ilifika na kuwatawanya. Waeleze majaji kama hayo maneno gari la polisi lilifika na mkatawanywa.
Shahidi wa kificho P6: Hayapo hayo.
Lissu: Kuhusu kwenda ofisi za Chama Mfaranyaki mlikoenda na viongozi wakataka kuzungumza na waandishi wa Habari kuwa polisi walifika na kuwapiga mabomu?
Shahidi wa kificho P6: Kutupiga mabomu hayapo kwenye maelezo.
Lissu: Je, wapi kuna maneno kuwa polisi waliwatawanya ofisi za Chama.
Shahidi wa kificho P6: Hayapo kwenye maelezo yangu.
Lissu: Sasa ngoja nikuulize mengine baada ya kumaliza kukutembeza kwenye maelezo yako.
Lissu: Kwa ufahamu wako Kiongozi wa Chama kama mimi kuitisha mkutano na kusema bila mabadiliko hakuna uchaguzi ni kosa la jinai?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu mimi.
Lissu: Kusema tutazuia uchaguzi nalo ni kosa la jinai?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu pia.
Lissu: Unafahamu hakuna sheria yoyote nchi hii inayokataza kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa kificho P6: Huko kwenye sheria mimi sifahamu.
Lissu: Polisi hawakukwambia kuwa sio kosa? Hao waliokuwa wanakufundisha kuja kusema hapa.
Shahidi wa kificho P6: Amenyamaza
Lissu: Ulisema mikutano ya Songea ilizuiwa kufanya mikutano na kupigwa mabomu. Je hiyo ni sawa na ni haki ya kisheria kwa Chama?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Lissu: Unafahamu polisi wa Tanzania hawana mamlaka ya kukataza mikutano?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Lissu: Unajua Mikutano hiyo ilitolewa taarifa siku mbili nyuma?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Lissu: Kwani wewe si ndio umesema ulikuwa umehamasika na Chadema?
Shahidi wa kificho P6: Ndio hivyo sasa sifahamu.
Lissu: Ulivaa tshirt imeandikwa No Reforms, No Election ni kosa?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Lissu: Ulikamatwa Tar. 20/04/2025 mkiwa katika eneo la DS Kitimoto mkakamatwa kwa tuhuma za kufanya maandamano yasiyo ha hiari ni kweli?
Shahidi wa kificho P6: Kweli
Lissu: maelezo ya hayo mahojiano yako wapi?
Shahidi wa kificho P6: Sifahamu.
Lissu: Hizo tuhuma ziliishia wapi za kutaka kufanya maandamano na kuhojiwa?
Shahidi wa kificho P6: ndio tulipelekwa Mahakamani ila kaka angu alikuwa ananiwakilisha.
Lissu: Kwahiyo Kaka yako alishtakiwa badala yako?
Shahidi wa kificho P6: ndio yeye alikuwa anaisimamia
Lissu: Sasa waeleze majaji ilikuwaje ukabadilika kuwa mtuhumiwa wa kupanga njama za kufanya maandamano na leo ukawa shahidi?
Shahidi wa kificho P6: Hata mimi sijui nini kilitokea.
Lissu: Polisi walikwambia ukiwa shahidi kwenye kesi hii watakufutia mashitaka yako si ndio?
Shahidi wa kificho P6: Hapana Mheshimiwa we acha tu.
Lissu: Wewe ni Mwanachama wa Chadema?
Shahidi wa kificho P6: Ndio.
Lissu: Umeingia lini? Niambie tarehe na mwezi.

Katuga amesema hilo swali akijibu ataweza kujulikana maana kwenye mfumo wanajulikana watu waliosajiliwa ni akina nani siku fulani.

Majaji wamejadili kama dakika tano. Tunasubiri watasema nini?

Sehemu ya 174

Anaendelea Tundu Lissu

Lissu: Mhe. Jaji hawako serious hawa kwanza ukisoma D4 kila kitu chake kipo hata jina lake hawajaficha lipo na taarifa zake zote zipo, hawajielewi hawa.
Katuga: Anasimama anasema Mh. Sisi ni maafisa wa mahakama aonywe mshitakiwa kwanini anasema hatuko serious.
Lissu: Mhe. Jaji ni kweli hayupo serious ila nataka niliondoe neno hilo lakini kama anasema nionywe siko tayari kuonywa naomba nifanye submission ya kuonesha ni kwa namna gani hawako serious?
Jaji Ndunguru: Basi Mshitakiwa tuishie hapo kama umesema umeliondoa.
Lissu: Je, umesema kokote kuwa uliwahi kutishiwa maisha?
Shahidi wa kificho P6: Sijawahi kutishiwa maisha mimi.
Lissu: Kuna mwanachadema au kiongozi amewahi kukutishia kukupiga au kukudhuru kwa wewe kwenda kutoa maelezo haya Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo kabisa.
Lissu: Je, kuna ndugu yako ametishiwa pia?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo hata mmoja.
Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.

Majaji wanaandika kidogo pale mbele.

Kwa sasa ni saa 7 na dakika 15 mchana, huu ni huwa ni muda wa kwenda Break, ngoja tusubiri Kitakachoendelea muda mfupi ujao.

Jaji: Re Examination Jamhuri?
Wakili Cathbert: Hatuna swali lolote Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru Kiogozi wa Jopo la Majaji watatu anateta tena ma wenzake kabla hajasema nini kiendelee.

Anawasha kipaza sauti.

Shahidi umemaliza sasa unaweza kwenda.

Renatus Mkude tunaomba ahirisho tukawaandae mashahidi, lisaa limoja.

Lissu: Sawa sina pingamizi.
Jaji Ndunguru: Basi tukutane baada ya saa moja.

Sehemu ya 175

Mahakama imerejea.

Anasimama Renatus Mkude na kusema tuko tayari kuendelea na tuko na shahidi wa wazi.

Muda huu tunaendelea na shahidi ambae ni H3923 Detective Coplo Michael, Mimi ni askari Polisi. Mimi ni Mristo.

Huyu Polisi mwingine ni shahidi ambae atakuwa ni PW6 Anaongozwa na Ignas Mwinuka, Wakili wa Serikali.

Detective Koplo Michael anasema anaishi Kiusa Street, Moshi Kilimanjaro.

Ninafanya kazi Askari Polisi, naifanyia kazi yangu ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro, nimekuwa katika ofisi hiyo tangu mwaka 2015.

Nimejiunga Jeshi la Polisi mwaka 2012 na kuhitimu mwaka 2013, nilipata mafunzo ya awali katika shule ya Polisi Tanzania TPS kwa maana ya Shule ya Polisi iliyopo Moshi.

Majukumu yangu ni upelelezi wa makosa ya jinai, ukamataji wa wahalifu, kuzuia uhalifu pamoja na majukumu mengine mbalimbali ya jeshi la Polisi.

Tarehe 08/04/2025 nakumbuka majira ya asubuhi nilikuwa doria na askari wenzangu tulikuwa tunazungukia maeneo mbalimbali ya Moshi mjini.

Anaendelea Detective Koplo Michael anasema lengo ni kufanya doria, kukamata wahalifu na kulinda raia na mali zao.

Tukiwa tumefika maeneo ya Njoro hapo wilayani Moshi, tulipata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kijana mmoja anahamasisha wenzake kuhusiana na kufanyika na Uchaguzi Mkuu uliokuwa unatarajiwa kufanyika mwaka 2025.

Baada ya kupata hizo taarifa kutoka kwa P8 ambae analindwa na Mahakama, tulimkamata mtuhumiwa na kumpeleka ofisi ya RCO kilimanjaro.

Tukampeleka ACP Abichi alinielekeza nifungue jalada la uchunguzi na nilifungua jalada lenye Kumb. No. KR/CID/PE/18/2025 ambalo ni jalada la Uchunguzi.

Afande alisema kijana huyo apigiwe simu na ahojiwe na D. Koplo Rashid na awekwe mahabusu kwanza na atatoa maelekezo baadae.

Wakili Ignas Mwinuka, anaendelea kumuhoji.

Detective Koplo Michael anasema kijana huyo alitolewa kwa masharti awe anaripoti kila jumatatu hapo Polisi.

Ilipofika Tarehe 22/04/2025 Afande RCO aliniambia nimtafute yule kijana anayekuja kuripoti, nimuandike maelezo upya.

Na hayo yalikuwa ni maelezo ya shahidi aeleze ni kitu gani kilichompelekea yeye kuhamasisha wenzake kufanya vurugu katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika.

Nilipofuatilia kumbukumbu nikagundua siku hiyo hiyo ndio alikuwa amepangiwa aje kuripoti, alipofika nilionana nae na nikamuandika maelezo ya shahidi.

Kwenye maelezo yake aliniambia yeye ni MwanaChadema alidai alikuwa Mwanachama toka akiwa anasoma Sekondari.

Alisema yeye ni mkereketwa wa Chadema na alikuwa anaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wake wa Chama Tundu Lissu ndio maana alikuwa anahamasisha fuko na kukinukisha.

Alidhamiria kufanya uasi kwa serikali inayoongozwa na CCM na aliongeza kwa kusema kuwa Mwenyekiti wao alisema hawatakubali uchaguzi kufanyika.

Na wako tayari kukinukisha hadi Serikali watakapofanya marekebisho ya tume huru ya Uchaguzi pamoja na Katiba Mpya.

Baada ya kumuandika maelezo nilimpa ayasaini kila page na akakubali kuwa ni malezo yake.

Waheshimiwa Majaji kwa shahidi huyu ni hayo tu. Amemaliza Ignas Mwinuka.

Credit: Hilda Newton
 
Back
Top Bottom