Kesi ya Lissu na wenzake: Makinda ahalalisha maamuzi ya Ndugai, aingiza kipengele kwenye kanuni

Busara ya mtu yeyote MUUNGWANA ni kuheshimu maamuzi ya mkuu wako hata kama huyapendi.
Au kukubali agizo kutoka kwa mamlaka iliyopo kihalali kwa faida ya baadaye.

Kinyume chake ni kukosa ADABU.

Ushauri wa bure kwa CDM. Kwa staili hii wasahau 2015 kwa mazonge ya UDINI na UGAIDI.
Wajipange kwa 2025. Waige mfano wa MUSLIM BROTHERHOOD!
washirikiane na wananchi katika kutoa huduma za jamii.
wasilazimishe kupendwa. Itawagharimu sana.

hata hiyo 2025 karibu sana
 
wewe haukumuelewa Spika naona, alitanguliwa kusoma kanuni ziliwasimamisha LISSU na wenzake, ambapo kwayo anaruhusiwa kuingiza hatua hizo kwenye kitabu chake.
Mkuu ebu angalia mwenyewe mbona kiswahili rahisi tuu
"Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu vjambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo."
 
Mkuu ebu angalia mwenyewe mbona kiswahili rahisi tuu
"Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu vjambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo."
kumbuka hata bunge hutunga sheria za nchi kutokana na kujitokeza kwa jambo ambalo halina tafsiri ya kisheria. rejea sheria ya ugaidi ya mwaka 2002. sheria hiyo ilitungwa kwa vile hakukuwa na sheria kwa mtu anayefanya kosa la kigaidi na wakati huo Tanzania tulikumbwa na tukio la kigaidi mwaka 1998 kwenye ubalozi wa marekani
 
Kwa hiyo Serukamba, Nkamia na Luside ni wabunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo au mbunge gani wa chadema ambae ametoa/alitoa matusi bungeni...shirikisha ubongo wako siyo suti za kuhongwa na waarabu na kulipiwa chumba...
wewe upo mtaa gani ambao hao ccm hawapo???? kwa hiyo chadema huko mitaa yako wanaunga mkono matusi,vurugu na fujo bungeni???? acha ujinga nenda ukale, mida hii.
 
Bunge siku hizi limesababisha futuhi na kina masanja wakose wafuasi
Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika. Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu vjambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.

Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo.

Sitaki kuweka hisia zangu naleta kama ilivyowasilishwa na Mh Anne Makinda
 
Habari zetu wana jf, nimeangalia haya mambo yanayoendelea katika taifa letu, hususani suala la vikao vinavyoendelea mjini Dodoma vya bunge. Nimegundua chanzo cha mambo mengi ni serikali ya ccm, na ccm yenyewe, kutokujali maslahi ya taifa letu na kuendeleza maslahi ya chama pekee. Hili limesababisha bunge kuongozwa kiccm zaidi kuliko kufuata kanuni na sheria! Mfano mzuri ni suala la kina lissu ambapo mpaka leo imeonekana hakuni kanuni zilizokiukwa, na kusababisha spika makinda kupenye kifungu haramu ili kubariki maamuzi hayo feki. Madhara yake tutakuwa na taifa lilogawanyika vipandevipande. Ccm hawawezi kukwepa lawama hii, kwa sababu wao walitakiwa kuonyesha mfano kama chama kikongwe kwa taifa letu! Nawasilisha!
 
kumbuka hata bunge hutunga sheria za nchi kutokana na kujitokeza kwa jambo ambalo halina tafsiri ya kisheria. rejea sheria ya ugaidi ya mwaka 2002. sheria hiyo ilitungwa kwa vile hakukuwa na sheria kwa mtu anayefanya kosa la kigaidi na wakati huo Tanzania tulikumbwa na tukio la kigaidi mwaka 1998 kwenye ubalozi wa marekani
Ebu nifumbue macho Speaker yeye kama yeye anaweza pitisha KANUNI na ikaanza kuwa effective?
 
Busara ndo inayomsaidia Mbowe laiti wote wangejifunza kuwa na busara kama yeye ingesaidia sana.
Kwani mimi naamini kuna namna ya kuonyesha kukasirishwa na jambo na ukatoa mawazo yako kwa hasira bila hata chembe ya tusi na ukaeleweka vizuri tu.

Busara kama ya Mbowe ni sawa na vyema wabunge wa CDM wangemuiga ila hapo kwenye matusi ni baadhi ya wabunge wa ccm ndo waliotukana, CDM hawakutukana kabisaaa

 
Aweda, wewe kama kiongozi wa chama ngazi ya maamuzi, ningekuomba usimame katikati ili uwe mshauri mzuri uwapo vikaoni...

1.ni kweli amani ni tunda la haki,hilo halina mjadala
2. kama unaamini maelezo yako ya mtenda na mtendewa, je unakumbuka mchango wa Godbless lema???? unakumbuka mwigulu alikuwa anajibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na lema kwamba kikwete ndio muasisi wa udini ndipo mwigulu akasema slaa ndio mwasisi wa udini katika uchaguzi mkuu wa 2010 na akatoa ushahidi kuwa akiwa singida alifanya mikutano/vikao vya kampeni na viongozi wa dini flani badala ya kufanya vikao/mikutano hiyo na wananchama wa chadema???

susan kiwanga alieleza vizuri kwamba yeye ndio alikuwa mratibu wa kampeni na ndie aliyeandaa mikutano ya kampeni ya dr slaa huko singida, alipinga vikali madai ya mwigulu.....

hatua ya ndugai kuzuia miongozo mingi ilikuja baada ya kuwa amemruhusu susan akatoa maelezo hayo mazuri na akataka kutokupoteza muda kwa kuwa aliyekuwa anachangia alikuwa ni mchangiaji wa mwisho ili kuahirisha bunge na alitaka kutoa haki kwa mchangiaji huyo kama alivyotoa haki hiyo kwa lema aliyetamka na kusimamia kauli yake kuwa kikwete kwa jina ni mdini hadi akatakiwa kuthibitisha ndani ya siku saba. hapo ndio kanuni ya action na reaction inapokuwa chungu inapong'ata kwako...aweda, ilin uwe mwanasiasa mzuri, kubali ukweli wa madhaifu yako uweze kujikosoa na kukosolewa.. lisu na wenzake walikosea.
Hiyo ndiyo tunayoiita double standard ya hali ya juu ya kupindkia!!

Kama wewe mwenyewe unakiri kumsikia Suzane Kiwanga kulikanusha aliloliongea Mwigulu Nchemba, ni kwa nini basi hakufanya kama alivyomfanyia Lema, la kumtaka Mwigulu naye aidha afute kauli yake au alete ushahidi katika siku 7. Sasa ni kwa nini Ndugai hakumpa hizo siku 7 ili alete huo ushahidi kuwa Dr Slaa, kwenye kampeni za mwaka 2010 mkoani Singida, hawakufanya kwenye majukwaa ya kisiasa, badala yake alifanyia kwenye nyumba za ibada??!!
 
Pengine tuwashangae wale ambao walitebgemea maamuzi tofauti na aliyoyatoa Spika! Kanuni zinamruhusu kutunga za kwake kuhalalisha maamuzi yamakosa yaliyotendeka. Kikao hakitaisha mmoja wa wabunge wa chama chake atafanya kosa na tuone ataamua vipi. Ni makosa kutengeneza kanuni kwa kulenga mtu au kikundi fulani.
 
FUMBO

Jamani ni saidieni. NDUGAI kila akiombwa mwongozo hudai atatoa baadaye. MAKIDA naye hivyo hivyo, alipoulizwa na Mbowe jana.
Hii inaonyesha kuna mtu anawapa mwongozo! JR HUYU NI NANI
 
Spika wa Bunge ana Makinda amehalalisha maamuzi ya Ndugai ya Kuwasimamisha Lissu na wenzake wakae nje ya Bunge kwa siku 5.

Katika hukumu hiyo, Spika amesema japokuwa hakuna kifungu kilichovunjwa,lakini kuna kifungu kinachosema kama hakuna kifungu cha kanuni kilichovujwa basi kiti cha spika kinaweza kufanya uamuzi na uamuzi huo mpya ukaingizwa katika kanuni na kuanza kutekelezwa kuanzia siku hiyo.

Hivyo, adhabu ya kukaa nje kwa siku 5 ni halali na itatumika kuanzia sasa kwa wabunge wengine watakaofanya vitendo vitakavyofanana hivyo mbele ya safari.

My take,
Je, kama ndivyo, hiyo kanuni yenyewe si mwisho wa siku itakosa maana? Je, spika na naibu wake wakitofautiana kimtazamo itakuwaje?
Kwa staili hii, 2015 ni mbali sana.


Jee tutasema tunaendeshwa na mfumo hai wa demokrasia ikiwa kanuni hazijavunjwa lakini speaker akaamua tu kuwa kumevunjwa na akatoa hukumu za namna hii kweli tutaliita bunge huru, jee hakuna harufu za misuse of power? naamini kuna wanaccm wengi wasioridhishwa na uongozi wa sasa wa bunge.

Hebu na waangalie house of common prime minister anapozomewa na kukatishwa hotuba zake na wapinzani huku speaker akiact bila ya bias kuhakikisha stability na heshima ya bunge inakuwa maintained.

hebu tazama link hii: Bumge lina heshima ya kipekee ambalo kwa wenzetu desturi za kupingwa za namna hii hatuna ndio chanzo cha machafuko bungeni..history itamkumbuka Mheshimiwa Sita kwa namna alivyoliongoza bunge ..
Top five PMQs moments of 2000 to '09 (16Dec09) - YouTube
 
Ieleweke kwamba bi kiro. . ni mwana CCM na hao CCM kazi yao ni kutetea yale yote wanayoyafanya wao 'mabaya yote wanatetea kwamba ndiyo mazuri' eg F*ck You kwao ni 'Ndiyooo'.
Kwahiyo ktk hili bi kiro. . . lazima afagilie ujinga wao
 
Back
Top Bottom