Kesi ya Lissu: CCM wakodi shahidi toka Dar es salaam

Shahidi amekiri analipwa kila anapokuja kutoa ushahidi
Hii pia ni dhahiri kuwa hata ushahidi wanaoutoa ni wa kutengenezwa
As a lawyer, mashahidi wote ulipwa wanapoitwa mahakamani. Kama hujui kitu usizungumze utaonekana zuzu. Ndiyo maana hat LT ameishia hapo kwa kuwa is an sdvocate and knows what is what
 
Zinaendaga hiv hiv kama ya Mh. Lema.. Mwisho mnacikia matokeo yametenguliwa.. Halafu wajinga wanakuja kutuambia ati mhimili wa mahakama hauingiliwi..
 
As a lawyer, mashahidi wote ulipwa wanapoitwa mahakamani. Kama hujui kitu usizungumze utaonekana zuzu. Ndiyo maana hat LT ameishia hapo kwa kuwa is an sdvocate and knows what is what

Wanalipwa nini? Kuwawezesha kufika mahakamani (reimbursables) au ujira kwa ajili ya kutoa ushahidi (honoraria)?
 
As a lawyer, mashahidi wote ulipwa wanapoitwa mahakamani. Kama hujui kitu usizungumze utaonekana zuzu. Ndiyo maana hat LT ameishia hapo kwa kuwa is an sdvocate and knows what is what

sidhani km wewe ni mwanasheria, mashahidi ulipwa ili iweje?. Hapo Lissu hakuendelea, ila katika majumuisho ndo utaona. Nakushauri rudi chuo kisha nenda law school, utajua technic kama hizi.
 
Mtoa hoja umesahau ku-update uzi wako, kama vipi tuambie nini kimejitokeza kwa kort singida town.
 
Inasikitisha kwa Kweli! yaani kesi ni yakupoteza muda! na kutumia hovyo rasilimali zetu.

Mwisho wa siku jaji atamvua ubunge lisu kwa kwa ushahidi huo huo wa kizushi; Kwa vyovyote vile maelekezo kutoka Ikulu yataheshimiwa na mhishimiwa jaji
 
HUKU SUMBAWANGA NAKO KESI IPO HIVI:
Mlalamikaji Ndugu NORBERT YAMSEBO - CHADEMA Mlalamikiwa Ndugu Aeshi Hilali - CCM (Mbunge)

Mlalamikaji aliwaleta mashahidi 19 Mahakamani. Na mlalamikiwa alileta Mashahidi wanne kumtete.
TUHUMA:
1. Shahidi aliieleza Mahakama Jinsi Mlalamikiwa alivyotoa Rushwa ya Mifuko 20 ya Sementi kwa Kanisa Katoliki Kigango cha Katumba - Parokia ya Pito - Sumbawanga
2. Shahidi wa pili alirudia ushahidi huo kwa kueleza alivyokabidhiwa mifuko hiyo ya Sementi iliyotolewa kwa Kanisa hilo kwa masharti ya waumini wamchague katika Uchaguzi wa Ubunge kwa kuwa yeye ni Mgombea wa nafasi hiyo.
3. Shahidi wa Tatu alitoa ushahidi juu ya Rushwa ya Mlalamikiwa kutoa Tsh 100,000/= na Bati 200 kwa Kanisa Katoliki Kigango cha Mtibwa - Sumbawanga, kwa sharti la kuchaguliwa
4. Shahidi wa NNe alitoa ushahidi kuhusu Mlalamikiwa kununua Pombe ya Kienyeji kwa ajili ya Wana kijiji cha Pito-Sumbawanga kwa masharti ya kumchagua
5. Shahidi wa Sita alizungumzia kuhusu mlalamikiwa kutoa Zawadi za Baiskeli kwa Vijana katika kijiji cha Pito
6. Shahidi wa Saba alieleza namna Mlalamikiwa walivyota Tsh. 2,500 kwa vijana 200 katika ukumbi wa shule ya msingi Kantalamba Mazoezi.
7. Jinsi kura zilivyobadilishwa katika kituo cha Kata ya Katandala - Sumbawanga na kusomwa tofauti katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi
8. Jinsi Masanduku yalivyocheleweshwa kwa massa 12 kufika ofisi ya Msimamizi kutoka kituo kikuu cha kata ya katandala kwende ofisi ya msimamizi sehemu yenye umbali wa kilomita 1.5 (moja na nusu)

MLALAMIKIWA WA MAGAMBA - CCM
Hakuwa na watetezi; alilazimika kujitetea mwenyewe kwa kusema hayo yote ni "UONGO"

Mniwie radhi kwa kuwajuza habari ya kesi hii katika blog isiyo mantiki na yangu. nimefanya hivi makusudi ili mpate majumuisho ya kesi za uchaguzi zinavyoendelea. kesi hii itatolewa hukumu tarehe 30/04/2012
Ahsante Mkuu kwa taarifa hii muhimu tuko pamoja saana, endelea kufatilia utupe matokeo!!!!!!!!!!
 
Kesi za kutengeneza ni ngumu sana kuziendesha! hii kesi inastahili kutupiliwa mbali kama aina ya mashahidi ndio hao!
 
Wana Cdm hutawaona magamba kwenye thread za maana kama hizi wanakimbilia udini tu kama wakina Ritz na wenzake hapa wanapita tu wanasema kwa aibu "no comment"

Ulitaka watoe mchango gani kama wanavyovipika haviivi? wao wanataka ushindi tu kwa gharama yoyote. Hivyo kumpeleka mtu wa IT ambaye anaweza kujua font size and type, to them huyo ni shaidi anayetoa ushaidi wa kitaalamu. Lakini tusishangae kusikia JAJI katoa hukumu inayowapa ushindi CCM kwa vile na JAJI naye ni "mchezaji" wao.
 
Hii imenifurahisha sana maana naona Jaji ameweka wazi kwamba maelezo ya shahidi ni irrelevant. Japo nilishangaa kwanini Tundu Lissu aliendelea kumhoji. Lakini huwezi jua bana, Jaji anaweza kuonyesha kwamba ushahidi wa shahidi huyo ni irrelevant na siku ya hukumu ukashangaa anamnukuu huyo shahidi.

JAJI: Tumbie nini unaona, acha kutueleza mambo ya font size, utuambie yanayoonekana kwa macho kila mtu aweze kuona. Kwanza haupo qualified, na hujawahi kutangazwa na gazeti la serikali, hivyo tunasikiliza tu ushahidi wako.


Walalamikaji wanachofanya ni kuleta mashahidi wengi kadiri wanavyoweza, labda kuna mmoja au wawili wanaweza kutoa ushahidi ambao unaweza kumshawishi Jaji.
 
Hawa jamaa wanachokifanya ni kuhamisha mawazo ya cdm na kuwafanya kuhangaika na mambo yasiyokuwa na msingi mfano kesi zisizo na tija, mwisho wasiku cdm wapotee kwenye lengo mfano campein ya M4C. Ushauri wangu Cdm wajipange kuwadhibit hawa watu.
 
Pamoja sana makamanda. Tusirudi nyuma hata kidogo manaake ukombozi wetu wanauchelewesha tu lakini kuuzuia kabisa hawawezi hata kidogo. Tupambambane nao usiku na mchana mpaka kieleweke. Viva kamanda Lisu, kamanda Lema, na wengineo wote kwa pamoja.
 
Kuna mchezo mchafu unafanywa na CCM ili wapitishe miswada mibovu bungeni. Wanajua uwezo wa Lissu kuchambua mambo na sasa wanatumia hii kesi ili asiweze kuhudhuria vikao vya bunge! Wakili wa CCM kama mmegundua anafanya mchezo wa kuigiza, kila kukicha anaomba kuongeza mashahidi, na hakuna hata shahidi mmoja anaonekana kujua nini kinaendelea! Hii yote ni kurefusha muda wa kesi, by the time wanamaliza na vikao vya bunge vitakuwa vimeisha! Miswada mibovu itakuwa imepita bila bugdha!
 
Mwanga sikuzote utalizidi giza; pamoja wenye nguvu za giza na pesa watashindwa
 
Dawa yao ni kuwapiga chini tu 2015, safari hii hata kwa viboko watatoka tu, hakuna cha kuiba kura wala kutangaza matokeo ya uongo, lazima vijana wafanye kazi yao kama Arumeru Mashariki kwa kulinda kura zetu!!!
 

KESI YA TUNDU LISSU CCM WAZIDI KUJICHANGANYA.
SHAHIDI:23.
SHAHIDI Stephen Jude, 37, Anaishi Dar, Tabata.
Mtaalamu wa ICT, and information and communication technology. Elimu yake ni ICT-Higher national Diploma 1999, London. Cyberom Certified network-Masuala ya usalama ya kimtandao.
Kwa miaka kadhaa nilikuwa katika technical support, and customer service. ( Head of Department.). katika kampuni ya Certcom Africa Limited, na sasa ni business development and public relations katika kampuni hiyo.
Wakili: Upo mahakamani, ni nini hasa kimekufanya uje hapa kuja kutoa ushahidi.
PW: Nilipata mawasiliano kama wiki mbili hivi, nilitumiwa documents ili niweze kujua kama zimeandaliwa katika Chanzo kimoja., Nilifanya physical identification, na baadaye technological identification
JAJI; Samahani wakili, niambie kama shahidi wako anafanya kazi, na anatambuliwa na serikali au NGO?.
Wakili:Kwa kuwa yupo hapa, naomba aseme mwenyewe.
PW: Mimi niliwahi kusaidia kuandaa website ya Taifa, iliyozinduliwa na Mkapa,
JAJI: Mimi sihitaji mambo ya Mkapa, je uliwahi kutangazwa kwenye gazeti la serikali?
JAJI: Basi huna sifa
Umesema kuwa ulipewa Nyaraka, je tukikuonyesha unaweza kuzikumbuka?
WAKILI:Tusaidie umeona nini?
PW: Nimgeundua kuwa zote zimeandikwa kwa Times New Roman., Jingine ni ‘font size' zote zimefanana katika barua zote.
JAJI: Tumbie nini unaona, acha kutueleza mambo ya font size, utuambie yanayoonekana kwa macho kila mtu aweze kuona. Kwanza haupo qualified, na hujawahi kutangazwa na gazeti la serikali, hivyo tunasikiliza tu ushahidi wako.

MASWALI:
T/L: Umewahi kuniona mahali?
PW: Ukweli sikufahamu kabisa.
T/L: Umewahi kuniona nikiandika chochote kwa mkono?
PW: Kwa kuwa sikufahamu sijawahi kukuona pia.
T/L; Vile vile hujawahi kuniona nina type barua popote
PW: NDIYO.
T/L: Hizo barua kwa kuzingalia tu unaweza kumwambia jaji zimeandikwa na nani?
PW: haiwezekani hata kwa kutumia vifaa
T/L: Mimi nimeshtakiwa kwenye kesi hii kwa sababu inadaiwa kuwa hizo barua nimeandika mimi, kwa muda uliokaa nazo unaweza kusema kuwa barua hizo nimeandika mimi?
PW: katika barua hizi sijaona jina lako
T/L: Kwa hiyo huwezi kusema kuwa zimeandikwa na Lissu?
PW: Hilo haliwezekani.
T/L Katika kuzifananisha fananisha kuna kitu hujakisahau?
PW: Kipo
T/L. Unaweza kumweleza Jaji?
PW: Jaji naomba niangalie karatasi nilipoandika majibu.
JAJI: Sikuruhusu
T/L. Angalia barua zote, uniambie kama hazina muhuri wa ‘received' zinazofanana. Mwambie jaji kama mhuri unafanana au haufanani?
PW; Zinafanana
T/L. Mbona hiyo hukutaja hiyo wakati unajieleza?
PW: Nilipoletewa niliambiwa niangalie kama zinatoka katika chanzo kimoja au la?
T/L. Uliagizwa na nani?
PW: Wakili Wasonga
T/L. Ulilipwa?
PW: SIKULIPWA.
T/L. Hiyo kampuni unayofanyia kazi ni kampuni au ni kituo cha misaada?
PW. Ni kampuni ya biashara.
T/L. Na wewe ni mfanykazi wa kampuni hiyo na unalipwa mshahara na kuifanyia kazi kampuni?
PW: Ni kweli
T/L. Mweleze jaji kwanini katika hili hukulipwa wakati ulitumia muda wa kampuni?
PW; Huwa hatulipwi kabla.
T/L. Kwa hiyo utalipwa ukitoka hapa kizimbani kwa ushahidi unaoutoa?
Pw: NDIYO.
T/L. Mwambie Jaji kama maandishi uliyosema ni Times New roman, yapo katika computer zote zinazotumia Microsoft word? Iwe Kenya, iwe Uganda, au hata mbinguni?
PW: Ndiyo.
T/L. Je kuna tatizo kutumia ‘Times New Roman kuandika barua?
PW: Hakuna
T/L; Kwa kuangalia hayo tu unaweza kusema barua imeandikwa na nani?
PW: Huwezi kabisa kujua.
T/L, Unajua ku copy na kupaste? Pamoja na kusave?
NDIYO.
Unafahamu Flash DISK?

KESI Inaendelea, tutaendelea kuwapa yanayojiri



Asa ikawaje hujaendelea tene kutujuza mkuu!! ama kesi iliishia hapohapo?
 
Back
Top Bottom