Kesi ya Lissu: CCM wakodi shahidi toka Dar es salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Lissu: CCM wakodi shahidi toka Dar es salaam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MADORO, Apr 10, 2012.

 1. M

  MADORO Senior Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  KESI YA TUNDU LISSU CCM WAZIDI KUJICHANGANYA.
  SHAHIDI:23.
  SHAHIDI Stephen Jude, 37, Anaishi Dar, Tabata.
  Mtaalamu wa ICT, and information and communication technology. Elimu yake ni ICT-Higher national Diploma 1999, London. Cyberom Certified network-Masuala ya usalama ya kimtandao.
  Kwa miaka kadhaa nilikuwa katika technical support, and customer service. ( Head of Department.). katika kampuni ya Certcom Africa Limited, na sasa ni business development and public relations katika kampuni hiyo.
  Wakili: Upo mahakamani, ni nini hasa kimekufanya uje hapa kuja kutoa ushahidi.
  PW: Nilipata mawasiliano kama wiki mbili hivi, nilitumiwa documents ili niweze kujua kama zimeandaliwa katika Chanzo kimoja., Nilifanya physical identification, na baadaye technological identification
  JAJI; Samahani wakili, niambie kama shahidi wako anafanya kazi, na anatambuliwa na serikali au NGO?.
  Wakili:Kwa kuwa yupo hapa, naomba aseme mwenyewe.
  PW: Mimi niliwahi kusaidia kuandaa website ya Taifa, iliyozinduliwa na Mkapa,
  JAJI: Mimi sihitaji mambo ya Mkapa, je uliwahi kutangazwa kwenye gazeti la serikali?
  JAJI: Basi huna sifa
  Umesema kuwa ulipewa Nyaraka, je tukikuonyesha unaweza kuzikumbuka?
  WAKILI:Tusaidie umeona nini?
  PW: Nimgeundua kuwa zote zimeandikwa kwa Times New Roman., Jingine ni ‘font size' zote zimefanana katika barua zote.
  JAJI: Tumbie nini unaona, acha kutueleza mambo ya font size, utuambie yanayoonekana kwa macho kila mtu aweze kuona. Kwanza haupo qualified, na hujawahi kutangazwa na gazeti la serikali, hivyo tunasikiliza tu ushahidi wako.

  MASWALI:
  T/L: Umewahi kuniona mahali?
  PW: Ukweli sikufahamu kabisa.
  T/L: Umewahi kuniona nikiandika chochote kwa mkono?
  PW: Kwa kuwa sikufahamu sijawahi kukuona pia.
  T/L; Vile vile hujawahi kuniona nina type barua popote
  PW: NDIYO.
  T/L: Hizo barua kwa kuzingalia tu unaweza kumwambia jaji zimeandikwa na nani?
  PW: haiwezekani hata kwa kutumia vifaa
  T/L: Mimi nimeshtakiwa kwenye kesi hii kwa sababu inadaiwa kuwa hizo barua nimeandika mimi, kwa muda uliokaa nazo unaweza kusema kuwa barua hizo nimeandika mimi?
  PW: katika barua hizi sijaona jina lako
  T/L: Kwa hiyo huwezi kusema kuwa zimeandikwa na Lissu?
  PW: Hilo haliwezekani.
  T/L Katika kuzifananisha fananisha kuna kitu hujakisahau?
  PW: Kipo
  T/L. Unaweza kumweleza Jaji?
  PW: Jaji naomba niangalie karatasi nilipoandika majibu.
  JAJI: Sikuruhusu
  T/L. Angalia barua zote, uniambie kama hazina muhuri wa ‘received' zinazofanana. Mwambie jaji kama mhuri unafanana au haufanani?
  PW; Zinafanana
  T/L. Mbona hiyo hukutaja hiyo wakati unajieleza?
  PW: Nilipoletewa niliambiwa niangalie kama zinatoka katika chanzo kimoja au la?
  T/L. Uliagizwa na nani?
  PW: Wakili Wasonga
  T/L. Ulilipwa?
  PW: SIKULIPWA.
  T/L. Hiyo kampuni unayofanyia kazi ni kampuni au ni kituo cha misaada?
  PW. Ni kampuni ya biashara.
  T/L. Na wewe ni mfanykazi wa kampuni hiyo na unalipwa mshahara na kuifanyia kazi kampuni?
  PW: Ni kweli
  T/L. Mweleze jaji kwanini katika hili hukulipwa wakati ulitumia muda wa kampuni?
  PW; Huwa hatulipwi kabla.
  T/L. Kwa hiyo utalipwa ukitoka hapa kizimbani kwa ushahidi unaoutoa?
  Pw: NDIYO.
  T/L. Mwambie Jaji kama maandishi uliyosema ni Times New roman, yapo katika computer zote zinazotumia Microsoft word? Iwe Kenya, iwe Uganda, au hata mbinguni?
  PW: Ndiyo.
  T/L. Je kuna tatizo kutumia ‘Times New Roman kuandika barua?
  PW: Hakuna
  T/L; Kwa kuangalia hayo tu unaweza kusema barua imeandikwa na nani?
  PW: Huwezi kabisa kujua.
  T/L, Unajua ku copy na kupaste? Pamoja na kusave?
  NDIYO.
  Unafahamu Flash DISK?

  KESI Inaendelea, tutaendelea kuwapa yanayojiri   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Hiyo kesi ni tamu sana! ccm watajibeba!!!
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ccm watajuta
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kweli ccm imeishiwakwani font inayotumika sana kwenye document ni ipi...nijuavyo mimi ni Times new Roman na font size 12 na line spacing ni double hivyo sitegemei kushangaa ni kikta dcument tano zenye vitu hivyo vimefanana....
   
 5. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  duh kweli nchi inatafunwa na wajinga sasa kesi kama hii eti ya nini?
   
 6. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha kwa Kweli! yaani kesi ni yakupoteza muda! na kutumia hovyo rasilimali zetu.
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mahakama haiko huru otherwise Kesi ingekuwa imeishia hapo
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Wana Cdm hutawaona magamba kwenye thread za maana kama hizi wanakimbilia udini tu kama wakina Ritz na wenzake hapa wanapita tu wanasema kwa aibu "no comment"
   
 9. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,207
  Likes Received: 3,621
  Trophy Points: 280
  Kwa nn kesi kama hii MAHAKAMA haiitaji kama ipo NULLIFIED?Why tutumie hela zetu haba za kodi kwa kesi kama hii?
   
 10. E

  ESAM JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Subiri hukumu uone maana nasikia kuna mkakati wa kuhakikisha Lissu anadondoka, lakini kwa hii kesi jaji hana namna ya kuwafurahisha magamba. Maana yule wa Lema alisingizia maadili lakini hii ya Lissu ni nyaraka ambayo ni ngumu sana kudhibitisha namna zilivyoathiri matokeo
   
 11. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,997
  Trophy Points: 280
  ni Kupoteza Fedha za Serikali
  ni Kupoteza Muda wa kesi za maana kusikilizwa
  ni kuidharirisha Mahakama na tasnia ya sheria kwa ujumla na upana wake
   
 12. p

  pstar01884 Senior Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hahahahaha. Híi kesi ni ful burudani. Big up TL. Unawabana kisawasawa
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Shahidi amekiri analipwa kila anapokuja kutoa ushahidi
  Hii pia ni dhahiri kuwa hata ushahidi wanaoutoa ni wa kutengenezwa
   
 14. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Subiri hukumu itakapotoka ndipo utakaposhangaa, sisi watu wa Arusha tumekwishashangaa ya Mussa (Lema) tunasubiri kustaajabu ya firauni (Lisu).!!!
   
 15. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hivi hizi fedha za kuendesha hizi kesi zinatoka wapi? Kesi za msingi zipo pending tunabaki kusikiliza pumba
   
 16. m

  matawi JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Magamba huenda wakaomba jaji mwingine maana huyu watadai ni mchadema
   
 17. s

  seifkud Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HUKU SUMBAWANGA NAKO KESI IPO HIVI:
  Mlalamikaji Ndugu NORBERT YAMSEBO - CHADEMA Mlalamikiwa Ndugu Aeshi Hilali - CCM (Mbunge)

  Mlalamikaji aliwaleta mashahidi 19 Mahakamani. Na mlalamikiwa alileta Mashahidi wanne kumtete.
  TUHUMA:
  1. Shahidi aliieleza Mahakama Jinsi Mlalamikiwa alivyotoa Rushwa ya Mifuko 20 ya Sementi kwa Kanisa Katoliki Kigango cha Katumba - Parokia ya Pito - Sumbawanga
  2. Shahidi wa pili alirudia ushahidi huo kwa kueleza alivyokabidhiwa mifuko hiyo ya Sementi iliyotolewa kwa Kanisa hilo kwa masharti ya waumini wamchague katika Uchaguzi wa Ubunge kwa kuwa yeye ni Mgombea wa nafasi hiyo.
  3. Shahidi wa Tatu alitoa ushahidi juu ya Rushwa ya Mlalamikiwa kutoa Tsh 100,000/= na Bati 200 kwa Kanisa Katoliki Kigango cha Mtibwa - Sumbawanga, kwa sharti la kuchaguliwa
  4. Shahidi wa NNe alitoa ushahidi kuhusu Mlalamikiwa kununua Pombe ya Kienyeji kwa ajili ya Wana kijiji cha Pito-Sumbawanga kwa masharti ya kumchagua
  5. Shahidi wa Sita alizungumzia kuhusu mlalamikiwa kutoa Zawadi za Baiskeli kwa Vijana katika kijiji cha Pito
  6. Shahidi wa Saba alieleza namna Mlalamikiwa walivyota Tsh. 2,500 kwa vijana 200 katika ukumbi wa shule ya msingi Kantalamba Mazoezi.
  7. Jinsi kura zilivyobadilishwa katika kituo cha Kata ya Katandala - Sumbawanga na kusomwa tofauti katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi
  8. Jinsi Masanduku yalivyocheleweshwa kwa massa 12 kufika ofisi ya Msimamizi kutoka kituo kikuu cha kata ya katandala kwende ofisi ya msimamizi sehemu yenye umbali wa kilomita 1.5 (moja na nusu)

  MLALAMIKIWA WA MAGAMBA - CCM
  Hakuwa na watetezi; alilazimika kujitetea mwenyewe kwa kusema hayo yote ni "UONGO"

  Mniwie radhi kwa kuwajuza habari ya kesi hii katika blog isiyo mantiki na yangu. nimefanya hivi makusudi ili mpate majumuisho ya kesi za uchaguzi zinavyoendelea. kesi hii itatolewa hukumu tarehe 30/04/2012
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hawajuti wao wanafurahia sana kumpotezea T Lisu mda wake, na hilo ndiyo lilikuwa lengo kuu
   
 19. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hivi haya majambazi (CCM) yanatafuta nini kwa wabunge wetu? Haya majambazi ccm yana roho mbaya sana kuliko hata mnavyodhani na kama mnabisha subirieni katiba mpya yatakavyoifanya, mi naomba Mungu hata ayaue tu yafe yote ili tufanye chaguzi ndogo kwani yanaiba haki za wabunge wetu makini kama lema, pia yanzidi kuiba rasilimali zetu na huku yakijitahidi kuwatoa makamanda wote mjengoni.
  NI HERI KJIUNGA NA FREEMASONS KULIKO HAYA MAJANGIRI CCM KWANI KAMA KUNA MTU ANAIPENDA CCM BASI MI NIPO SURE 100% HUYO MTU SIO TIMAMU.
   
 20. l

  luckman JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  hatuwezi kupata ufumbuzi wa haya matatizo kwa njia rahisi rahisi, lazima tuamue ili wajue kuwa tumefika kikomo!
   
Loading...